Advertising

  • Matunda

    faida ya tunda la KITZ
  • Matunda

    kula matunda kwa wingi
  • GYm

    Mazoezi muhimu kwa afya
  • Mazoezi

    dada anaimarisha misuli
  • Jovago

    Promoo siku ya watendao

February 3, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:21 PM | Be the first to comment!

TIBA ZA KISUKARI: CHAKULA NA MAZOEZI KWA MGONJWA WA KISUKARI



                                                      kwa waume tuu 
Hapo zamani, kabla ya uvumbuzi wa insulin (1921), ugonjwa wa kisukari, Type 1 Diabetes, ulikuwa ni ugonjwa ulioua watu wengi sana miaka michache tu baada ya mtu kuupata ugonjwa huo. Lakini sasa mambo yamebadilika kwa kiasi kikubwa sana. Mtu mwenye ugonjwa huu anaweza kuishi maisha ya kawaida kabisa, ili mradi anakuwa na mpango mzuri wa chakula, mazoezi ya kutosha na anatumia insulin. Kuwa ni mgonjwa wa kisukari maaana yake ni kubali namna ya kuishi na siyo kushindwa kufanya jambo lo lote lile ulilokusudia. Unaweza kufanya biashara zako, kushiriki michezo na kufikia malengo yako bila tatizo lo lote.
Kuna orodha ya watu wengi waliokukwa na kisukari na wakafanya vizuri katika michezo, siasa, uigizaji wa filamu, muziki, uandishi wa habari n.k. kinachotakiwa ni mpango wa kula, mazoezi ya kutosha na kuzingatia tiba unayopewa na daktari wako. Hakuna sababu KAMWE ya kushindwa kufikia malengo yako. Mfano mzuri ni Sir Steven Redgrave, mwanamichezo aliyeweza kunyakua medali za dhahabu katika michezo ya Olympiki kwa miaka mitano mfululizo akiwa mwathirika wa Type 1 Diabetes kuanzia mwaka 1997.
Mgonjwa wa kisukuri anapaswa kuchukua vipimo mara kwa mara ili kujua kiwango cha sukari alicho nacho, anapaswa vilevile kuhakikisha kuwa anapima blood pressure na kudhibiti kiwango cha cholesterol kwani vinaweza kumsababishia mgonjwa ya moyo.

Kisukari Cha Juu Na Kisukari Cha Chini

Mgonjwa anatakiwa ahakikishe kiwango chake cha sukari katika damu hakibadiliki sana. Kuwa na kiwango kidogo cha sukari katika damu (Hypoglycemia) kuna madhara madhara mengi katika mwili wa mgonjwa kama vile ilivyo kwa mgonjwa kuwa na kiwango kikubwa cha sukari katika damu (Hyperglycemia).

Mpango Wa Chakula Kwa Mgonjwa Wa Kisukari


Mgonjwa wa kisukari hana masharti ya ajabu kuhusu chakula anachotakiwa kula, kimsingi anaweza kula chakula cho chote anachopenda. Kuna mambo matatu ambayo yanabidi kuangaliwa katika kuweka kiwango cha sukari cha mgonjwa kwenye kiwango kinachofaa. Mamboo hayo ni:
  • Ni chakula gani
  • Chakula hicho kinaliwa kwa kiasi gani
  • Chakula hicho kinaliwa muda gani
Watalaamu wa afya na mambo ya chakula wanabainisha kwamba chakula kinachotakiwa kuliwa kwa wingi zaidi ni chakula chenye wanga (carbohydrates), kikifuatiwa na mboga na matunda, kisha chakula chenye protini na mwisho ni chakula chenye mafuta (fats). Wataalamu na washauri wa magonjwa ya kisukari wanamshauri mgonjwa wa kisukari kupata chakula kwa mpango huo huo.

Chakula Chenye Wanga

Chakula chenye wanga hupatikana zaidi kutoka kwenye nafaka, mboga, maziwa ya mgando na matunda.
Mwili wa binadamu huhitaji chakula chenye wanga, hatuwezi kuishi bila chakula cha aina hii. Mwili hubadilisha wanga na kuwa glucose-aina ya sukari ambayo hutumiwa na seli za mwili kwa ajili ya kupata nguvu na kukua.
Imeonekana kuwa mtu akila kiasi kile kile cha chakula chenye wanga na muda ule ule kila siku, anakuwa na nafasi kubwa sana ya kudhitibi kiwango chake cha sukari katika mwili wake. Ni muhimu kuhakikisha kuwa mgonjwa haruki mlo wo wote kwani kufanya hivyo kutasababisha badiliko kubwa la kiwango cha sukari katika damu kitu ambacho kinatakiwa kikwepwe kwa mgonjwa wa kisukari. Kuwa na ongezeko la glucose katika damu ambalo ni la kawaida kunasaidia kuweza kujua namna ya kuweka uwiano kati ya chakula, dawa na mazaoezi ya mwili na hivyo kudhibiti kiwango cha sukari katika mwili wa mgonjwa.
Uwiano mzuri wa chakula chenye wanga, protini na mafuta umeonekana kuwa:
  • Wanga asilimia 45-65
  • Protini asilimia 15-20
  • Mafuta asilimia 20-35
Kuchanganya aina tofauti tofauti za nafaka, matunda na mboga kumeonyesha kusaidia zaidi na mboga zinasidia kupunguza sukari mwilini kwa sababu ya nyuzinyuzi zake. Hilo pia ni sahihi kwa nafaka ambazo ni nzima, zile ambazo hazikukobolewa.

Mazoezi Ya Mwili Kwa Mgonjwa Wa Kisukari


Mazoezi ya mwili kwa mtu anayeishi na tatizo la kisukari ni muhimu kwa sababu zifuatazo:
  • yanasaidia katika kudhibiti kiwango cha sukari katika mwili
  • yanasaidia kupunguza wa mwili
  • yanasaidia kudhibit blood pressure
  • yanasaidia kuweka cholesterol kwenye kiwango kizuri
Pamaoja na faida hizi hapo juu, mazoezi pia yanasiadia kupata usingizi mzuri na kupunguza msongo wa mawazo. Inashauriwa kufanya mazoezi angalau kwa siku tano katika wiki na mazoezi hayo yawe ya kawaida, siyo ya nguvu, ambayo yatafanywa kwa muda usiopungua nusu saa kila siku. Mazoezi ambayo unaweza kuyafanya ni pamoja na kutembea kwa mwendo waw haraka, kuogelea, kuendesha baiskeli kwenye sehemu ya tambalale au milima ya kadri, kucheza muziki au hata kukata majani kwenye bustani.
Kama hujafanya mazoezi kw muda mrefu, anza na mazoezi madog na kuongeza viwango taratibu. Zingatia kuwa mazoezi yawe kama ya nusu saa kila siku na yafanywe angalau kwa sikumara tano katika wiki na siyo mazoezi ya saa mbili mara moja kwa wiki.
Unaweza kujiunga na gymn sehemu ambayo utapata mataalamu wa kutoa mazoezi kwa watu wemye matatizo mbalimbali. Kupata mtu wa kukusaidia na kukuelekeza katika mazoezi kutakupa ari ya kufanya mazoezi kwa umakini zaidi. Isitoshe, gymn zina vifaa vya kisasa vya kukupa vipimo vya mazoezi yako na maendeleo yako.

Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:16 PM | Be the first to comment!

UJUE UGONJWA WA KISUKARI NA TIBA ZAKE





Ugonjwa wa Kisukari ni hali ambayo hutokea wakati sukari katika damu inapokuwa nyingi kupita kiwango cha kawaida kwa muda mrefu. Sukari hutumiwa na mwili ili kupata nishati lishe. Ili mwili uweze kutumia sukari inayotokana na vyakula, unahitaji kichocheo cha insulin. Insulin husaidia sukari kuingia kwenye chembechembe hai ili kutengeneza nishati lishe. Ugonjwa wa kisukari unasababishwa na kichocheo hiki kupungua au kutofanya kazi kama inavyotakiwa, hivyo kiwango cha kisukari kinabaki kikubwa kwenye damu kwa sababu sukari haikuwezeshwa kuingia kwenye chembechembe hai za mwili.
Tafiti za ugonjwa wa kisukari zinaonyesha kuwa mwaka 2007 kulikuwa na wagonjwa 246 milioni duniani. Takwimu za mwaka 2012 zinaonyesha kuwa kulikuwa na wagonjwa 371 milioni ulimwenguni kote, Takwimu za mwaka 2013, zinaonyesha kuwa kulikuwa na wagonjwa 382 duniani kote.Ifikapo mwaka 2035 kutakuwa na wagonjwa 592 millioni. Katika bara la Afrika kulikuwa na wagonjwa wa kisukari 19.8 millioni mwaka 2013 na wataongezeka mpaka million 41.4 ifikapo mwaka 2035, ambapo nusu ya wagonjwa hawa walikuwa hawajaanza matibabu. Asilimia 80 ya wagonjwa wote wa kisukari ulimwenguni wanaishi katika nchi zinazoendelea, ikiwemo Tanzania.
Utafiti uliofanyika mwaka 2012 na kuhusisha wilaya 50 nchini Tanzania ulionyesha ya kuwa asilimia 9.1 ya Watanzania wenye umri wa miaka 25 na kuendelea wana ugonjwa wa kisukari. Katika nchi 10 zinazoongoza kwa kisukari Barani Afrika Tanzania inashika nafasi ya 8.
Dalili za Kisukari
Mara nyingi, watu wengi hawajitambui ya kuwa wana ugonjwa huu. Wengine wanakuwa na dalili lakini hawachukui hatua mapema. Dalili za kisukari ni rahisi kuzitambua nazo ni: kiu isiyoisha, kukojoa mara kwa mara, kupungua uzito, kusikia njaa kila wakati na mwili kukosa nguvu. Ukiwa na dalili hizi nenda hospitali ukapime sukari.
Mgonjwa pia anaweza kuona dalili ya kuchoka haraka, kupungua uzito, vipele mwilini ambavyo kitaalamu huitwa diabetic dermadromes.
Mgonjwa wa kisukari pia huwa katika hatari ya kupata maambukizi katika kibofu cha mkojo, ngozi na kwa wanawake sehemu za siri. Aidha kuna dalili maalumu ambazo hutokea kwa wagonjwa wa kisukari iwapo mgonjwa atapatwa na mojawapo ya madhara (complications) ya ugonjwa huo.
Madhara hayo ambayo hujulikana kwa kifupi DKA hutokea kwenye aina ya kwanza ya kisukari na huwa na dalili zifuatazo: Mgonjwa kutoa harufu ya acetone inayofanana kidogo na harufu ya pombe.
Mgonjwa pia hupumua kwa haraka na kwa nguvu, kujihisi kichefuchefu, kutapika, kuhisi maumivu ya tumbo na kupoteza fahamu. Kupoteza fahamu mgonjwa kunakoitwa Hyperosmolar Non-ketotic coma hutokea kwenye kisukari cha aina ya pili ambapo mara nyingi husababishwa na upungufu wa maji mwilini.
Tiba ya ugonjwa wa kisukari
Kwa Bahati mbaya ugonjwa wa Kisukari hauna tiba kamili hivyo pale unapokupata utaendelea kuwa nao lakini ugonjwa wa kisukari unaweza kudhibitiwa na malazi mazuri, virutubisho, mazoezi na tiba mbadala ya ugonjwa wa kisukari inayotakiwa kuifanya kabla ya tatizo halijawa kubwa.
Kwa hali ya kawaida wataalamu wa afya hupendekeza lishe ambayo si tiba ya ugonjwa wa kisukari lakini unaweza kurudisha virutubisho muhimu ambayo vinaweza kukosekana kutokana na ugonjwa wa kisukari.
Bidhaa za afya za Optimum Diabetics – 80 pointi. Kisukari optimum zimekuwa zikiandaliwa na kutumika kutoa msaada wa lishe kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari.
Kila kuongezeka kwa kinga ni lazima kukamilisha, full-potency ya uundaji wa vitamini, madini sanifu na Extracts ya mitishamba hasa kwa mara zote kula chakula bora kitokanacho na optimum Diabetics Afya Supplement ambayo hutoa virutubisho vinavyokosekana mwilini na kama ikitumika vizuri kwa miezi sita tatizo la Kisukari hupungua kabisa namara nyingine Kuisha kwani lishe hii inasaidia kwa asilimia 80%.
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:13 PM | Be the first to comment!

Ugonjwa wa kisukari ni nini




KISUKARI ni moja ya magonjwa yanayoathiri watu wengi siku hizi nchini mwetu na hata nje. Kati ya hao, wengi huishi na ugonjwa huo kwa muda mrefu na kuja kugundua kwamba wana kisukari baada ya muda wa kama miaka mitano hivi, baada ya mwili kuanza kuonesha dalili kuu za kisukari.
Ndani ya kipindi hicho cha miaka mitano, tayari mwili unakuwa umepoteza baadhi ya uwezo wake katika macho, figo, fizi na neva za fahamu. Kisukari hakina dawa ya kutibu kabisa, bali vipo vichocheo (hormone) na dawa zinazosaidia kurekebisha kiwango cha sukari mwilini.
DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI
Baadhi Ya Hizo Ni ;
Kiu Ya Maji Isiyoisha
Njaa Kali,
Kwenda Haja Ndogo Mara Kwa Mara
Vidonda Au Michubuko Kuchukua Muda Mrefu Kupona. Nyingine Ni Ngozi Kuwa Kavu Na Kuwasha,
Mgonjwa Kupoteza Uzito Bila Sababu,
Kuwa Na Ukungu Machoni,
Kuchoka Kusiko Kwa Kawaida,
Hisia Kupungua Katika Vidole Na Viganja Mikononi Na Miguuni Na Kuwa Na
Ukungu Katika Fizi, Ngozi Na Kibofu Cha Mkojo.
Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa Na Uume Kutoku Simama.
Mwanamke Kujifungua Mtoto Mwenye Uzito Wa Zaidi Ya Kilo Nne Na Aliyekuwa Na Kisukari Cha Ujauzito Anaangukia Pia Kwenye Kundi Hilo, Sawa Na Wale Wanaokuwa Wamepata Ajali Na Kuumia Sehemu Za Tumboni Au Kula Chakula Chenye Sumu Ambacho Kinaweza Kuumiza Kongosho.
MADHARA YA KISUKARI
Watu Wenye Kisukari Wapo Katika Hatari Zaidi Ya Kupatwa Na :
Magonjwa Ya Moyo,
Kiharusi,
Matatizo Na Kuharibika Kwa Kibofu Cha Mkojo,
Shinikizo La Juu La Damu
Upofu
Kufa Neva Za Fahamu,
Uharibifu Katika Fizi Na Ugonjwa Wa Fangasi.
Mtu Anapokuwa Na Kisukari, Mzunguko Wa Damu Miguuni Hupungua Na Hii Ndiyo Sababu Kubwa Ya Kufa Kwa Neva Za Fahamu Na Hivyo Mtu Kukosa Hisia Katika Eneo Hilo La Mwili.
Read More