Advertising

  • Matunda

    faida ya tunda la KITZ
  • Matunda

    kula matunda kwa wingi
  • GYm

    Mazoezi muhimu kwa afya
  • Mazoezi

    dada anaimarisha misuli
  • Jovago

    Promoo siku ya watendao

February 3, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 8:46 PM | Be the first to comment!

FAHAMU KANSA YA DAMU (LEUKEMIA)


Leukemia ni saratani inayoshambulia tishu za mwili zinazohusika na utengenezaji wa damu zikiwemo supu ya mifupa (bone marrow) na mfumo wa lymph (lyphatic system). Kwa maneno rahisi, leukemia humaanisha saratani ya damu. Kuna aina mbalimbali za leukemia, nyingine zikiathiri watoto na nyingine zikiathiri zaidi watu wazima.
Kwa kawaida leukemia huanzia kwenye chembe nyeupe za damu yaani white blood cells, ambapo mwili huzalisha kiwango kikubwa cha seli zenye maumbo mabaya ambazo hazina uwezo wa kufanya kazi zake sawasawa. Kazi ya chembe nyeupe za damu ni kulinda mwili dhidi ya vimelea waletao maradhi mbalimbali.
SABABU
Leukemia husababishwa na nini?
Kama zilizo kwa aina nyingi za saratani, mpaka sasa chanzo halisi cha leukemia hakijulikani. Hata hivyo, wanasayansi wanadai kuwa leukemia hutokea kutokana na mkusanyiko wa vyanzo mbalimbali vikiwemo vinavyohusu sababu za kinasaba (genetic factors) na kimazingira.
Kwa ujumla, leukemia hutokea pindi chembe nyeupe za damu zinapobadilika muundo wake wa kinasaba yaani viasili vyake vya DNA, ambavyo kwa kawaida hubeba maelekezo yanayoifanya seli yeyote ya kiumbe hai iweze kuishi, kutenda kazi zake, kujizaa na hata kufa, vinapobadilika maumbile na muundo wake kutokana na sababu mbalimbali. Kitendo cha kubadilika kwa maumbile na muundo wa DNA hujulikana kama mutation. Ndiyo kusema basi, seli yeyote iliyopatwa na tatizo hili huwa na tabia ya kukua kwa haraka na kujizaa (kujigawa) kwa kasi zaidi kuliko kawaida, na pindi inapofikia muda wake wa kufa seli hiyo hugoma kufa badala yake huendelea kujizaa zaidi hatimaye kusambaa kwa wingi katika mfumo mzima wa damu, hali inayosababisha saratani ya damu.
VIHATARISHI
Je, kuna vihatarishi vya leukemia?
Ndiyo vipo! Pamoja na kwamba chanzo halisi cha saratani ya damu hakijulikani, lakini kuna mambo ambayo humuongezea mtu hatari ya kupata ugonjwa wa saratani ya damu.
Mambo ambayo yanaweza kuongeza uwezekano wa kupata saratani ya damu ni pamoja na:
1.Historia ya matibabu ya saratani hapo kabla: Watu ambao wamekuwa kuwa na aina nyingine za saratani hapo awali, na wakati wa matibabu wakapewa tiba ya mionzi au madawa makali ya saratani, wapo katika hatari kubwa ya kupata saratani ya damu kwa sababu baadhi ya dawa hizi pamoja na mionzi huwa na tabia ya kuathiri pia seli nyeupe za damu pamoja na tishu zinazotengeneza seli hizo.
2.Kuwa na magonjwa mengine ya vinasaba: Ingawa haieleweki sawasawa uhusiano wake ulivyo, kuwa na baadhi ya magonjwa ya kinasaba kama vile ugonjwa wa Down syndrome, yasemekana huongeza uwezekano wa muathirika kuugua pia ugonjwa wa saratani ya damu.
3.Baadhi ya magonjwa mengine ya damu: Watu wenye magonjwa mengine ya damu kama vile ugonjwa wa damu unaoshambulia tishu za supu ya mifupa na kuzifanya zizalishe seli nyingi za damu bila uwiano unaotakiwa yaani myelodysplastic syndromes, huongeza pia uwezekano wa mtu kuugua saratani ya damu.
4.Kupigwa na kiasi kikubwa cha mionzi: Watu ambao wamewahi kupigwa na kiasi kikubwa cha mionzi kama vile mlipuko wa mabomu au kulipuka kwa vinu na mitambo ya nuklea (nuclear reactors), wana hatari kubwa zaidi ya kupata saratani ya damu pamoja na saratani nyingine.
5.Kupigwa/kutumia baadhi ya kemikali: Watu waliowahi kukumbana na baadhi ya kemikali kama vile benzene au zile zinazotumika kwenye viwanda vya kuyeyusha vyuma au kutengeneza magurudumu au mabomba ya plastic, nao pia wapo katika uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya damu.
6.Uvutaji sigara: Jambo hili pia huongeza uwezekano wa kupata aina mojawapo ya saratani ya damu.
7.Kuwa na historia ya ugonjwa huu katika familia: Watu ambao, baadhi ya ndugu zao wamewahi kuugua ugonjwa huu, nao pia wana uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya damu. Hata hivyo, hii haina maana kwamba leukemia inaambukizwa isipokuwa kuna uhusiano wa kifamilia tu katika kusababisha ugonjwa huu.
Jambo moja la kufahamu ni kuwa, wapo watu wengi ambao wamewahi kukumbana na vihatarishi nilivyovieleza hapo juu bila kupata leukemia, kadhalika wapo waliopata leukemia bila kukumbana na kihatarishi hata kimoja kati ya hivi. Kwahiyo. Uwepo wa vihatarishi hivi haimaanishi kuwa ni lazima mtu apate leukemia isipokuwa inaongeza uwezekano wa kupata ugonjwa huu.
Makundi ya leukemia
Wataalamu wa afya wanaiainisha leukemia katika makundi mbalimbali kulingana na kasi ya kusambaa kwa ugonjwa pamoja na aina ya chembe damu zilizoathirika.
Kulingana na aina ya chembe damu zilizoathirika, leukemia inaweza kugawanywa katika makundi makuu mawili, ambayo ni:
Leukemia inayoathiri zaidi chembe damu zinazounda mfumo wa lymph ambayo kwa kitaalamu huitwa Lymphocytic leukemia. Mfumo wa lymph au lymphatic system ndiyo unaolinda mwili wako dhidi ya maradhi na maambukizi mbalimbali kama vile VVU n.k. Chembe damu zinazohusika hapa huitwa lymphocytes.
Leukemia inayoathiri zaidi chembe/seli zinazounda chembe damu nyingine za mwili yaani kwa kitaalamu Myelogenous leukemia. Aina hii ya leukemia huathiri chembe zinazoitwa myeloid cells, ambazo ndizo huzaa chembe nyekundu za damu, chembe nyeupe za damu pamoja na chembe sahani. Chembe nyekundu husaidia kusafirisha hewa safi ya oksijeni mwilini na kutoa hewa chafu ya kabondioksaidi, chembe nyeupe hupambana na vimelea wa magonjwa mbalimbali kama vile uti wa mgongo, minyoo, kifua kikuu, nk., wakati chembe sahani husaidia kuganda kwa damu pindi mtu unapoumia au kujikata.
Njia ya pili ya kuainisha makundi ya leukemia ni kwa kuangalia kasi ya kusambaa kwa ugonjwa wa saratani ya damu mwilini mwa muathirika. Kwa njia hii, kuna makundi makuu mawili ya leukemia, ambayo ni:
1.Leukemia inayosambaa kwa haraka au wataalamu wanaita acute leukemia. Katika aina hii, chembe damu huwa changa, zenye mambo mabaya yasiyo ya kawaida, na zisizoweza kufanya kazi zao vizuri. Lakini mbaya zaidi, hujigawa na kuzaliana kwa kasi kubwa kiasi cha kusambaa na kujazana katika damu kwa muda mfupi sana.
2.Leukemia inayosambaa taratibu au kwa kitabibu chronic leukemia. Katika aina hii, chembe damu huwa zimekomaa na zenye uwezo wa kujigawa na kuzaliana taratibu na hata kufanya kazi zake kama kawaida. Chembe damu huweza kuishi kwa muda mrefu bila hata mgonjwa kuonesha dalili yeyote ya kuugua leukemia.
AINA ZA LEUKEMIA
Bila kujalisha kasi ya kusambaa kwa ugonjwa au aina ya chembe damu iliyoathirika, leukemia inaweza kugawanywa katika aina zifuatazo:
1.Leukemia inayosambaa kwa haraka huku ikishambulia chembe damu zinazounda mfumo wa lymph yaani Acute lymphocytic leukemia (ALL). Aina hii huwapata zaidi watoto wenye umri mkubwa kidogo ingawa pia inaweza kwa kiasi fulani kuwapata hata watu wazima.
2.Leukemia inayosambaa kwa haraka huku ikishambulia chembe/seli zinazounda chembe damu nyingine za mwili yaani Acute myelogenous leukemia (AML). Aina hii ya leukemia inaongoza kati aina nyingine zote na huwapata watoto pamoja na watu wazima.
3.Leukemia inayosambaa taratibu huku ikishambulia chembe damu zinazounda mfumo wa lymph yaani chronic lymphocytic leukemia (CLL). Aina hii huwapata zaidi watu wazima, na nadra sana kutokea kwa watoto. Wagonjwa wa aina hii ya leukemia huweza kuishi vizuri kabisa bila kuwa na dalili zozote zile.
4.Leukemia inayosambaa taratibu huku ikishambulia chembe/seli zinazounda chembe damu nyingine za mwili yaani chronic myelogenous leukemia (CML). Watu wazima ndiyo waathirika wakubwa zaidi wa aina hii ya saratani ya damu. Mtu mwenye aina hii ya leukemia anaweza akapata dalili chache au asiwe na dalili kabisa kwa miezi hata miaka kabla ya ugonjwa kufumuka ghafla na kuanza kumshambulia.
DALILI.
Dalili za leukemia hutofautiana kutoka aina moja mpaka nyingine. Hata hivyo, dalili za jumla za leukemia ni pamoja na;
1.Homa au kujihisi baridi
2.Uchovu na ulegevu wa mwili
3.Maambukizi ya mara kwa mara
4.Kupoteza uzito bila kukusudia
5.Kuvimba tezi za mitoki
6.Kuvimba wengu (splenomegaly)
7.Kuvimba ini (hepatomegaly)
8.Kutokwa damu kirahisi na kupata michubuko ya mara kwa mara
9.Kuvilia kwa damu chini ya ngozi
10.Kutokwa jasho kupita kiasi hasa nyakati za usiku
11.Kuhisi maumivu ya mifupa
12.Kupungukiwa damu mara kwa mara
Mara nyingi dalili za Leukemia hazipo wazi na ni rahisi sana kwa mgonjwa kuchanganya na dalili za magonjwa mengine,Kama malaria,TB na HIV, hivyo ni vema kuwahi hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa kina na vipimo, mara tu uonapo dalili zilizotajwa hapo juu.
Uchunguzi na vipimo
Ni rahisi kwa daktari kugundua leukemia inayosambaa kwa kasi (acute leukemia) kuliko ile inayosambaa taratibu (chronic leukemia). Mara nyingi leukemia inayosambaa taratibu hugunduliwa mgonjwa anapoenda hospitali kwa ajili ya matibabu ya kitu kingine tofauti.
Pamoja na kukuuliza historia yako kwa lengo la kufahamu dalili na vihatarishi vya ugonjwa huu, daktari pia atakufanyia uchunguzi wa kina wa mwili kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa viashiria vya saratani ya damu kama vile ngozi nyeupe (katika viganja, macho au ulimi), kuvimba kwa tezi za mitoki, kuvimba wengu na ini; kuvilia damu katika ngozi, michubuko, au kama una dalili zozote za upungufu wa damu mwilini.
VIPIMO.
Vipimo utakavyofanyiwa ni pamoja na
1.Kipimo cha damu almaarufu kama Full Blood Picture ambacho huonesha kiwango cha kila chembe damu iliyopo mwilini. FBP huonesha kama chembe damu nyeupe zimeongezeka ama la, sambamba na chembe damu nyingine. Pia huonesha kiasi cha wingi wa damu, na iwapo mgonjwa ana upungufu wa damu ama la. Kwa ujumla wagonjwa wa leukemia huwa na ongezeko kubwa la chembe damu nyeupe zilizo changa, wakati chembe damu nyekundu pamoja na chembe sahani huwa chini.
2.Kipimo cha supu ya mifupa (bone marrow biopsy) hufanyika kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa seli za saratani. Kipimo hiki hufanyika kwa kuchukua sehemu ya mfupa wa nyonga au paja, kisha kuepelekwa maabara kwa uchunguzi. Biopsy husaidia kutofautisha kati ya leukemia na magonjwa mengine ambayo husababisha kuwepo kwa ongezeko la chembe damu nyeupe. Kwa maneno mengine, hiki ni kipimo tosha cha uthibitisho wa kuwepo kwa leukemia.
Vipimo vingine ni pamoja na vile vinavyoonesha utendaji kazi wa figo (renal function tests) na ini (liver function tests).
Baadhi ya madaktari hupenda pia kufanya kipimo cha uti wa mgongo (lumbar puncture) ili kuchunguza uwepo wa chembe za leukemia katika maji ya uti wa mgongo (spinal fluid).
MATIBABU
Matibabu ya leukemia hutegemea mambo mbalimbali kama vile hatua ugonjwa ulipofikia, umri wa mgonjwa, hali ya jumla ya kiafya ya mgonjwa, na aina ya leukemia.
Leukemia inaweza kutibiwa kwa kutumia:
Dawa za kuua seli za saratani (chemotherapy): Hii ni njia kuu ya matibabu ya leukemia, ambapo dawa hutumika kuua seli zenye saratani. Kutegemeana na aina na hatua iliyofikiwa na ugonjwa, mgonjwa anaweza kupewa dawa moja au mkusanyiko wa dawa kadhaa tofauti tofauti kwa muda fulani.
Tiba ya mionzi (radiotherapy): Njia hii hutumia mionzi yenye nguvu kubwa iliyoelekezwa kwa ajili ya kuua chembe za leukemia na kuzuia ukuaji wake. Mionzi inaweza kutolewa katika eneo fulani maalum la mwili ambapo kuna kusanyiko la chembe za leukemia au mwili mzima.
Dawa zinazoelekezwa mahsusi kuua viasili vya seli za saratani (targeted therapy): Dawa hizi hufanya kazi maalum ya kuzuia seli kuzaliana au kujigawa kwa kuingilia mfumo wake wa utendaji kazi.
Tiba ya upandikizaji (stem cell transplant): Tiba hii hufanyika kwa ajili ya kurejesha sehemu ya supu ya mfupa iliyoharibika kwa kuweka supu mpya. Kabla ya tiba hii, mgonjwa hupewa dawa za kuua seli za saratani au mionzi ili kuua kabisa eneo lililoathiriwa kisha supu mpya hupandikizwa. Mara nyingi supu hii hutoka kwa mtu mwingine (donor) au inaweza ikatoka kwa mgonjwa mwenyewe kwa kuchukua sehemu ambayo haijaathirika.
Na njia nyingine ni tiba ya kuchochea mfumo wa kinga ya mwili kuzitambua, kushambulia na hatimaye kuua seli za saratani (biological therapy).
Nini cha kufanya?
Saratani ya damu ni jambo la kutisha na kusikitisha hususani kwa familia ambayo inamuhudumia mgonjwa wa tatizo hilo. Aidha ni jambo la kuhuzunisha sana kwa wazazi wenye mtoto aliyegunduliwa kuwa na ugonjwa huu. Kwa familia iliyokumbana na tatizo hili ni vema kufahamu nini cha kutarajia na kufanya. Kwa mzazi, hana budi kutafuta taarifa zaidi ya ugonjwa wa mtoto wake, aina ya ugonjwa, hatua iliyofikia na aina za matibabu yanayomfaa mtoto wake. Kwa mgonjwa, ni vema kufuatilia ushauri wa wataalamu wa afya na kuwa makini katika kutoa taarifa ya mabadiliko yeyote unayoyaona kuhusu maendeleo ya afya yako.
Kwa jamii nzima, ni muhimu kujiepusha na vihatarishi vinavyoweza kuongeza uwezekano mtu kupata saratani ya damu
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 8:44 PM | Be the first to comment!

SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI INAPUNGUZA FURAHA KWA WANAWAKE

Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani inayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanawake wengi duniani. Inakadiriwa kuwa asilimia 85 ya vifo hivi hutokea katika nchi zinazoendelea. Kwa Tanzania, wastani wa wanawake 6,241 huugua saratani hii kila mwaka, ambapo 4,355 kati yao hufa, hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la afya duniani (W.H.O) ya mwaka 2010.
Saratani ya shingo ya kizazi ndio saratani ya kwanza kwa wanawake nchini Tanzania, na Saratani namba moja kwa wanawake walio kati ya umri wa miaka 15 hadi 44. Tanzania ina wanawake milioni 10.97 walio na umri wa miaka 15 na kuendelea, ambao wako kwenye hatari kubwa ya kupata saratani hii. Kwa afrika mashariki, asilimia 33.6 ya wanawake wote, wanasadikiwa kuwa na virusi aina ya human papilloma virus ambavyo ndio visababishi vya ugonjwa huu.
Je nini kinasababisha saratani ya shingo ya kizazi?
Maambukizi ya human papilloma virus ndio yanayosababisha saratani ya shingo ya kizazi. Kuna zaidi ya aina 150 ya virusi hivi vya human papilloma virus, ambapo aina tatu (yaani aina ya 26,53,66) ndio venye hatari sana ya kusababisha ugonjwa huu, aina ya 16 na 18 ndivyo vinavyojulikana kusababisha zaidi ya asilimia 70 ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi. Virusi hivi huambukizwa kwa njia ya kujamiana au kugusana kwa ngozi ya mtu mmoja na mwengine, na huambukiza wanaume na wanawake.
Visababishi vya saratani ya shingo ya kizazi
Kuanza kufanya ngono mapema - Wanawake wanaoanza kujamiana wakiwa na umri wa miaka 16 wako kwenye hatari baadae kupata saratani ya shingo ya kizazi.
Kuwa na wapenzi wengi – Mwanamke mwenye wapenzi wengi au mwenye mwanamume mwenye wapenzi wengi yupo kwenye hatari ya kupata ugonjwa huu. Utumiaji wa kondomu hupunguza hatari ya kupata saratani hii, lakini ikumbukwe ya kwamba kondomu sio kinga ya ugonjwa huu.
Maambukizi ya human papilloma virus.
Uvutaji sigara – Kemikali zilizopo kwenye sigara huchanganyikana na seli au chembechembe za shingo ya kizazi hivyo kuleta mabadiliko katika shingo ya kizazi hatimaye kusababisha saratani.
Utumiaji wa vidonge vya kupanga uzazi kwa muda mrefu hasa wale wanaotumia kwa zaidi ya miaka mitano.
Ugonjwa wa masundosundo (dalili ni matezi na muda mwingine vidonda katika sehemu ya siri ya mwanamke). Hii husababishwa na virusi vya human papilloma virus.
Lishe duni au utapia mlo.
Kuzaa watoto wengi – Wanawake ambao wamepata watoto zaidi ya watano wako kwenye hatari kubwa sana ya kupata saratani ya shingo ya kizazi. Ndio maana mama akishafikisha watoto watano anashauriwa kufunga kizazi.
Umri mkubwa – Baada ya kufikisha umri wa miaka 25, hatari ya kupata saratani hii huongezeka. Wanawake wenye zaidi ya miaka 45 wako kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya shingo ya kizazi.
Uasili wa mtu – Saratani ya shingo ya kizazi huonekana sana kwa watu weusi kuliko watu weupe.
Upungufu wa kinga mwilini – Magonjwa yanayosababisha upungufu wa kinga mwilini kama ukimwi huchangia kupata saratani ya shingo ya kizazi. Hata baadhi ya dawa pia husababisha upungufu wa kinga mwilini, mfano, dawa zinazotolewa baada ya mgonjwa kupewa kiungo cha mtu mwengine kama figo,moyo nk.
Historia ya saratani ya shingo ya kizazi katika familia – Saratani hii pia inahusishwa na kiashiria cha aina ya HLA-B7 ambacho kinaweza kurithishwa kwenye familia ya mgonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.
Matumizi ya dawa aina ya diethystilbestrol (DES).
Kujamiana na mwanaume ambaye hajatahiriwa - Tafiti zimeonyesha ya kwamba wanaume ambao hawajatahiriwa wako katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya human papilloma virus. Hii ni kutokana na uchafu ndani ya gozi linalofunika kichwa cha uume hivyo kuweka mazingira mazuri kwa virusi vya human papilloma virus kustawi na hatimaye kuambukiza mwanamke wakati wa kujamiana.
Dalili na viashiria vya saratani ya shingo ya kizazi
Saratani ya shingo ya kizazi katika hatua za awali haina dalili au viashiria vyovyote.
Dalili au viashiria vya saratani ya shingo ya kizazi ni;
Kutokwa na damu katika tupu ya mwanamke (uke) ambayo sio ya kawaida. Damu hii inaweza kuwa matone, au damu inayotoka katikati ya mzunguko wa hedhi (yaani baada ya hedhi kabla ya hedhi inayofuata) au damu itokayo kwa mwanamke ambae ameacha kupata hedhi.
Kutokwa na damu baada ya kujamiana baada ya tendo la ndoa.
Maumivu wakati wa kujamiana.
Dalili za saratani iliyosambaa ni kama zifuatavyo;
Kupungua kwa hamu ya kula.
Kupungua uzito.
Kuhisi uchovu.
Maumivu ya nyonga.
Maumivu kwenye mgongo.
Maumivu ya mguu.
Mguu mmoja kuvimba.
Kutokwa na damu nyingi kwenye tupu ya mwanamke.
Kuvunjika mifupa.
Kutokwa na mkojo au kinyesi kwenye tupu ya mbele ya mwanamke.
Vipimo vya saratani ya shingo ya kizazi
Pap smear – Chembechembe au seli za shingo ya kizazi huchukuliwa na kuchunguzwa kutumia hadubini. Kipimo hiki pia hutumiwa katika uchunguzi wa wanawake ili kujua kama wamepata saratani ya shingo ya kizazi au la. Wanawake wenye zaidi ya miaka 18 au wale wenye upungufu wa kinga mwilini wanashauriwa kufanya kipimo hiki angalau mara moja kwa mwaka ili wajue afya yao.
Cervical Biopsy – Kipimo hiki huhusisha uchukuaji wa nyama kutoka kwenye uvimbe katika shingo ya kizazi na hupelekwa maabara kuchunguzwa kama kuna saratani au la. Kipimo hiki kinathibitisha uwepo wa saratani.
Colposcopy – Hii ni aina ya darubini inayotumiwa kuchunguza shingo ya kizazi ili kuangalia kama kuna tishu ambayo si ya kawaida. Kipimo hiki kinaweza kufanywa na daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama.
Cone Biopsy – Kipimo hiki hufanywa kwa kuchukua nyama kutoka katika shingo ya kizazi mfano wa koni kwa uchunguzi zaidi na hufanywa katika chumba cha upasuaji mgonjwa akiwa amepewa dawa ya nusu kaputi. Hiki kipimo kinaweza kutumiwa kama njia moja ya kutibu saratani ambayo haijaenea na ambayo ni ndogo sana kuondolewa kwa njia hii. Kuna aina mbili ya kufanya kipimo hiki;
(1) Kukata nyama kutoka katika shingo ya kizazi kwa kutumia nyaya ya umeme inayojulikana kitaalamu kama loop electrosurgical excision procedure (LEEP).
(2) Kukata nyama ya shingo ya kizazi kwa kutumia visu maalum vya upasuaji au laser.
PET Scan – Kipimo hiki pia huweza kuthibitisha uwepo wa saratani na kuangalia maendeleo ya mgonjwa baada ya kupata tiba.
Blood test – Vipimo vya damu, kuangalia wingi wa damu, kwa sababu wagonjwa wengi wanakuwa na upungufu wa damu kutokana na kuvuja damu mara kwa mara.
Picha ya kifua ya X-ray – Kuangalia kama saratani imesambaa kwenye mapafu au la.
CT Scan – Kuangalia kibofu cha mkojo kama kimeathirika au la, na pia kuangalia kama saratani imesambaa kwenye mifupa, ini, figo na sehemu nyingine za mwili.
Makundi ya saratani ya shingo ya kizazi
Saratani ya shingo ya kizazi imegawanywa katika makundi mbali mbali kulingana na TNM ama FGO (Classification) kama ifuatavyo;
Stage 0 – Saratani iliyo kwenye chembechembe au seli za aina ya epithelium lakini haifiki kwenye nyama za ndani za shingo ya kizazi.
Stage 1 – Saratani iliyopo kwenye shingo ya kizazi.
Stage 2– Saratani iliyosambaa hadi kwenye tupu ya mwanamke sehemu ya juu kwa 2/3.
Stage 3 – Saratani iliyosambaa hadi kwenye ukuta wa nyonga na sehemu ya chini ya uke kwa 1/3. Hii inaleta madhara katika figo.
Stage 4 – Saratani iliyosambaa hadi nje ya tupu ya mwanamke na pia husambaa hadi kwenye sehemu nyingine za mwili kama mapafu, figo, mifupa nk.
Tiba ya saratani ya shingo ya kizazi
Tiba ya saratani hii inategemea na kundi na aina ya saratani mgonjwa aliyonayo. Tiba ni kama ifuatavyo;
Tiba ya kuchoma (cauterization) – Tiba hii hutolewa kwa wagonjwa wenye matatizo ya shingo ya kizazi kabla hayajakuwa saratani na hutumia joto kali , umeme, na kemikali kuchoma sehemu iliyoathirika.
Tiba ya dawa (Chemotherapy) – Tiba kwa kutumia dawa za saratani ambazo huuwa chembechembe au seli za saratani ya shingo ya kizazi. Dawa hizi hutolewa kwa mgonjwa ambae saratani imeshasambaa mwilini na inahusisha dawa moja pekee au mchanganyiko wa dawa zaidi ya moja ambazo mgonjwa hupewa kwa njia ya dripu au humeza kupitia mdomoni. Dawa hizi hutumiwa zaidi ya mzunguko mmoja na ni za gharama. Dawa hizi zinaweza kutumiwa ili;
(a) Kutibu saratani
(b) Kuzuia saratani isisambae sehemu nyingine mwilini
(c) Kupunguza kasi ya ukuaji wa saratani
(d) Kupunguza madhara ya saratani
Madhara ya dawa hizi yanatofautiana kulingana na aina ya dawa, muda wa utumiaji, na kiwango cha dawa yenyewe. Madhara yake ni kichefuchefu, uchovu, nywele kunyofyoka (hair loss) nk.
Tiba ya mionzi (radiation therapy) – Tiba ya mionzi kwa kutumia mionzi ya X-ray, gamma na neutrons ambayo huua seli za saratani hii. Mionzi hii haina maumivu na madhara yake ni uchovu, tupu kuwa nyembamba sana (narrowing of vagina) na mgonjwa kupungukiwa na damu.
Tiba ya upasuaji (surgical treatment) – Aina za upasuaji kwa mgonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi ni kama zifuatazo;
Cryosurgery – Mpira maalum (probe) huingiziwa kupitia kwenye tupu hadi kwenye shingo ya kizazi na majimaji ya nitrogen hupitishwa yaliyo na baridi ya -160 0 celsius yenye uwezo wa kugandisha na kuharibu seli za shingo ya kizazi hivyo kuzuia saratani.
Laser surgery – Aina hii ya upasuaji inatumia mionzi ya laser ambayo huchoma seli za shingo ya kizazi ambazo haziko kwenye hali ya kawaida, mionzi hii haiharibu tishu za pembeni na hutumiwa kwa matatizo ya shingo ya kizazi kabla hayajakuwa saratani.
Cone biopsy – Kama nilivyoeleza kwenye vipimo hapo juu.
Simple hysterectomy – Hii inahusisha kuondoa mfuko wa kizazi (uterus) kupitia sehemu ya tumboni au kupitia kwenye tupu ya mwanamke kwa wagonjwa wa kundi I (Stage I). Madhara yake ni ugumba, kuvuja damu, kupata madhara sehemu ya haja ndogo au utumbo na maambukizi kwenye kidonda.
Radical hysterectomy – Hii inahusiha kuondoa mfuko wa uzazi kupitia kwenye tumbo pamoja na tishu za mfuko wa uzazi, sehemu ya juu ya tupu ya mwanamke, na tezi za kwenye nyonga. Mayai (ovaries) na mirija ya uzazi yanabakizwa. Madhara yake ni kama ya hapo juu pamoja na kuleta karaha na maumivu wakati wa kujamiana.
Pelvic exenteration – Huhusisha uondoaji wa kibofu cha mkojo, uke, puru (rectum) na sehemu ya utumbo mpana (colon). Upasuaji huu hutumiwa kwa wagonjwa wenye na saratani iliyojirudia.
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 8:42 PM | Be the first to comment!

DALILI ZA KANSA YA MATITI(BREAST CANCER)





Nijua kuwa wanawake wengi wanajiuliza ni zipi dalili za saratani ya matiti? Dalili ya awali inayoweza kutambulisha saratani ya matiti ni kuwepo kwa uvimbe kwenye titi ambao huwa na hali tofauti na sehemu nyingine za titi. Hata hivyo, si kila uvimbe kwenye titi unaashiria uwepo wa saratani ya matiti. Uvimbe huu huwa mgumu, unaochezacheza au ambao hauko thabiti, ambapo wakati mwingine unaweza kuwa na maumivu makali au kusiwe na maumivu yoyote. Uvimbe huu huwepo zaidi ya mzunguko mmoja wa hedhi kwa wale ambao hawajaacha kupata hedhi. Dalili nyingine ni pamoja na  kuwepo uvimbe kwenye sehemu za kwapa, sehemu ya titi kuingia ndani
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:34 PM | Be the first to comment!

UGONJWA WA KANSA NI NINI?Tiba Ya Kansa

Tiba ya ugonjwa huu wa saratani inatolewa kwa kutegemea aina ya kansa aliyo nayo mgonjwa, kansa hiyo imeenea kiasi gani katika mwili wa mgonjwa huyo, umri wa mgonjwa, afya aliyo nayo na mambo mengine yanayoendana na mgonjwa huyo. Hakuna tiba ya wote na mara nyingine mgonjwa atapewa mchanganyiko wa tiba
na uangalizi. Tiba zilizopo zinaangukia katika makundi yafuatayo: upasuaji, mionzi, chemotherapy, immunotherapy, hormone therapy au gene therapy. Tutapitia kwa kifupi aina hizi za tiba za kansa hapa
chini.
Tiba Ya Kansa Kwa Upasuaji: Tiba ya kansa kwa upasuaji ndiyo tiba ambayo imetumika kwa muda mrefu zaidi kuliko tiba nyingine zote. Endapo kansa ya eneo moja haijaenea kwenye sehemu nyingine ya mwili, mgonjwa anaweza kupona kabisa kwa tiba hii ya uapasuaji. Mafanikio makubwa kabisa ya tiba hii yameonekana katika tiba za kansa za maziwa na kansa za tezi dume. Kansa ikiishaenea toka sehemu moja ya mwili hadi nyingine, tiba hii haiwezi kuondoa seli zote za kansa.
Tiba hii inapotumika kwa sasa hivi kuondoa uvimbe, madaktari huondoa kipande cha seli za kawaida kuzunguka eneo la seli za kansa kuhakikisha kuwa seli zote za kansa zimeondolewa. Mgonjwa hulazilka kubaki kwenye nusu-kauti wakati vipimo vinachukuliwa kuhakikisha kuwa eneo la kida lililoondolewa halina seli za kansa na kwa bahati mbaya wakigundua uwepo wa seli hizo za kansa, humrudia mgonjwa na kukata kipande zaidi.
Maendeleo ya teknolojia sasa hivi yamekuja na kifaa kipya kitwacho IKnife ambacho chenyewe hugundua seli za kansa hivyo kuwawezesha madaktari kujua upeo wa eneo la kulikata na kuondoa seli zote za kansa bila ya kusubiri vipimo vya kwenye maabara.
Tiba Ya kansa Kwa Mionzi: Tiba hii ambayo pia huitwa radiotherapy huondoa kansa kwa kuelekeza mionzi yenye nguvu kwenye seli za kansa. Mionzi hii huziharibu seli hizo na kuzifanya zijiue zenyewe. Tiba hii ya mionzi hutumia mionzi yenye nguvu inayoitwa gamma-rays inayotolewa na machine maalumu.
Tiba za mwanzo kwa kutumia mionzi zilikuwa na madhara makubwa ya kuharibu seli za kawaida lakini maendeleo katika teknolojia yameiboresha tiba hii na sasa mionzi hiyo ina uwezo wa kulenga seli za kansa kwa uhakika zaidi na hivyo kutoleta madhara kwa seli za kawaida. Radiotherapy hutumika kufanya uvimbe unywee au kuharibu seli za kansa (pamoja na kansa za aina ya leukemia na lyphoma). Tiba hii hutumika pia pamoja na tiba nyingine za kansa.
Tiba Ya Kansa Ya Chemotherapy: Chemotherapy ni tiba inayotumia kemikali ambazo zinavuruga tendo la seli za mwili kujigawa na kusababisha seli hizo kujiua zenyewe. Tiba hii hulenga zile seli ambazo zinajigawa kwa haraka na kwa kawaida hutumika kutibu kansa zilizoenea kutoka eneo moja ya mwili hadi eneo jingine
(metastatic cancers) kwa sababu kemikali hizi zina uwezo wa kusambaa katika mwili wote wa mgonjwa. Hii ni tiba ya lazima kwa aina fulani ya kansa za aina ya leukemia na lymphoma.
                                                
hemotherapy hutolewa kwa vipindi ili mwili uweze kupona katikati ya dozi moja na nyingine. Madhara ya tiba hii ni pamoja na
kunyonyoka nywele, kichefuchefu, uchovu wa mwili na kutapika. Ni tiba ambayo mara nyingine hutolewa kwenda sambamba na tiba nyingine za saratani.
Tiba Ya kansa Ya Immunotherapy: Immunotherapy ni tiba inayokusudia kuziongeza kinga za mwili ili mwili uweze kupambana na uvimbe. Sindano inweza kudungwa kwenye eneo lililoathirika ili uvimbe unywee (Local immunotherapy). Namna nyingine ni kuuwezesha mwili wote kuongeza kinga ili kupambana na uvimbe katika sehemu zote za mwili (Systemic immunotherapy). Tiba hii bado ni changa lakini zimeonyesha mafanikio katika kutibu kansa za maziwa.
Utafiti unaendelea na kila siku wanasayansi wanakuja na tiba nyigine na kuzijaribu. Tiba ambazo zipo kwenye majaribio ni pamoja na Gene therapy yenye lengo la kukarabati genes zilizoharibika

Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:31 PM | Be the first to comment!

UGONJWA WA KANSA NI NINI? DALILI ZAKE







Ugonjwa wa kansa una ishara nyingi ambazo hutegemea zaidi kansa hiyo ipo kwenye sehemu gani ya mwili, imekwisha enea kwakiwango gani na ukubwa wa uvimbe wa kansa hiyo. Kansa nyingine huonekana kwa macho au kwa kupapasa juu ya ngozi – uvimbe juu ya ziwa au kwenye korodani huweza kuwa ishara ya kansa. Kansa aina ya melanoma mara nyingi hutambuliwa kutokana na mabadiliko ya vijipele juu ya ngozi. Kansa nyingine hutoa mabaka meupe ndani ya midomo au madoa meupe kwenye ulimi.
Kansa nyingine hutoa dalili ambazo hazionekani dhahiri. Uvimbe wa kwenye ubongo, mathalani, huathiri jinsi mtu anavyoweza kutambua vitu na kansa za kwenye kongosho hazitoi ishara mapema hadi maumivu yatakapoanza pale neva za maeneo ya karibu zitakapoanza kuminywa au shughuli za ini zitakapoathiriwa na
kusababisha ngozi na macho kuwa ya rangi ya njano (jaundice). Ishara nyingine zitaonekana uvimbe utakapoanza kusukuma viungo vya karibu au mishipa ya damu. Kwa mfano, kansa za kwenye utumbo huweza kusababisha kukosa choo kikawaida, kuharisha au kiasi cha kinyesi kinachotolewa. Kansa za tezi dume huathiri ufanyakazi wa kibofu cha mkojo na kusababisha kupta haja ndogo mara kwa mara au kutopata haja ndogo.
 Kwa vile seli za kansa hunyonya nguvu za mwili na kuvuruga mfumo wa kinga za mwili, ishara nyingine za homa, uchovu, kutokwa jasho, kukosa damu, kupungua uzito kusiko na sababu huweza kutokea.
Kansa iliyoenea hadi kwenye maeneo ya ubongo husababisha kizunguzungu na maumivu ya kichwa. Kansa ya mapafu inawezaa kusababisha kukohoa na kupumua kwa shida. Ini linaweza kuwa kubwa na kusababisha ugonjwa wa homa ya manjano, mifupa huweza kuuma na kuvunjika kirahisi.

Read More