Advertising

  • Matunda

    faida ya tunda la KITZ
  • Matunda

    kula matunda kwa wingi
  • GYm

    Mazoezi muhimu kwa afya
  • Mazoezi

    dada anaimarisha misuli
  • Jovago

    Promoo siku ya watendao

January 27, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 11:24 AM | Be the first to comment!

Ombeni Sefue akutana na makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu kutoka wizara zote za serikali



                                                    
Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu kutoka wizara zote za serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekutana hii leo (02 Januari, 2016) katika ukumbi wa Mikutano wa Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata semina elekezi iliyoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
Akizungumza kabla ya kuanza kwa mada zilizoandaliwa katika semina hiyo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, amesema semina hiyo ni ya kikazi zaudu na kwamba lengo la serikali ni kuhakikisha Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu hao ambao waliapishwa jana wanatekeleza wajibu wa kusimamia utendaji kazi wa serikali vizuri.
Balozi Sefue ameelekeza kuwa kila Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu anapaswa kutambua kuwa nafasi yake ni ya maamuzi, hivyo serikali inatarajia kuona kuwa daima anafanya maamuzi kwa usahihi na kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazomuongoza katika majukumu yake.
Aidha, ameonya kuwa serikali ya awamu ya tano inawatarajia viongozi hao kuwa watakuwa wasimamizi wazuri wa fedha za umma na kwamba haitarajii kuwepo kwa hati za ukaguzi wa mahesabu zenye kasoro.
Balozi Sefue ameongeza kuwa Makatibu Wakuu hao na Naibu Makatibu Wakuu ni mamlaka ya nidhamu katika wizara zao, hivyo Serikali haitarajii kuona wanakua na kigugumizi katika kuchukua hatua dhidi ya watumishi watakaokuwa na makosa, na akakumbusha kuwa haikubaliki kwa mtumishi aliyefanya makosa katika sehemu moja ya kazi, kuhamishiwa katika sehemu nyingine badala ya kuchukuliwa hatua palepale alipo.
Semina hii elekezi imefanyika kwa siku moja
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:28 AM | Be the first to comment!

Mpango wa Uendeshaji Shughuli za Serikali kwa Uwazi ni nini

Mpango wa Uendeshaji Shughuli za Serikali kwa Uwazi(OGP) ni juhudi ya kimataifa inayolenga kuhimiza uwazi, kuwawezesha wananchi, kupambana dhidi ya rushwa na kuhimiza kutumia teknolojia mpya na kuboresha utawala. OGP ilizinduliwa rasmi tarehe 20 Septemba 2011 mjini New York na nchi 8 wanachama waanzilishi za Brazili, Indonesia,  Mexico, Norway, Philippines, Afrika Kusini, Uingereza na Marekani. OGP inasimamaiwa na Kamati ya Uendeshaji ya Kimataifa ya wadau mbalimbali yenye wawakilishi wa serikali na asasi za kiraia. Miongoni  mwa manufaa ya OGP ni kuboresha utoaji wa huduma na kufanya serikali ziwe na majukumu na  kuwajibika  zaidi kwa raia wao. Kutokana na manufaa ya juhudi hizi, Tanzania ilionyesha nia yake ya kujiunga na OGP wakati wa mkutano wa uzinduzi. Uamuzi wa kujiunga na OGP ni hatua muhimu ya kusaidia juhudi za sasa za serikali kuhamasisha utawala bora kwenye sekta zote
                          

               Dhamira za OGP


                        Uwajibikaji na Uaminifu
                              Uwazi             
                        Kuhusisha Wananchi
                         Teknolojia na Ubunifu
Read More