Mpango wa Uendeshaji Shughuli za Serikali kwa Uwazi(OGP) ni juhudi ya kimataifa inayolenga kuhimiza uwazi, kuwawezesha wananchi, kupambana dhidi ya rushwa na kuhimiza kutumia teknolojia mpya na kuboresha utawala. OGP ilizinduliwa rasmi tarehe 20 Septemba 2011 mjini New York na nchi 8 wanachama waanzilishi za Brazili, Indonesia, Mexico, Norway, Philippines, Afrika Kusini, Uingereza na Marekani. OGP inasimamaiwa na Kamati ya Uendeshaji ya Kimataifa ya wadau mbalimbali yenye wawakilishi wa serikali na asasi za kiraia. Miongoni mwa manufaa ya OGP ni kuboresha utoaji wa huduma na kufanya serikali ziwe na majukumu na kuwajibika zaidi kwa raia wao. Kutokana na manufaa ya juhudi hizi, Tanzania ilionyesha nia yake ya kujiunga na OGP wakati wa mkutano wa uzinduzi. Uamuzi wa kujiunga na OGP ni hatua muhimu ya kusaidia juhudi za sasa za serikali kuhamasisha utawala bora kwenye sekta zote
January 27, 2016
Mpango wa Uendeshaji Shughuli za Serikali kwa Uwazi ni nini
Mr Mtinangi | 12:28 AM |
serikalitz
About Mr Mtinangi -
Hajasomea uandishi wa habari yeye anapenda kuisaidia jamii kufahamu yale yanayotokea duniani japo kwa kiasi kidogo na nifuraha kwako hata kama mtu mmoja akipata taarifa mpya kupitia moojuhudi,namini katika haba ile na ile hujaza kibaba