Advertising

  • Matunda

    faida ya tunda la KITZ
  • Matunda

    kula matunda kwa wingi
  • GYm

    Mazoezi muhimu kwa afya
  • Mazoezi

    dada anaimarisha misuli
  • Jovago

    Promoo siku ya watendao

February 7, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 4:06 AM | Be the first to comment!

Leicester City Baada ya Kuilaza City Yatuma Salamu Kwa Arsenal



Leicester City wanazidi kujikita kileleni mwa ligi kuu England baada ya leo kuwatungua vigogo wa EPL Man City kwa mabao 3-1.
Licha ya kuwa hawapewi nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa, vijana hao wa Ranieri wanaonekana kuwa na ari ya hali ya juu na kuwapa fursa kubwa ya kuendelea kuongoza ligi na hatimaye kutwaa ubingwa
Ifuatayo ni michezo ambayo endapo watashinda, basi watakuwa wamejipalilia njia ya kutwaa ndoo ya EPL msimu huu.

Robert Huth amepiga bao mbili kwenye game hiyo huku Riyad Mahrez akipiga bao moja wakati huo akiwa amepika moja ya bao ambalo lilifungwa na Huth na kumfanya kuingia top Five of master assist
Sergio Aguero aliifungia Manchester City bao pekee la kufutia machozi dakika za lala salama na kumfanya ashike nafasi ya nne baada ya kufikisha magoli 14.
Leicester tayari imeshatoa kichapo kwa Tottenham ambayo ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kwenye uwanja wa Spurs White Hart Lane mwezi January lakini matokeo ya leo dhidi ya City yalikuwa muhimu sana kwenye msimu huu wa kihistoria kwao.
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 3:47 AM | Be the first to comment!

Samatta Aanza Kwa Kishindo, Timu yake Yashinda 1 – 0



Baada ya nyota wa Tanzania Mbwana Samatta kufanikiwa kukipiga kwa mara ya kwanza kwenye klabu yake ya KCR Genk, mkali huyo ameandika ujumbe kwenye account yake ya instagram kuwashukuru wale wote wanaom-support na kumtakia mema.
Samatta ameandika ujumbe unaosomeka kama ifuatavyo: “Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru watanzania pamoja na mashabiki wangu wote wa @krc_genk_ kwa maombi na support yenu, Leo nimefanikiwa kucheza mchezo wa kwanza rasmi nikiwa na klabu yangu mpya @krc_genk_na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0”.
Kwenye mchezo huo ambao Genk ilikuwa ugenini ikicheza dhidi ya Muscron, Popa aliingia dakika ya 73 kuchukua nafasi ya Nikos Kareli na kumaliza dakika zote zilizo salia.
Mtanzania Mbwana Samatta ameishaanza kuichezea KRC Genk ya Ubelgiji baada ya jana kuingia katika mechi ya ligi na kucheza kwa dakika 17 wakati timu hiyo ilipoivaa Mouscron na kushinda kwa bao 1-0.
Samatta anaonyesha ni mtu wa malengo kweli baada ya kuacha magari yake zaidi ya matatu, na kwenda kuanza kutafuta maisha upya Genk.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa TP Mazembe, ameamua kuachana na kila kitu ukiwemo umaarufu wake mkubwa nchini DR Congo na kwenda kuanza upya nchini Ubelgiji kwa kuwa anataka kutimiza ndoto yake


Read More

February 6, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:17 AM | Be the first to comment!

Kun Sergio Aguero Kutoa tuzo ya mchezaji bora January 2016





Mkali wa kucheka na nyavu wa the blues wa jijini Manchester ameisaidia timu yake kubeba point 8 katika mechi nne na kuifanya manchester city unbeaten.
 Katika mechi hizo nne Sergio Aguero amefunga magoli matano na kutoa asist moja,December tuzo hiyo ilichukuliwa na mkali wa Nigeria na club ya watford Odion Ighalo ambaye pia alifunga magoli 5 december
               
Read More

February 5, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 11:59 PM | Be the first to comment!

Kwanini kocha Mayanja wa Simba hampi nafasi kikosini Said Ndemla?


February 3 kocha wa Simba Jackson Mayanja amekutana na swali la waaandishi wa habari juu ya kiungo wa Simba anayeichezea timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Said Hamisi Ndemla kutopewa nafasi kwenye kikosi cha Simba toka kocha Masanja aanze kazi.
Kama ulikua hujui, Wataalamu wa mambo wanasema Ndemla ameichezea Simba sio zaidi ya dakika 50 hadi sasa
Read More

February 4, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 3:41 AM | Be the first to comment!

Kwa Mwendo Huu wa Barcelona Wengi Watalia Mwaka Huu!na kwa moto huu Arsenal wataweza kuwazuia?

Klabu ya Valencia chini ya nyota wa zamani wa Manchester United Gary Neville ilipokezwa kichapo cha mwaka na klabu ya Barcelona katika nusufainali ya michuano ya Copa del Rey baada ya kubebeshwa magoli saba.
Mechi hiyo ya mkondo wa kwanza ilichezewa uwanjani Nou Camp.Luis Suarez alifunga mabao manne, huku nyota wa Argentina Lionel Messi naye akijizolea magoli matatu.

Neymar alishindwa kufunga penalti. Valencia walidhofishwa zaidi na hatua ya beki Shkodran Mustafi kumchezea visivyo Messi kipindi cha kwanza, kosa lililomfanya kufukuzwa uwanjani
Neville hajashinda mechi hata moja ligini kati ya nane alizosimamia tangu kuchukua usukani Desemba.
Neville alikuwa amerejea uwanja ambao enzi yake ya uchezaji alipanda ushindi mkubwa na muhimu sana.
Akiwa na umri wa miaka 24, alikuwa kwenye timu ya United iliyoshinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kujikwamua dhidi ya Bayern Munich fainali ya 1999 uwanjani Nou Camp.
Akizungumza baada ya mechi hiyo dhidi ya Barca, Neville alisema siku hiyo ni moja ya siku zenye machungu zaidi katika maisha yake katika ulimwengu wa soka

Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 1:42 AM | Be the first to comment!

Guinea Yatupwa Nje CHAN,DR Congo Yatinga Fainali

Jamhuri ya Demokrasia ya Congo imefuzu kwa fainali ya mchuano wa CHAN. Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ilijikatia tikiti ya fainali baada ya kuilaza Guinea mabao 5-4 kwa mikwaju ya penalti.
Mechi hiyo ilikuwa imeishia sare ya moja kwa moja katika muda waziada baada ya Ibrahim Sankhon kuisawazishia Guinea kunako dakika ya mwisho ya kipindi cha pili cha muda wa ziada.

Lakini dalili za kufuzu zilionekana mapema,Ibrahim Bangoura alipokosa penalti ya kwanza ya Guinea. Kimwaki,Mika,Jonathan Bolingi,Gikanji,Mechak Elia walifungia Leopards ya DRC huku
Ibrahim Sankhon,Leo Camara,Kile Bangoura,Daouda Camara wakiifungia Guinea. Hata hivyo Kipa nambari moja wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo Vumi Ley Matampi aliokoa mkwaju wa penalti uliopigwa na Youla na kuipa DRC ushindi wa mabao 5-4 Guinea
Timu hizo zilitoshana nguvu muda wa kawaida na mechi ikaingia muda wa ziada uwanjani Amahoro, Rwanda. Ni katika muda wa ziada ambapo Jonathan Bolingi Mpangi kunako dakika ya 101 alifanikiwa kutikisa wavu wa Guinea.
Mapema kwenye mechi, mchezaji wa DR Congo Padou Bompunga alipewa kadi ya njano dakika ya 38. Hili lina maana kwamba hataweza kucheza fainali iwapo timu yake itafuzu.
Kipa wa DR Congo Ley Matampi pia alipewa kadi ya njano, kosa lake likiwa kunawa mpira nje ya eneo lake.
Rais wa Rwanda Paul Kagame ni miongoni mwa wageni mashuhuri waliohudhuria mechi hiyo. DRC sasa watasubiri hadi kesho kujua mpinzani wao kati ya Mali na Cote de Voire.
Mechi hiyo ya nusu fainali ya pili imeratibiwa kusakatwa katika uwanja wa taifa wa Kigali kuanzia saa kumi jioni saa za Afrika ya kati.



Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 1:36 AM | Be the first to comment!

Mnyama Simba Aunguruma Taifa, Yanga Yapigishwa Kwata Mbeya



Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea tena leo February 3 kwa michezo mitano kupigwa katika viwanja tofauti tofauti Tanzania, klabu ya Dar Es Salaam Young Africans ilikuwa mgeni wa klabu ya Tanzania Prisons uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati watani zao wa jadi Simba walikuwa wenyeji wa Mgambo JKT uwanja wa Taifa Dar Es Salaam
Simba ambao kwa sasa wapo na kocha wao msaidizi Jackson Mayanja bila kuwa na kocha mkuu wamefanikiwa kuendeleza hali ya ushindi kwa kila mechi, baada ya mchezo wao wa wiki iliyopita dhidi ya Africans Sports kuibuka na ushindi wa goli 4-0. February 3 Simba wamefanikiwa kuibuka na ushindi mwingine mnono dhidi ya Mgambo JKT uwanja wa Taifa, kwa kuwafunga idadi ya goli 5-1.
Wekundu wa Msimbazi Simba walikuwa mahiri katika kuuchezea mpira, kwani dakika ya 5 tu walifanikiwa kupachika goli la kwanza kupitia kwa Hamis Kiiza, kabla ya Mwinyi Kazimoto hajafunga goli la pili dakika ya 28 na Ibrahim Ajib kufunga goli la tatu dakika ya 45. Kipindi cha pili Simba waliendeleza ubabe baada ya dakika ya 77 Danny Lyanga kupachika goli la nne
Mshambuliaji wao tegemeo Hamis Kiiza alihitimisha ushindi huo kwa kufunga goli la tano, Mgambo walipata goli la kufutia machozi dakika ya 87 kupitia kwa Fully Maganga baada ya ngome ya ulinzi ya Simba kujisahau. Kwa matokeo hayo Simba wanakuwa nafasi ya pili wakiwa na point 39 nyuma ya Yanga kwa tofauti ya point moja
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa February 3
• Prisons 2 – 2 Yanga
• Kagera Sugar 2 – 1 Majimaji FC
• Africans Sports 1 – 0 Mwadui FC
• Mtibwa Sugar 2 – 2 Toto Africans
Read More

February 2, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 10:57 AM | Be the first to comment!

JKT Ruvu Yarejesha Majeshi Ligi Kuu Tanzania Bara



Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa Rais wake, Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa klabu ya Ruvu Shooting kwa kufanikiwa kupanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu ujao.
Malinzi ametuma salamu hizo kwa Mwenyekiti wa klabu ya Ruvu Shooting, Col. Charles Mbuge, viongozi, benchi la ufundi na wachezaji na kuwataka kujipanga kwa maandalizi ya nguvu msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Ruvu Shooting imekua timu ya kwanza kupanda ligi kuu kwa ajili ya msimu ujao baada ya juzi kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lipuli FC mjini Iringa na kufikisha alama 31 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yeyote kutoka katika kundi B.
Washindi wawili kutoka makundi ya A na B wataungana na Ruvu Shooting kupanda Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao huku timu zote zikiwa zimebakiza michezo miwili miwili kabla ya kumalizika kwa ligi daraja la kwanza msimu huu.
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 10:55 AM | Be the first to comment!

Kundi la Navy Kenzo Waanza Mwaka Kwa Kishindo



Baada ya kutamba Mwaka Jana Africa nzima na wimbo unaoitwa ‘Game’, Kundi la Navy Kenzo limeanza mwaka vizuri baada ya kutoa wimbo mpya pamoja na video yake unaitwa “Kamatia” , Wimbo huo umeshaanza kuwa gumzo sehemu mbali mbali na kuonyeshwa kwenye TV za kimataifa siku mbili tu baada ya kutoka
Uzinduzi wa Wimbo Huo ulifanyika Kiaina yake kwa Staili ya ‘Flash Mob’ Kwenye Club ya Rhapsody kwa kuwasuprise waliokuwa ndani ya Club hiyo.
Kundi la Navy Kenzo linaloundwa na Aika na Nahreel mpaka sasa wameshatoa nyimbo kadhaa zilizotamba sana kama Moyoni, Bokodo, Visa na nyingine nyingi.
Navy Kenzo wameamua kutoa Wimbo pamoja na Video yake moja kwa moja kutokana na ushindani uliopo kwa sasa kwenye Music wa Bongo Flava, Video imefanyika nchini South Africa na Muongozaji wa Video wa kimataifa anayeitwa Justin Campos.
Kamatia ni wimbo ambao unaongelea kuhusu wapenzi wawili waliomua kushikana hasa kwenye mapenzi , Midundo ya nyimbo hiyo ina mahadhi ya Dancehall na vionjo vya kipekee kutoka kwa Producer bora Tanzania Nahreel.
Nahreel Ambaye ni mmoja wa Kundi la Navy Kenzo ni Producer wa Muziki bora Mwenye tuzo ya Kilimanjaro Music, Ametengeneza nyimbo mbali mbali zilitamba Kama Nana ya Diamond Ft Flavor, Joh Makini Ft Aka Don’t Bother and Vanessa Mdee’s Nobody but me, Never ever na Hawajui, pia ndio mpishi wa Nyimbo ya Navykenzo ‘Game’
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 10:52 AM | Be the first to comment!

TFF Yasema Hawana Bifu na ZFA, Maana Lengo lao ni Moja


                                             
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), limesema hakuna vita kati ya Shirikisho na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) bali mawasiliano yanaendelea kati ya TFF na vyombo husika kuhakikisha ZFA ambaye ni mwanachama mshiriki wa CAF anaendesha shughuli zake kwa mujibu wa taratibu.
Kanuni na taratibu za CAF ziko wazi kuhusu nani aongoze Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) na anapatikana kwa utaratibu upi.
Kikubwa ni kuzuia ZFA isipate madhara ya kufungiwa na Chama Cha Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 10:50 AM | Be the first to comment!

Malinzi Ampongeza Makunga Kuwa Mwenyekiti



Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Theophil Makunga kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) mwishoni mwa wiki.
Katika salamu hizo, Malinzi amempongeza Makunga kwa nafasi hiyo aliochaguliwa na kusema imani waliyonayo wahariri wenzake juu ya utendaji wake wa kazi ndio kumepelekea wao kumchagua kuongoza jukwa hilo.
Aidha Malinzi amewapongeza Deodatus Balile aliyechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti na Neville Meena aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa jukwaa hilo na kuahidi kuwa TFF itaendelea kushirikiana nao.
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 10:21 AM | Be the first to comment!

Kipute Ligi Kuu ya Uingereza Kuendelea tena Leo




Ligi kuu ya England inatarajia kuendelea tena leo jumanne o3 february kufuatia mapumziko ya michuano ya FA, kwa michezo kadhaa,ambapo Arsenal watawakaribisha Southampton,Leicester city watakuwa wenyeji wa Liverpool, Norwich watakuwa wakimenyana na Tottenham Hotspurs.
Michezo mingine Sunderland watawaalika Manchester City, Aston Villa watakuwa wageni wa West Ham United,Crystal Palace watawakaribisha Bournemouth, Stoke watakuwa wenyeji wa Manchester Unted na West Brom watachuana na Swansea city.
Mpaka sasa Leicester city wanaongoza ligi kwa alama 47 ikifuatiwa na Manchester city katika nafasi ya pili,nafasi ya tatu ni Arsenal na nafasi ya nne ni Tottenham.
Read More

February 1, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 9:38 PM | Be the first to comment!

Club ya Simba yazindua duka la vifaa vya mihezo jiji Dar es salaam





Rais wa Simba Evans Aveva akikata utepe kuzindua duka la club 
Baada ya Azam FC kufungua duka lao la bidhaa za timu, simba sc nao hii leo wamezindua duka la kuudha bidhaa za Simba SC, ambalo linapatikana katika Dar Free Market jijini Dar es salaam.

Duka hilo lililochini ya kampuni ya Insight Media yenye ubia na Simba SC litakuwa linauza bidhaa halali za Simba SC, kwa bei nafuu.

Wakati wauzinduzi wa duka hilo hii leo raisi wa Simba SC Evans Aveva amewakaribisha mashabiki na wanachama wa Simba SC wanaotaka kuuza bidhaa za Simba SC waende wazungumze na uongozi.

“Waje nao tuwapa tenda kama hii kwa Insight, wasaidie kuuza vifaa hivi. Wao watafaidika, klabu pia itafaidika na kupata maendeleo,” alisema Aveva.


Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 11:02 AM | Be the first to comment!

HAYA NI MANENO YA IDRIS SULTAN KUHUSU UJIO WA TV SHOW YAKE MPYA BET

Mshindi wa Big Brother Africa 2014 Idris Sultan anaziandika headlines kwenye kurasa za burudani… baada ya kuiwakilisha #255 vizuri kwenye shindano hilo kubwa la Africa, mafanikio mengi yamekuwa yakimfuata nyuma Idris Sultan
    
Kama wewe ni miongoni wa watu wanaompenda na kumfuatilia Idris kwenye social networks basi hii good news ikufikie popote ulipo mtu wangu… Idris Sultan siku chache zilizopita alitudokeza kuhusu ujio wa TV Show yake mpya itakayo kuwa inaonyeshwa moja kwa moja kupitia channel ya BET pamoja na channel ya Vuzu za South Africa! Yote ikiwa ni sehemu ya kufanikisha ndoto zake kubwa za kwendaHollywood, Marekani
Read More

January 29, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:03 AM | Be the first to comment!

Manchester City Yapata Pigo, Bruyne nje Wiki kumi




Kiungo wa Manchester City, Kevin de Bruyne, atakua nje ya dimba kwa muda wa wiki sita baada ya kuumia goti siku ya Jumatano.
De Bruyne aliumia goti la kulia katika mchezo kombe la Capital, ambapo Man City, waliwakabali Everton, na kushinda kwa mabao 3-1.
Wakala wa mchezaji huyu Patrick de Koster, amesema” Nimezungumza na Kevin, amesema atarudi uwanja kwa nguvu zaidi.”
Mchezaji huya atakosa michezo muhimu ya timu yake ukiwemo ule wa fainali ya kombe la Capital, dhidi ya Liverpool, hapo Februari 28, pia atakosa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi Dynamo Kiev.
Kulikua na wasiwasi huenda nyota huyu asingeweza rudi dimbani mpaka mwisho wa msimu.
Read More

January 28, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 11:21 PM | Be the first to comment!

Je ataweza kuziba pengo la mkali Michael Jackson katika miondoko ya POP


Muigizaji wa filamu kutoka nchini Uingereza Joseph Fiennes, amekiri kuwa alishangazwa na kitendo cha kumuigiza mfalme wa muziki aina ya POP, Michael Jackson katika mchezo wa runinga ,baada ya kukosekana kwa muigizaji mweupe









Muigizaji huyu atakayeigiza kama mwanamuziki katika vichekesho vinavyorushwa na mtandao wa ”sky network” unaohusu safari ya barabarani iliyofanywa na Michael Jackson na marafiki zake kina Marlon,Brando na Elizabeth Taylor baada ya uvamizi wa mara 9
Fiennes alieleza kuwa tabaka hilo la kati halikuwa chaguo lake lakini alisema Michael Jackson alikuwa na tatizo la rangi yake ngozi kutokuwa ya asili,hivyo suala la utofauti wa rangi halikuwa kikwazo kwake

Read More

January 27, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:03 AM | Be the first to comment!

Neymar pamoja na mshikaji wake wadizaini kiatu cha kuchezea mpira kilichopewa jina la Ousadia Alegria

Mchezaji mahiri wa club ya Barcelona pamoja na timu ya Taifa ya Brazil neymar jr pamoja na mbrazil mwenzake Bruno Big wamedizaini kiatu ambocho wengi wanaamin kitakuwa na ubora wa hali juu kupitia nembo ya Nike






Jamaa kumbe ukiachana na kipaji chake cha kuchezea gozi pia na designer. plan B yake siku akiwa hayupo uwanjani 


Read More

January 25, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 9:25 PM | Be the first to comment!

Manchester united hawajakata tamaa kwa Pep Guardiola

moo
Manchester united hawajawa na msimu mzuri toka alivoondoka kocha bora kwa club bora moja Sir Alex.
Manchester united wataki tena kurudia dhambi ya kufukuza kocha katikati ya msimu kama walivofanya mwaka juzi kumfukuza david moyes(choosen one)hivyo wamemuweka wazi Van gaal kwamba yuko salama mpaka mwisho wa msimu huu



moo




Manchester united wanaamini bado wananafasi ya kuweza kumpeleka pep Guardiola Old Trafford jambo ambalo linaonekana ni gumu kwani kocha huyo inaaminika yuko karibu kuchukuliwa na wasimu wao Manchester city








Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 10:15 AM | Be the first to comment!

Full Time ya Azam FC Vs African Lyon FA Cup Jan 25 2016 (+Pichaz)













Timu hiyo inayofundishwa na Stewart Hall imefanikiwa ilianza kupata goli la kwanza dakika ya 1 kupitia kwa kiungo wake Mudathir Yahaya, wakati goli la pili na la tatu  yalifungwa na Farid Mussa dakika ya 3 na 37, Ame Ally alipachika goli la nne na la mwisho dakika ya 54 ya mchezo. Kwa sasa Kombe la FA litaingia hatua ya 16 bora.
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 9:51 AM | Be the first to comment!

Martial wa Man utd

Gazeti la The Sun lilimuweka kwenye headlines mkali wa kucheka na nyavu wa Man United, baada ya kumuandika kuhusu stori za usaliti wa mapenzi. Mastaa wa soka huwa wanaingia kwenye headlines za usaliti wa mapenzi aliwahi kuingia katika headlines hizoJohn Terry wa Chelsea ila yeye kulikuwa na ushahidi sasa ni Anthony Martial wa Man United
Read More