Advertising

  • Matunda

    faida ya tunda la KITZ
  • Matunda

    kula matunda kwa wingi
  • GYm

    Mazoezi muhimu kwa afya
  • Mazoezi

    dada anaimarisha misuli
  • Jovago

    Promoo siku ya watendao

February 7, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 4:06 AM | Be the first to comment!

Leicester City Baada ya Kuilaza City Yatuma Salamu Kwa Arsenal



Leicester City wanazidi kujikita kileleni mwa ligi kuu England baada ya leo kuwatungua vigogo wa EPL Man City kwa mabao 3-1.
Licha ya kuwa hawapewi nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa, vijana hao wa Ranieri wanaonekana kuwa na ari ya hali ya juu na kuwapa fursa kubwa ya kuendelea kuongoza ligi na hatimaye kutwaa ubingwa
Ifuatayo ni michezo ambayo endapo watashinda, basi watakuwa wamejipalilia njia ya kutwaa ndoo ya EPL msimu huu.

Robert Huth amepiga bao mbili kwenye game hiyo huku Riyad Mahrez akipiga bao moja wakati huo akiwa amepika moja ya bao ambalo lilifungwa na Huth na kumfanya kuingia top Five of master assist
Sergio Aguero aliifungia Manchester City bao pekee la kufutia machozi dakika za lala salama na kumfanya ashike nafasi ya nne baada ya kufikisha magoli 14.
Leicester tayari imeshatoa kichapo kwa Tottenham ambayo ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kwenye uwanja wa Spurs White Hart Lane mwezi January lakini matokeo ya leo dhidi ya City yalikuwa muhimu sana kwenye msimu huu wa kihistoria kwao.
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 3:47 AM | Be the first to comment!

Samatta Aanza Kwa Kishindo, Timu yake Yashinda 1 – 0



Baada ya nyota wa Tanzania Mbwana Samatta kufanikiwa kukipiga kwa mara ya kwanza kwenye klabu yake ya KCR Genk, mkali huyo ameandika ujumbe kwenye account yake ya instagram kuwashukuru wale wote wanaom-support na kumtakia mema.
Samatta ameandika ujumbe unaosomeka kama ifuatavyo: “Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru watanzania pamoja na mashabiki wangu wote wa @krc_genk_ kwa maombi na support yenu, Leo nimefanikiwa kucheza mchezo wa kwanza rasmi nikiwa na klabu yangu mpya @krc_genk_na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0”.
Kwenye mchezo huo ambao Genk ilikuwa ugenini ikicheza dhidi ya Muscron, Popa aliingia dakika ya 73 kuchukua nafasi ya Nikos Kareli na kumaliza dakika zote zilizo salia.
Mtanzania Mbwana Samatta ameishaanza kuichezea KRC Genk ya Ubelgiji baada ya jana kuingia katika mechi ya ligi na kucheza kwa dakika 17 wakati timu hiyo ilipoivaa Mouscron na kushinda kwa bao 1-0.
Samatta anaonyesha ni mtu wa malengo kweli baada ya kuacha magari yake zaidi ya matatu, na kwenda kuanza kutafuta maisha upya Genk.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa TP Mazembe, ameamua kuachana na kila kitu ukiwemo umaarufu wake mkubwa nchini DR Congo na kwenda kuanza upya nchini Ubelgiji kwa kuwa anataka kutimiza ndoto yake


Read More

February 6, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:17 AM | Be the first to comment!

Kun Sergio Aguero Kutoa tuzo ya mchezaji bora January 2016





Mkali wa kucheka na nyavu wa the blues wa jijini Manchester ameisaidia timu yake kubeba point 8 katika mechi nne na kuifanya manchester city unbeaten.
 Katika mechi hizo nne Sergio Aguero amefunga magoli matano na kutoa asist moja,December tuzo hiyo ilichukuliwa na mkali wa Nigeria na club ya watford Odion Ighalo ambaye pia alifunga magoli 5 december
               
Read More

February 5, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 11:59 PM | Be the first to comment!

Kwanini kocha Mayanja wa Simba hampi nafasi kikosini Said Ndemla?


February 3 kocha wa Simba Jackson Mayanja amekutana na swali la waaandishi wa habari juu ya kiungo wa Simba anayeichezea timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Said Hamisi Ndemla kutopewa nafasi kwenye kikosi cha Simba toka kocha Masanja aanze kazi.
Kama ulikua hujui, Wataalamu wa mambo wanasema Ndemla ameichezea Simba sio zaidi ya dakika 50 hadi sasa
Read More

February 4, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 3:41 AM | Be the first to comment!

Kwa Mwendo Huu wa Barcelona Wengi Watalia Mwaka Huu!na kwa moto huu Arsenal wataweza kuwazuia?

Klabu ya Valencia chini ya nyota wa zamani wa Manchester United Gary Neville ilipokezwa kichapo cha mwaka na klabu ya Barcelona katika nusufainali ya michuano ya Copa del Rey baada ya kubebeshwa magoli saba.
Mechi hiyo ya mkondo wa kwanza ilichezewa uwanjani Nou Camp.Luis Suarez alifunga mabao manne, huku nyota wa Argentina Lionel Messi naye akijizolea magoli matatu.

Neymar alishindwa kufunga penalti. Valencia walidhofishwa zaidi na hatua ya beki Shkodran Mustafi kumchezea visivyo Messi kipindi cha kwanza, kosa lililomfanya kufukuzwa uwanjani
Neville hajashinda mechi hata moja ligini kati ya nane alizosimamia tangu kuchukua usukani Desemba.
Neville alikuwa amerejea uwanja ambao enzi yake ya uchezaji alipanda ushindi mkubwa na muhimu sana.
Akiwa na umri wa miaka 24, alikuwa kwenye timu ya United iliyoshinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kujikwamua dhidi ya Bayern Munich fainali ya 1999 uwanjani Nou Camp.
Akizungumza baada ya mechi hiyo dhidi ya Barca, Neville alisema siku hiyo ni moja ya siku zenye machungu zaidi katika maisha yake katika ulimwengu wa soka

Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 1:42 AM | Be the first to comment!

Guinea Yatupwa Nje CHAN,DR Congo Yatinga Fainali

Jamhuri ya Demokrasia ya Congo imefuzu kwa fainali ya mchuano wa CHAN. Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ilijikatia tikiti ya fainali baada ya kuilaza Guinea mabao 5-4 kwa mikwaju ya penalti.
Mechi hiyo ilikuwa imeishia sare ya moja kwa moja katika muda waziada baada ya Ibrahim Sankhon kuisawazishia Guinea kunako dakika ya mwisho ya kipindi cha pili cha muda wa ziada.

Lakini dalili za kufuzu zilionekana mapema,Ibrahim Bangoura alipokosa penalti ya kwanza ya Guinea. Kimwaki,Mika,Jonathan Bolingi,Gikanji,Mechak Elia walifungia Leopards ya DRC huku
Ibrahim Sankhon,Leo Camara,Kile Bangoura,Daouda Camara wakiifungia Guinea. Hata hivyo Kipa nambari moja wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo Vumi Ley Matampi aliokoa mkwaju wa penalti uliopigwa na Youla na kuipa DRC ushindi wa mabao 5-4 Guinea
Timu hizo zilitoshana nguvu muda wa kawaida na mechi ikaingia muda wa ziada uwanjani Amahoro, Rwanda. Ni katika muda wa ziada ambapo Jonathan Bolingi Mpangi kunako dakika ya 101 alifanikiwa kutikisa wavu wa Guinea.
Mapema kwenye mechi, mchezaji wa DR Congo Padou Bompunga alipewa kadi ya njano dakika ya 38. Hili lina maana kwamba hataweza kucheza fainali iwapo timu yake itafuzu.
Kipa wa DR Congo Ley Matampi pia alipewa kadi ya njano, kosa lake likiwa kunawa mpira nje ya eneo lake.
Rais wa Rwanda Paul Kagame ni miongoni mwa wageni mashuhuri waliohudhuria mechi hiyo. DRC sasa watasubiri hadi kesho kujua mpinzani wao kati ya Mali na Cote de Voire.
Mechi hiyo ya nusu fainali ya pili imeratibiwa kusakatwa katika uwanja wa taifa wa Kigali kuanzia saa kumi jioni saa za Afrika ya kati.



Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 1:36 AM | Be the first to comment!

Mnyama Simba Aunguruma Taifa, Yanga Yapigishwa Kwata Mbeya



Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea tena leo February 3 kwa michezo mitano kupigwa katika viwanja tofauti tofauti Tanzania, klabu ya Dar Es Salaam Young Africans ilikuwa mgeni wa klabu ya Tanzania Prisons uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati watani zao wa jadi Simba walikuwa wenyeji wa Mgambo JKT uwanja wa Taifa Dar Es Salaam
Simba ambao kwa sasa wapo na kocha wao msaidizi Jackson Mayanja bila kuwa na kocha mkuu wamefanikiwa kuendeleza hali ya ushindi kwa kila mechi, baada ya mchezo wao wa wiki iliyopita dhidi ya Africans Sports kuibuka na ushindi wa goli 4-0. February 3 Simba wamefanikiwa kuibuka na ushindi mwingine mnono dhidi ya Mgambo JKT uwanja wa Taifa, kwa kuwafunga idadi ya goli 5-1.
Wekundu wa Msimbazi Simba walikuwa mahiri katika kuuchezea mpira, kwani dakika ya 5 tu walifanikiwa kupachika goli la kwanza kupitia kwa Hamis Kiiza, kabla ya Mwinyi Kazimoto hajafunga goli la pili dakika ya 28 na Ibrahim Ajib kufunga goli la tatu dakika ya 45. Kipindi cha pili Simba waliendeleza ubabe baada ya dakika ya 77 Danny Lyanga kupachika goli la nne
Mshambuliaji wao tegemeo Hamis Kiiza alihitimisha ushindi huo kwa kufunga goli la tano, Mgambo walipata goli la kufutia machozi dakika ya 87 kupitia kwa Fully Maganga baada ya ngome ya ulinzi ya Simba kujisahau. Kwa matokeo hayo Simba wanakuwa nafasi ya pili wakiwa na point 39 nyuma ya Yanga kwa tofauti ya point moja
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa February 3
• Prisons 2 – 2 Yanga
• Kagera Sugar 2 – 1 Majimaji FC
• Africans Sports 1 – 0 Mwadui FC
• Mtibwa Sugar 2 – 2 Toto Africans
Read More

February 2, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 10:57 AM | Be the first to comment!

JKT Ruvu Yarejesha Majeshi Ligi Kuu Tanzania Bara



Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa Rais wake, Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa klabu ya Ruvu Shooting kwa kufanikiwa kupanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu ujao.
Malinzi ametuma salamu hizo kwa Mwenyekiti wa klabu ya Ruvu Shooting, Col. Charles Mbuge, viongozi, benchi la ufundi na wachezaji na kuwataka kujipanga kwa maandalizi ya nguvu msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Ruvu Shooting imekua timu ya kwanza kupanda ligi kuu kwa ajili ya msimu ujao baada ya juzi kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lipuli FC mjini Iringa na kufikisha alama 31 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yeyote kutoka katika kundi B.
Washindi wawili kutoka makundi ya A na B wataungana na Ruvu Shooting kupanda Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao huku timu zote zikiwa zimebakiza michezo miwili miwili kabla ya kumalizika kwa ligi daraja la kwanza msimu huu.
Read More