Advertising

  • Matunda

    faida ya tunda la KITZ
  • Matunda

    kula matunda kwa wingi
  • GYm

    Mazoezi muhimu kwa afya
  • Mazoezi

    dada anaimarisha misuli
  • Jovago

    Promoo siku ya watendao

February 2, 2016

Mr Mtinangi

Kundi la Navy Kenzo Waanza Mwaka Kwa Kishindo

Mr Mtinangi | 10:55 AM |



Baada ya kutamba Mwaka Jana Africa nzima na wimbo unaoitwa ‘Game’, Kundi la Navy Kenzo limeanza mwaka vizuri baada ya kutoa wimbo mpya pamoja na video yake unaitwa “Kamatia” , Wimbo huo umeshaanza kuwa gumzo sehemu mbali mbali na kuonyeshwa kwenye TV za kimataifa siku mbili tu baada ya kutoka
Uzinduzi wa Wimbo Huo ulifanyika Kiaina yake kwa Staili ya ‘Flash Mob’ Kwenye Club ya Rhapsody kwa kuwasuprise waliokuwa ndani ya Club hiyo.
Kundi la Navy Kenzo linaloundwa na Aika na Nahreel mpaka sasa wameshatoa nyimbo kadhaa zilizotamba sana kama Moyoni, Bokodo, Visa na nyingine nyingi.
Navy Kenzo wameamua kutoa Wimbo pamoja na Video yake moja kwa moja kutokana na ushindani uliopo kwa sasa kwenye Music wa Bongo Flava, Video imefanyika nchini South Africa na Muongozaji wa Video wa kimataifa anayeitwa Justin Campos.
Kamatia ni wimbo ambao unaongelea kuhusu wapenzi wawili waliomua kushikana hasa kwenye mapenzi , Midundo ya nyimbo hiyo ina mahadhi ya Dancehall na vionjo vya kipekee kutoka kwa Producer bora Tanzania Nahreel.
Nahreel Ambaye ni mmoja wa Kundi la Navy Kenzo ni Producer wa Muziki bora Mwenye tuzo ya Kilimanjaro Music, Ametengeneza nyimbo mbali mbali zilitamba Kama Nana ya Diamond Ft Flavor, Joh Makini Ft Aka Don’t Bother and Vanessa Mdee’s Nobody but me, Never ever na Hawajui, pia ndio mpishi wa Nyimbo ya Navykenzo ‘Game’

Mr Mtinangi

About Mr Mtinangi -

Hajasomea uandishi wa habari yeye anapenda kuisaidia jamii kufahamu yale yanayotokea duniani japo kwa kiasi kidogo na nifuraha kwako hata kama mtu mmoja akipata taarifa mpya kupitia moojuhudi,namini katika haba ile na ile hujaza kibaba

Subscribe to this Blog via Email :