Nijua kuwa wanawake wengi wanajiuliza ni zipi dalili za saratani ya matiti? Dalili ya awali inayoweza kutambulisha saratani ya matiti ni kuwepo kwa uvimbe kwenye titi ambao huwa na hali tofauti na sehemu nyingine za titi. Hata hivyo, si kila uvimbe kwenye titi unaashiria uwepo wa saratani ya matiti. Uvimbe huu huwa mgumu, unaochezacheza au ambao hauko thabiti, ambapo wakati mwingine unaweza kuwa na maumivu makali au kusiwe na maumivu yoyote. Uvimbe huu huwepo zaidi ya mzunguko mmoja wa hedhi kwa wale ambao hawajaacha kupata hedhi. Dalili nyingine ni pamoja na kuwepo uvimbe kwenye sehemu za kwapa, sehemu ya titi kuingia ndani