Advertising

  • Matunda

    faida ya tunda la KITZ
  • Matunda

    kula matunda kwa wingi
  • GYm

    Mazoezi muhimu kwa afya
  • Mazoezi

    dada anaimarisha misuli
  • Jovago

    Promoo siku ya watendao

February 3, 2016

Mr Mtinangi

SERIKALI KUDHIBITI UGONJWA WA UKIMWI KUFIKIA MAAMBUKIZI SIFURI

Mr Mtinangi | 8:51 PM |




Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka akifungua Mkutano wa Serikali na wadau wa Ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi jana jijini Dar es 

Serikali imepanga mikakati na kusimamia juhudi zinazofanywa na kuendelezwa na wadau wa ukimwi kuhakikisha kuwa maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi yanapungua hadi kufikia sifuri ifikapo mwaka 2025.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti mtendaji kutoka Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt. Fatma H. Mrisho wakati wa mkutano wa serikali na wadau wa ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi jana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa mkutano huo Dkt. Mrisho amesema kuwa maambukizi ya ukimwi yamepungua ukilinganisha na miaka 10 iliyopita kwani idadi imepungua kutoka waathirika laki moja na elfu themanini hadi kufikia waathirika elfu sabini na mbili kwa sasa.
Akitoa mfano Dkt. Mrisho amesema kuwa Mkoa wa Njombe, Shinyanga, Dar es Salaam, Mbeya na Rukwa ni mikoa ambayo inaonyesha kuwa na idadi kubwa ya waathirika wa ukimwi hivyo kuwataka wadau wa ukimwi kutoka mikoa hiyo kutoa elimu ya kutosha kwa jamii ili kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi pamoja na magojwa ya zinaa.
Akifungua mkutano huo, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka amesema kuwa serikali imedhamiria kuanzisha mfuko utakaokua unashughulikia masuala ya ukimwi wakati wa bajeti ya mwaka 2015/2016 wenye lengo la kuondoa maambukizi mapya ya ukimwi nchini.
Aidha Dkt. Turuka ameitaka jamii kutowanyanyapaa waathirika wa ukimwi bali wawapende na kuwapa moyo ili waendelee kuwa na afya bora kwani serikali inawapigania na kuhakikisha kuwa wanatumia dawa za kuongeza maisha ili kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo.
Mkutano wa serikali na wadau wa ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi ulianzishwa mwaka 2003 ukifuatiwa na ule wa mwaka 2006 na kuendelezwa kila baada ya miaka miwili ambapo mkutano wa mwaka huu ni wa sita na umebeba kauli mbiu inayosema “Kwa yale mafanikio ambayo tumeyapata mpaka sasa tunayaendeleza”

Mr Mtinangi

About Mr Mtinangi -

Hajasomea uandishi wa habari yeye anapenda kuisaidia jamii kufahamu yale yanayotokea duniani japo kwa kiasi kidogo na nifuraha kwako hata kama mtu mmoja akipata taarifa mpya kupitia moojuhudi,namini katika haba ile na ile hujaza kibaba

Subscribe to this Blog via Email :