Mke wa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli, mama Janeth Magufuli ametembelea katika kituo cha Nunge kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam ambacho kinatumika kuhifadhi wazee wasiojiweza na walemavu.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi mchele, unga na maharage Mzee Anthony Kingongoti Mwenyekiti wa wakaazi wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na wagonjwa waliofika kupata huduma katika zahanati ya Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao