Advertising

  • Matunda

    faida ya tunda la KITZ
  • Matunda

    kula matunda kwa wingi
  • GYm

    Mazoezi muhimu kwa afya
  • Mazoezi

    dada anaimarisha misuli
  • Jovago

    Promoo siku ya watendao

February 6, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:59 AM | Be the first to comment!

Serikali yatoa tamko kuhusu udhalilishwaji aliyofanyiwa Mtanzania, India

Serikali imetoa tamko la kulaani kitendo kilichotokea nchini India kwa mwanafunzi wa kike wa kitanzania kuvuliwa nguo na kutembezwa barabarani ambapo Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje,Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na kimataifa imetoa tamko la kulaani suala hilo kwa kuitaka Serikali ya india kuchukua hatua.
Akitoa tamko hilo Bungeni Mjini Dodoma Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Dkt. Augustine Mahiga amesema ni kweli kwamba kuna mwanafunzi wa kike wa kitanzania alifanyiwa kitendo cha udhalilishaji nchini India kwa kuvuliwa nguo na kutembezwa 


barabarani suala ambalo lilizua mijadala mikubwa nchini kuhusu udhalilishaji huo.
“Wizara yetu imezungumza na Balozi wa India nchini na kumweleza ni kwa jinsi gani watanzania wamefadhaika na kusononeshwa na kitendo alichofanyiwa mtanzania mwenzao huko India na Balozi alituhakikishia kwamba amewasiliana na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi yake na kusema Serikali ya India kwa kushirikiana na Jeshi la polisi nchini humo wamefanikisha kuwakamata wote waliohusika na kitendo hicho na kuwafikisha mahakamani kujibu mashataka hayo”
“Pia Serikali ya India imeahidi kutoa ulinzi kwa wanafunzi wa kitanzania na wenye asilia ya Afrika  wanaosoma huko ili kuwalinda na kuwaepusha na vitendo hivyo vinavyofanya na raia ambao hawana nia njema kwa mahusiano mazuri ya kimataifa yaliyopo kati ya India na Tanzania”Alisema Mhe. Mahiga.
Serikali ya Tanzania imekuwa na mahusiano mazuri na Serikali ya India kwa miaka mingi sasa na kutokana na kitendo hiki kilichotokea nchini India,Waziri wa Mambo ya Nje ya India amefatana na Balozi wa Tanzania nchini humo kwenda Mji wa Bangalo ili kuongea na wanafunzi wakitanzania na wale wenye asili ya Afrika wanaosoma huko ili kujenga mahusiano mazuri na wazawa ikiwa ni jitihada za kupunguza vitendo hivyo kutokea mara kwa mara.
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:55 AM | Be the first to comment!

AU yaitaka Burundi kukubali wanajeshi wake

                                                 Rais wa Chad Idris Deby ndio mwenyekiti wa AU
Muungano wa Afrika, AU, umetoa wito kwa viongozi wa mataifa matano kuishawishi Burundi kukubali kikosi maalum cha kudumisha amani kufuatia miezi kadhaa ya ghasia za kisiasa nchini humo.


Kamati hiyo maalumu ya AU, inamshirikisha Waziri Mkuu wa Ethiopia, pamoja na Marais wa Afrika Kusini, Mauritania, Gabon na Senegal.
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza amepinga mpango huo, akisema huo ni uvamizi.
Uamuzi wake wa mwaka uliopita kutaka kugombea awamu ya tatu ulianzisha mapigano hayo ambapo kufikia sasa mamia ya watu wameuawa.
iongozi wa Afrika waliokuwa wakikutana juma lililopita walighairi juu ya swala la kuwatuma wanajeshi 5,000 wa kudumisha amani, na badala yake wakaamua kutumia njia za kidiplomasia.

Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:49 AM | Be the first to comment!

Wengine waliomvua nguo Mtanzania mbaroni

                                            Gari la wanafunzi hao liliteketezwa
Washukiwa zaidi wamekamatwa na maafisa wa polisi nchini India kuhusiana na kisa ambapo mwanafunzi Mtanzania alipigwa na kuvuliwa nguo mjini Bangalore.
Washukiwa wengine wanne wamekamatwa na kufikisha tisa, jumla ya washukiwa wanaozuiliwa na polisi.
Maafisa watatu wa polisi pia wamesimamishwa kazi, wakisubiri kufanyiwa uchunguzi.
Watatu hao wanatuhumiwa kukataa kupokea malalamiko kuhusu kushambuliwa kwa mwanafunzi huyo wa kike wa umri wa miaka 21 pamoja na wenzake wa tatu.
Balozi wa Tanzania nchini India John WH Kijazi anatarajiwa kukutana na waziri wa mambo ya ndani ya jimbo la Karnataka.
Baadaye, atakutana na wanafunzi waliodhalilishwa karibu na chuo chao.
Maafisa wawili kutoka afisi ya wizara ya mambo ya nje ya India wataandamana na balozi huyo.
Kisa cha kushambuliwa kwa wanafunzi hao kimeshutumiwa vikali na serikali ya Tanzania ambayo imeitaka India kuhakikisha usalama wa wanafunzi wanaoishi na kusomea humo.
Watanzania mtandaoni pia wamekuwa wakishutumu kisa hicho na kuitaka serikali kuchukua hatua.
Tangu kutokea kwa kisa hicho, wanafunzi wengi kutoka Tanzania wamekuwa wakihofia usalama wao
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:44 AM | 1 Comment so far

Balozi wa Tanzania aridhishwa na hali Bangalore


Balozi Kijazi amesema wenyeji na Waafrika wanafaa kuwa wakikutana na kujadiliana
Balozi wa Tanzania nchini India John Kijazi amesema ameridhika kwamba serikali ya nchi hiyo imeweka mikakati ya kutosha kuwalinda wanafunzi, kufuatia kisa ambapo wanafunzi wanne walishambuliwa mjini Bangalore Jumapili.
Akizungumza baada ya kutembelea pahala ambapo wanafunzi hao walishambuliwa, na mmoja wao kuvuliwa nguo, Bw Kijazi amesema huenda kisa hicho kilitokana na suitafahamu.
“Kilicho muhimu ni tuangalie siku za usoni kwa sababu tusipofanya hivyo tutapotea. Tunahitaji kutatua tatizo la sasa lakini pia tuangalie mikakati ya muda mrefu,” ameambia wanahabari.
“Nimeridhishwa na hatua za kiusalama ambazo zimechukuliwa na serikali hapa. Kuna maafisa ambao wamesimamishwa kazi.”
Balozi huyo alikata kutaja kisa hicho kama cha ubaguzi wa rangi.
“Hatukutaka kuangazia masuala ya ubaguzi wa rangi na mambo mengine kwa sababu nadhani vyombo vya habari vinapendezwa sana na hilo. Tumejadiliana kuhusu masuala halisi na hatua madhubuti ambazo tayari zimechukuliwa na serikali ya hapa,” amesema.
Bw Kijazi alisafiri hadi Bangalore akiandamana na maafisa wawili wa wizara ya mambo ya nje ya India ambapo walikutana na waziri wa mambo ya ndani wa jimbo la Karnataka Dkt G Parameshwara na wakuu wa polisi wa jimbo hilo.
Polisi mjini Bangalore wamewakamata watu tisa kuhusiana na kisa hicho.
Mkuu wa kituo cha polisi cha Soldevenahalli pia amesimamishwa kazi kwa tuhuma kwamba hakuchunguza kwa undani kisa hicho baada ya mmoja wa wanafunzi hao kupiga ripoti.
Konstebo wa polisi pia amesimamishwa kazi kwa kutochukua hatua kuzuia wanafunzi hao wasishambuliwe na umati
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:40 AM | Be the first to comment!

Tetemeko baya lakumba Taiwan



Tetemeko kubwa la ardhi limekumba Taiwan Kusini, na kuangusha jengo moja la ghorofa 17 ambapo hadi kufikia sasa watu watatu wamethibitishwa kufariki.
Tetemeko hilo la kipimo cha Ritcher 6.4 lilitokea karibu na mji wa Tainan.
Zaidi ya watu 200 wameokolewa kutoka kwa jengo hilo, ingawa waokoaji wangali wanajaribu kuwafikia watu wengine ambao inadhaniwa wangali wamekwama katika mabaki ya jengo hilo.
Tetemeko hilo liligonga usiku wa manane wakati watu wengi walikuwa wamelala.
Kumetokea matetemeko mengine madogo matano mda mfupi baada ya tetemeko hilo kuu.
Idara ya kusimamia maswala ya chini ya radhi inasema kuwa tetemeko hilo lilitokea sehemu ya juu pekee, hali ambayo husababisha madhara makubwa zaidi
Read More

February 4, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 7:52 AM | Be the first to comment!

Kinana aanza shughuli mbalimbali za maendeleo kuelekea siku ya maadhimisho ya miaka 39 ya Kuzaliwa kwa CCM




Wajumbe wa Kamati ya Siasa CCM mkoa wakisikiliza wakati Kaimu Katibu wa Mkoa Ndugu Mary Maziku akiwakilisha taarifa za maandalizi ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye ofisi za CCM mkoa wa Singida
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 7:46 AM | Be the first to comment!

Mama Janeth Magufuli atembelea kambi ya wazee wasiojiweza na walemavu ya Nunge

Mke wa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli, mama Janeth Magufuli ametembelea katika kituo cha Nunge kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam ambacho kinatumika kuhifadhi wazee wasiojiweza na walemavu.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi mchele, unga na maharage Mzee Anthony Kingongoti Mwenyekiti wa wakaazi wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao



Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na wagonjwa waliofika kupata huduma katika zahanati ya  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao

Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 7:40 AM | Be the first to comment!

Kasi ya Rais Dkt. Magufuli yagonga mwamba kwa polisi Mlandizi




Askari wa Kikosi cha Polisi cha Usalama barabarani, Kituo cha Polisi Mlandizi wamewasotesha kwa takribani masaa mawili  na nusu wanahabari kupata risiti ya malipo ya faini aliyotozwa dereva wao baada ya kudaiwa kufanya kosa la kutaka kulipita gari lingine sehemu isiyoruhusiwa.
Sakata hilo lilianza wakati polisi alipolisimamisha gari hilo katika Kituo cha Visiga, Mlandizi, wilayani Kibaha, Pwani ambapo alimuomba dereva leseni yake na kumuamuru ateremke ili ajieleze akiwa nje ya gari na hatimaye kumlipisha faini ya sh. 30,000 kwa kosa hilo.
Baada ya wanahabari waliokuwa kwenye gari hilo kumsubiri dereva kwa takribani nusu saa, waliamua kuteremka kumfuata kujua kinachoendelea, kwani walikuwa wana haraka ya kufika Dodoma muda waliopangiwa  ili waungane na msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenda Singida kwenye maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM.
Lakini baada ya mmoja wao kuwauliza trafiki sababu zinazosababisha kutomwachia dereva, walijibu kwa kashfa na kejeli, wakihoji kwani nyie ni akina nani? na dereva wenu asipolipa faini basi watakaa hapo kituoni hadi jioni.
Mmoja wa wanahabari hao alilipa faini ya sh. 30,000 na kuomba risiti, hapo ndo songombingo ilianza ambapo Trafiki wa kike alijibu kuwa hawana risti bali kinachofanyika pale ni kuandikiwa tu taarifa ya kosa lao na kwenda Kituo cha Polisi cha Mlandizi kilichopo takribani umbali wa Km 5, na wengine waliokamatwa kwa makosa mbalimbali ya usalama barabarani waliamuliwa kwenda kupata risiti katika kituo hicho.
Mabishano makubwa yalitokea hapo baina ya Trafiki na wanahabari waliokuwa wanahoji ni kwa nini kitabu cha risiti wala mashine za kielekroniki havipo hapo ili kurahisisha kazi. Askari wa kike na mmoja wa kiume walijibu kuwa wasifundishwe kazi.
“Msitupotezee muda hapa, nendeni Mlandizi, mkapate hiyo risiti,”alisema trafiki wa kike. Wakati anasema hivyo kumbe mhasibu wao alikuwepo palepale Visiga, lakini bila kuwaambia ondokeni naye ili akawahudumie.”
Pia, mmoja wa Trafiki aliuponda sana utaratibu wa wakosaji kulipia faini kwa kutumia mashine za elekroniki akidai kwamba ni hasara kwa trafiki na madereva ni bora mashine hizo ziishie Dar es Salaam zisipelekwe Mkoa wa Pwani.
Trafiki wengine walisikika wakisema kuwa hivi hawa jamaa wanaolazimisha kupewa risiti ni akina nani, waache waende zao, wakafie mbali.
Maneno hayo yalionekana kuwaudhi wanahabari na kuamua kuondoka kwenda Kituo cha Polisi Mlandizi, kufuatilia risiti, lakini walichokikuta huko ni maajabu, hasa ya kuambiwa kuwa Mhasibu hayupo ofisini kwake amekwenda kununua peni.
Baada ya wanahabari hao kusubiri kwa takribani saa moja, waliamua kwenda kaunta kuulizia na kuomba kuzungumza na Mkuu wa Kituo ili awasaidie kupata risiti wawahi kwenda Dodoma, lakini mmoja wa askari aliyekuwa zamu aliwajibu kuwa Mkuu wa Kituo hajafika ofisini amepitia Kibaha Mjini kwenye mkutano.
Alipoombwa awasaidie kumpata mhasibu, askari huyo alitoka nje hadi ofisi ya Mhasibu alipomkosa akaamua kumpigia simu na kuwajibu kuwa ametoka mara moja kwenda kununua peni. Jambo hilo liliwashangaza sana wanahabari na kuanza kuhoji kwamba iweje kitendo cha kununua peni  kitumie muda wote huo na kusababisha watu wakiwemo wao kukosa huduma tena asubuhi majira ya saa 3.
Mmoja wa wananchi aliyekwenda kituoni kupata huduma ya risiti, alisikika akilalamika kuwa tabia hiyo ya kuchelewesha kutoa huduma ipo sana kituoni hapo na kwamba wanaoonekana kabisa hawaendani na kasi ya kufanya kazi anayoitaka Rais Dk  John Magufuli ya ‘Hapa Kazi Tu’.
Mle ndani ya Kituo cha Polisi walisikika wakiulizana kwamba hivi hawa watu wanaowasumbua na kutaka kuzungumza na mkuu wa kituo ni akina nani hawa, eti wanataka risiti, ebu tumpigie simu mhasibu aje atuondolee balaa hapa.
Baada ya muda askari mwenye E 3275 alitoka nje na kuwaambia wanahabari kuwa mhasibu amepigiwa simu atakuja muda si mrefu mhudumiwe muondoke, lakini mmoja wa wanahabari hao anayemiliki blogu ya Full Shangwe, John Bukuku,  alihoji kuwa hivi ni kwanini polisi wa kituo hicho hawaendani na kasi ya Rais Dk. Magufuli? alijibu kuwa kwani kuna nini?
Baada ya muda Mhasibu aliwasili kwa Bodaboda, na alipofika aliwakebehi wanahabari kwamba anawashangaa kwa yeye kumuacha kule Visiga alikokuwa nao na kuwahi kituoni, ndipo wanahabari nao wakashangaa kumuona tena kituoni hapo wakati wlipofika kituoni waliambiwa ameenda kununua peni.
Dereva alimwambia haya twende ukachukue risiti yako muondoke na watu wako. Dereva aliingia na kupatiwa risiti kutoka kwenye kitabu kipya ambacho kwa mujibu wa dereva kilionekana dhahiri kuwa ni kipya.
Lakini kwa masaa yote waliyokaa wanahabari kituoni hapo (takribani masaa mawili), hawakuwaona madereva wa magari waliokamatwa pamoja na gari lao na kuandikiwa makosa na faini pale Visiga, hawakufika Kituo cha Polisi kupatiwa risiti, kitendo ambacho kinaashiria fedha wanazolipishwa madereva kwa kutenda makosa hazitolewi risiti, hivyo mapato ya serikali kupotelea mifukoni mwa baadhi ya askari wa kikosi cha usalama barabarani.
Baada ya wanahabari hao kupata risiti majira ya saa 4:15 waliamua kuondoka kituoni hapo kuanza safari ya kwenda Dodoma kuwahi msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Abdulrahman Kinana uliokuwa unawasubiri kwenda Singida.
Read More