Tetemeko kubwa la ardhi limekumba Taiwan Kusini, na kuangusha jengo moja la ghorofa 17 ambapo hadi kufikia sasa watu watatu wamethibitishwa kufariki.
Tetemeko hilo la kipimo cha Ritcher 6.4 lilitokea karibu na mji wa Tainan.
Zaidi ya watu 200 wameokolewa kutoka kwa jengo hilo, ingawa waokoaji wangali wanajaribu kuwafikia watu wengine ambao inadhaniwa wangali wamekwama katika mabaki ya jengo hilo.
Tetemeko hilo liligonga usiku wa manane wakati watu wengi walikuwa wamelala.
Kumetokea matetemeko mengine madogo matano mda mfupi baada ya tetemeko hilo kuu.
Idara ya kusimamia maswala ya chini ya radhi inasema kuwa tetemeko hilo lilitokea sehemu ya juu pekee, hali ambayo husababisha madhara makubwa zaidi