Thailand imezindua kampeni kabla ya siku ya wapendanao ya Valentine ikiwataka vijana kutosikia aibu wanapobeba mipira ya kondumu.
Mpango huo unaonekana kubadilika ikilinganishwa na kampeni zilizokuwa zikifanywa hapo awali,ambapo vijana walihamasishwa kuzuru maeneo ya kidini na baadaye kwenda nyumbani baada ya mikutano na wapenzi wao badala ya kushiriki katika ngono.
Thailand ina idadi kubwa ya wasichana waliotungwa mimba duniani pamoja na na viwango vya juu vya magonjwa yanayoambukizwa kupitia ngono
Kampeni hiyo inayotarajiwa kuendelea hadi mwaka 2019,inaambatana na mipiango ya hivi karibuni inayolenga kuangazia mimba za vijana.
Mamlaka zimehamasisha umuhimu wa kutumia mipiria ya kondomu katika miaka ya nyuma pamoja na kuwashuri vijana kutoshiriki ngono.
Lakini mwaka huu wamesema watalenga kupunguza unyanyapaa kuhusu utumizi wa kondomu pamoja na kurahisisha upatikanaji wake mbali na kuimarisha mipira hiyo.
Msemaji wa Wizara ya afya nchini Thailand Lertwilairrattanapong amesema kwamba vijana hawafai kuaibishwa kuhusu ununuzi wa mipira ya kondomu.
''Jamii pia inafaa kukubali kwamba vijana wasichana wanafaa kununua kondomu,ambazo ni bora badala ya wasichana hao kupata mimba'',akisema.