Advertising

  • Matunda

    faida ya tunda la KITZ
  • Matunda

    kula matunda kwa wingi
  • GYm

    Mazoezi muhimu kwa afya
  • Mazoezi

    dada anaimarisha misuli
  • Jovago

    Promoo siku ya watendao

February 6, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:57 AM | Be the first to comment!

Twitter yazifunga akaunti za IS


Mtandao wa kijamii wa Twitter, umesema kuwa umesimamisha akaunti zaidi ya 120,000 kwa uchochezi tangu katikati mwa mwaka uliopita.
Kampuni hiyo inasema akaunti nyingi zilikuwa na uhusiano mkubwa ma kundi la kigaidi la Islamic State.
Twitter walisema kuwa kutokana na hatua hiyo mawasiliano ya kigaidi imeanza kutoweka kwenye mtandao wao.
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:36 AM | Be the first to comment!

Washauriwa kubeba Kondomu siku ya Valentine

Thailand imezindua kampeni kabla ya siku ya wapendanao ya Valentine ikiwataka vijana kutosikia aibu wanapobeba mipira ya kondumu.


Mpango huo unaonekana kubadilika ikilinganishwa na kampeni zilizokuwa zikifanywa hapo awali,ambapo vijana walihamasishwa kuzuru maeneo ya kidini na baadaye kwenda nyumbani baada ya mikutano na wapenzi wao badala ya kushiriki katika ngono.
Thailand ina idadi kubwa ya wasichana waliotungwa mimba duniani pamoja na na viwango vya juu vya magonjwa yanayoambukizwa kupitia ngono
Kampeni hiyo inayotarajiwa kuendelea hadi mwaka 2019,inaambatana na mipiango ya hivi karibuni inayolenga kuangazia mimba za vijana.
Mamlaka zimehamasisha umuhimu wa kutumia mipiria ya kondomu katika miaka ya nyuma pamoja na kuwashuri vijana kutoshiriki ngono.
Lakini mwaka huu wamesema watalenga kupunguza unyanyapaa kuhusu utumizi wa kondomu pamoja na kurahisisha upatikanaji wake mbali na kuimarisha mipira hiyo.
Msemaji wa Wizara ya afya nchini Thailand Lertwilairrattanapong amesema kwamba vijana hawafai kuaibishwa kuhusu ununuzi wa mipira ya kondomu.
''Jamii pia inafaa kukubali kwamba vijana wasichana wanafaa kununua kondomu,ambazo ni bora badala ya wasichana hao kupata mimba'',akisema.
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:25 AM | Be the first to comment!

Alikiba azindua video ya Lupela, mastaa wenzie wampa kampani






Alikiba amezindua video ya wimbo wake Lupela Alhamis hii kwenye hoteli ya Slipway jijini Dar es Salaam.

Alikiba akiongea mbele ya wageni waalikwa
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na mastaa kibao walioenda kumpa kampani. Video hiyo iliyofanyika nchini Marekani na sehemu ya mradi wa Wild Aid 
Inamuonesha Kiba akicheza dance ya kukata na shoka na msichana mrembo wa Kimarekani aliyechukua uhusika wa Lupela.
Mastaa waliouhudhuria uzinduzi huo ni pamoja na Weusi, Wema Sepetu, Jokate, Vanessa Mdee, Lady Jaydee, Navy Kenzo, Ommy Dimpoz, Mr Blue, Mwana FA, Barakah Da Prince na wengine.
Pia walikuwepo watangazaji mbalimbali kama B12 na Perfect Crispin wa Clouds FM, Dulla wa EA Radio na wengine. Mama yake Alikiba pamoja na dada yake nao walikuwepo
                                                

Read More

February 4, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 4:44 AM | Be the first to comment!

Wabunifu chipukizi walivyolipamba jukwaa la Lady In Red Fashion show 2016




Wabunifu zaidi ya thelasini (30) wameweza kulipamba vilivyo jukwaa la mitindo hapa nchini la Lady In Red fashion show 2016 lililofanyika jijini Dar es Salaam huku likishuhudiwa na wadau mbalimbali wa mitindo hapa nchini.Jukwaa hilo linaloandaliwa kila mwaka na Mama wa Mitindo nchini,  Asya Idarous Khamsini  ameelezea kuwa lengo la jukwaa hilo ni kuwa kimbilio la wabunifu chipukizi na kama darasa la tasnia hiyo.Onesho hilo kwa mwaka huu ni la 12 tokea kuanzishwa kwake huku likia limewatoa wabunifu chipukizi mbalimbali hapa nchini ambao wanamajina makubwa kwa sasa

Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 4:36 AM | Be the first to comment!

Dayna Nyange anatukaribisha kuitazama hii video yake mpya ‘angejua’

Dayna Nyange ni kipaji kingine tulichonacho kwenye muziki wa bongofleva Tanzania, 2016 ameianzisha kwa kutusogezea hii single yake ya kwanza kwa mwaka huu inaitwa ‘angejua‘ na video yake mpya ndio hii                angejua





                           
Read More

February 3, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 9:19 PM | Be the first to comment!

Kweli Diamond Platnum wa Kimataifa, Azoa Tuzo Nyingine Nchini Uganda



Mwanamziki anaye ipeperusha vizuri Bendera ya Tanzania ambaye kwa sasa anatamba na kibao cha ‘Utanipenda‘ Diamond Platnumz amezidi kuziandika vichwa vya magazeti na mitandao katika ulimwengu wa sanaa baada ya usiku wa jana kuzinyakua tuzo mbili za Hipipo Awards zilizofanyika Uganda.
Ushindi alioupata ni Nyimbo bora Afrika Mashariki na Video bora Afrika Mashariki ambazo zote ni kupitia wimbo wa Nana.
Baada ya ushindi kupitia account yake ya Instagram Diamond aliandika maneno haya
“Wow! Realy wanna Thank GOD for keep blessing the innocent kid… also wana thank all Media and My Loyal fans for the Big love.. Two Awards tonight on @HipipoAwardsUGANDA…EAST AFRICA SUPER HIT#NANA and EAST AFRICA BEST VIDEO#NANA many thanks to my brother@2niteflavour
@i_am_godfather and all Behind this Hit!!!… thanks alot @HIPIPOAwards for keep supporting the real African talent!
(Wadau kijana wenu nimefanikiwa kushinda tunzo mbili Usiku wa leo kama NYIMBO BORA AFRICA MASHARIKI#NANA na VIDEO BORA AFRICA MASHARIKI #NANA nawashkuru sana kwa kura na support zote mnazoendelea kunipa….. tafadhali nisaidieni kuhesabu ni tunzo ngapi tumechukua tangu Mwaka 2016 uanze? ) shukran sana“
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 9:16 PM | Be the first to comment!

Adele Asisitiza Songi lake Jipya la Hello Hajaliruhusu Kupigwa Bila Idhini



Mwanamuziki Muingereza aliyegonga vichwa habari na kukonga nyoyo za mamilioni ya watu kote duniani kwa wimbo wake maararufu ”Hello” Adele amekariri kuwa hajatoa idhini yeyote kwa wimbo wake kutumika katika mikutano ya hadhara ya kisasa nchini Marekani.
Kupitia kwa msemaji wake, Adele anasema kuwa japo muaniaji tikiti ya urais wa chama cha Republican Donald Trump amekuwa akitumia wimbo wake uliotamba mwaka wa 2011 wa “Rolling in the Deep” katika mikutano ya hadhara katika jimbo la Iowa.
Vile vile mgombea mwengine wa tikiti ya urais Mike Huckabee alitumia wimbo mpya kabisa wa Adele “Hello.” katika video moja ya kampeini yake iliyochapishwa kwenye mtandao wa Youtube.
“Adele hajatoa idhini ya mtu yeyote kutumia wimbo wake katika kampeini za kisiasa. Alisema kupitia barua pepe.
Hata hivyo barua hiyo haikubainisha iwapo mwanamuziki huyo huenda akachukua hatua za kinidhamu dhidi ya wale wote wanaocheza nyimbo zake bila Idhini.
Adele ambaye albam yake ya “25” ndiyo iliyouzwa sana nchini Marekani mwaka uliopita ndiye mwanamuziki wa pekee ambaye nyimbo zake zimetumika katika kampeini ya vyama vyote nchini Marekani.
Mwaka uliopita kundi la waimbaji wa muziki chapa Rock, R.E.M. walimuonya bwana Trump dhidi ya kutumia nyimbo zao katika mikutano ya kisiasa.
Trump alikuwa ametumia wimbo waoa wa “It’s the End of the World”.
Isitoshe msanii mwengine Frankie Sullivan hakufurahishwa na matumizi ya wimbo wake uliovuma mwaka wa 1982 t “Eye of the Tiger,” katika mkutano wa wanahabari uliohudhuriwa na Kim Davis, wakala wa jimbo la Kentucky aliyefungwa jela kwa kukataa kutoa vyeti vya ndoa kwa wapenzi wa jinsia moja wanaofunga ndoa katika mji huo
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 9:14 PM | Be the first to comment!

Kampuni ya Jay Z imempeleka Mahakamani Rita Ora



Kampuni ya kurekodi ya Jay Z’s Roc Nation, imemshtaki mwanamuziki Rita Ora ikidai alivunja kandarasi yake mbali na kutotengeza idadi ya albamu alizoahidi.
Kesi hiyo imeanzishwa mjini New York wiki sita baada ya Rita kuanzisha mashtaka dhidi ya kampuni hiyo mjini Los Angeles.
Rita anadai kwamba kampuni hiyo ina kandarasi haramu naye na kwamba anaomba kutoka.
Rita Ora alijiunga na kampuni hiyo akiwa na umri wa miaka 18 na alikuwa miongoni mwa wanamuziki wa kwanza kusajiliwa na Jay Z.
Tangu ajiunge na kampuni hiyo ya kurekodi muziki ,Rita ametoa albamu moja ya kibinafsi ambayo ni yake ya kwanza mwaka 2012.
Hatahivyo kampuni ya Roc Nation imesema itataka kulipwa dola milioni 2.4 ikisema kuwa imetumia zaidi ya dola milioni 2 kutengeneza na kuiuza albamu ya pili ya mwanamuziki huyo ambayo haijatoka.



Kulingana na ukurasa wa sita wa gazeti la The New York Post,kampuni hiyo inadai kwamba mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 25 aliingia katika kandarasi ya kutoa albamu tano na kampuni hiyo lakini ametoa albamu moja kufikia sasa.
Roc Nation inasema kuwa ilimsajili Rita Ora alipokuwa hajulikani na imemuuzia kazi yake na kuwekeza mamilioni ya madola za kurekodi na gharama nyengine hivyobasi kumsaidia Bi. Ora kupata ufanisi na kuwa maarufu
Read More