Mwanamuziki Muingereza aliyegonga vichwa habari na kukonga nyoyo za mamilioni ya watu kote duniani kwa wimbo wake maararufu ”Hello” Adele amekariri kuwa hajatoa idhini yeyote kwa wimbo wake kutumika katika mikutano ya hadhara ya kisasa nchini Marekani.
Kupitia kwa msemaji wake, Adele anasema kuwa japo muaniaji tikiti ya urais wa chama cha Republican Donald Trump amekuwa akitumia wimbo wake uliotamba mwaka wa 2011 wa “Rolling in the Deep” katika mikutano ya hadhara katika jimbo la Iowa.
Vile vile mgombea mwengine wa tikiti ya urais Mike Huckabee alitumia wimbo mpya kabisa wa Adele “Hello.” katika video moja ya kampeini yake iliyochapishwa kwenye mtandao wa Youtube.
“Adele hajatoa idhini ya mtu yeyote kutumia wimbo wake katika kampeini za kisiasa. Alisema kupitia barua pepe.
Hata hivyo barua hiyo haikubainisha iwapo mwanamuziki huyo huenda akachukua hatua za kinidhamu dhidi ya wale wote wanaocheza nyimbo zake bila Idhini.
Adele ambaye albam yake ya “25” ndiyo iliyouzwa sana nchini Marekani mwaka uliopita ndiye mwanamuziki wa pekee ambaye nyimbo zake zimetumika katika kampeini ya vyama vyote nchini Marekani.
Mwaka uliopita kundi la waimbaji wa muziki chapa Rock, R.E.M. walimuonya bwana Trump dhidi ya kutumia nyimbo zao katika mikutano ya kisiasa.
Trump alikuwa ametumia wimbo waoa wa “It’s the End of the World”.
Isitoshe msanii mwengine Frankie Sullivan hakufurahishwa na matumizi ya wimbo wake uliovuma mwaka wa 1982 t “Eye of the Tiger,” katika mkutano wa wanahabari uliohudhuriwa na Kim Davis, wakala wa jimbo la Kentucky aliyefungwa jela kwa kukataa kutoa vyeti vya ndoa kwa wapenzi wa jinsia moja wanaofunga ndoa katika mji huo