Advertising

  • Matunda

    faida ya tunda la KITZ
  • Matunda

    kula matunda kwa wingi
  • GYm

    Mazoezi muhimu kwa afya
  • Mazoezi

    dada anaimarisha misuli
  • Jovago

    Promoo siku ya watendao

February 3, 2016

Mr Mtinangi

UGONJWA WA KANSA NI NINI?Tiba Ya Kansa

Mr Mtinangi | 12:34 PM |

Tiba ya ugonjwa huu wa saratani inatolewa kwa kutegemea aina ya kansa aliyo nayo mgonjwa, kansa hiyo imeenea kiasi gani katika mwili wa mgonjwa huyo, umri wa mgonjwa, afya aliyo nayo na mambo mengine yanayoendana na mgonjwa huyo. Hakuna tiba ya wote na mara nyingine mgonjwa atapewa mchanganyiko wa tiba
na uangalizi. Tiba zilizopo zinaangukia katika makundi yafuatayo: upasuaji, mionzi, chemotherapy, immunotherapy, hormone therapy au gene therapy. Tutapitia kwa kifupi aina hizi za tiba za kansa hapa
chini.
Tiba Ya Kansa Kwa Upasuaji: Tiba ya kansa kwa upasuaji ndiyo tiba ambayo imetumika kwa muda mrefu zaidi kuliko tiba nyingine zote. Endapo kansa ya eneo moja haijaenea kwenye sehemu nyingine ya mwili, mgonjwa anaweza kupona kabisa kwa tiba hii ya uapasuaji. Mafanikio makubwa kabisa ya tiba hii yameonekana katika tiba za kansa za maziwa na kansa za tezi dume. Kansa ikiishaenea toka sehemu moja ya mwili hadi nyingine, tiba hii haiwezi kuondoa seli zote za kansa.
Tiba hii inapotumika kwa sasa hivi kuondoa uvimbe, madaktari huondoa kipande cha seli za kawaida kuzunguka eneo la seli za kansa kuhakikisha kuwa seli zote za kansa zimeondolewa. Mgonjwa hulazilka kubaki kwenye nusu-kauti wakati vipimo vinachukuliwa kuhakikisha kuwa eneo la kida lililoondolewa halina seli za kansa na kwa bahati mbaya wakigundua uwepo wa seli hizo za kansa, humrudia mgonjwa na kukata kipande zaidi.
Maendeleo ya teknolojia sasa hivi yamekuja na kifaa kipya kitwacho IKnife ambacho chenyewe hugundua seli za kansa hivyo kuwawezesha madaktari kujua upeo wa eneo la kulikata na kuondoa seli zote za kansa bila ya kusubiri vipimo vya kwenye maabara.
Tiba Ya kansa Kwa Mionzi: Tiba hii ambayo pia huitwa radiotherapy huondoa kansa kwa kuelekeza mionzi yenye nguvu kwenye seli za kansa. Mionzi hii huziharibu seli hizo na kuzifanya zijiue zenyewe. Tiba hii ya mionzi hutumia mionzi yenye nguvu inayoitwa gamma-rays inayotolewa na machine maalumu.
Tiba za mwanzo kwa kutumia mionzi zilikuwa na madhara makubwa ya kuharibu seli za kawaida lakini maendeleo katika teknolojia yameiboresha tiba hii na sasa mionzi hiyo ina uwezo wa kulenga seli za kansa kwa uhakika zaidi na hivyo kutoleta madhara kwa seli za kawaida. Radiotherapy hutumika kufanya uvimbe unywee au kuharibu seli za kansa (pamoja na kansa za aina ya leukemia na lyphoma). Tiba hii hutumika pia pamoja na tiba nyingine za kansa.
Tiba Ya Kansa Ya Chemotherapy: Chemotherapy ni tiba inayotumia kemikali ambazo zinavuruga tendo la seli za mwili kujigawa na kusababisha seli hizo kujiua zenyewe. Tiba hii hulenga zile seli ambazo zinajigawa kwa haraka na kwa kawaida hutumika kutibu kansa zilizoenea kutoka eneo moja ya mwili hadi eneo jingine
(metastatic cancers) kwa sababu kemikali hizi zina uwezo wa kusambaa katika mwili wote wa mgonjwa. Hii ni tiba ya lazima kwa aina fulani ya kansa za aina ya leukemia na lymphoma.
                                                
hemotherapy hutolewa kwa vipindi ili mwili uweze kupona katikati ya dozi moja na nyingine. Madhara ya tiba hii ni pamoja na
kunyonyoka nywele, kichefuchefu, uchovu wa mwili na kutapika. Ni tiba ambayo mara nyingine hutolewa kwenda sambamba na tiba nyingine za saratani.
Tiba Ya kansa Ya Immunotherapy: Immunotherapy ni tiba inayokusudia kuziongeza kinga za mwili ili mwili uweze kupambana na uvimbe. Sindano inweza kudungwa kwenye eneo lililoathirika ili uvimbe unywee (Local immunotherapy). Namna nyingine ni kuuwezesha mwili wote kuongeza kinga ili kupambana na uvimbe katika sehemu zote za mwili (Systemic immunotherapy). Tiba hii bado ni changa lakini zimeonyesha mafanikio katika kutibu kansa za maziwa.
Utafiti unaendelea na kila siku wanasayansi wanakuja na tiba nyigine na kuzijaribu. Tiba ambazo zipo kwenye majaribio ni pamoja na Gene therapy yenye lengo la kukarabati genes zilizoharibika

Mr Mtinangi

About Mr Mtinangi -

Hajasomea uandishi wa habari yeye anapenda kuisaidia jamii kufahamu yale yanayotokea duniani japo kwa kiasi kidogo na nifuraha kwako hata kama mtu mmoja akipata taarifa mpya kupitia moojuhudi,namini katika haba ile na ile hujaza kibaba

Subscribe to this Blog via Email :