Aliyesimama mbele ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jovago Afrika Mashariki, Estelle Verdier-Watine akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
KAMPUNI ya Jovago Tanzania ambayo ni wadau wakubwa wa sekta ya utalii nchini Tanzania imeahidi kuwapeleka wapendanao (Wana Valentine) kupumzika kwa siku moja kwenye Hoteli ya kisasa ya Ramada ya jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wapendanao duniani (Valentine’s day). Akizungumza na wanahabari Meneja Uhusiano wa Jovago Tanzania, Lilian Kisasa alisema kampuni hiyo kwa kushirikiana na Hoteli ya Ramada imeandaa shindano hilo ambapo mshindi (Bibi na Bwana) atakayefanikiwa kupata ofa hiyo ni yule atakayekuwa na idadi kubwa ya ‘LIKE’ mara baada ya ku-post picha yoyote yenye ujumbe wa siku ya wapendanao kwenye mtandao wa Instagram na kutaja neno kiungo cha shindano lenyewe #JOVAGOVALENTINE. Alisema mshindi pamoja na mwenza wake watalipiwa gharama za chakula na malazi kwa siku moja kwenye hoteli hiyo ya kisasa. Februari 14 wapendanao duniani huitumia siku hii kusherehekea na wapendwa wao wakijumuika kula na kunywa. Nifahamishe tunakuletea historia fupi ya siku hii ya wapendanao aka Valentine’s day