Advertising

  • Matunda

    faida ya tunda la KITZ
  • Matunda

    kula matunda kwa wingi
  • GYm

    Mazoezi muhimu kwa afya
  • Mazoezi

    dada anaimarisha misuli
  • Jovago

    Promoo siku ya watendao

February 4, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 1:24 AM | Be the first to comment!

Mambo ya Kuzingatia Wakati Mnaanza Kuchumbiana

HAMNA raha ya pekee kama kuwa kwenye mahusiano ambayo mume na mke au ‘boyfriend’ na ‘girlfriend’ wanaelewana vizuri. Ni vigumu kupata mtu ambaye mnaelewana kila jambo.
Sio lazima kama mwenzako anasapoti Arsenal na wewe usapoti Arsenal. Wataalamu wa masuala ya mahusiano wanashauri kuwa, ili uweze kuishi vizuri na mtu kama mume na mke ni vizuri kuwa mnaelewana kwenye masuala ya msingi na mnashea visheni moja ya maisha. Kati ya masuala ya msingi ambayo ni muhimu kuwa kwenye ukurasa mmoja ni Matumizi ya fedha na kujamiiana. Haya ndio mambo makuu mawili ambayo yanasababisha ndoa nyingi sana kuvunjika. Utajuaje matumizi ya mtu ya fedha kama ndio wachumba na bado hamjaanza kuishi pamoja? Ni rahisi, utakuwa unajua mwenzako anafanya kazi wapi, dadisi kwa watu kuwa kazi kama anayofanya mwenzako ina mshahara kiasi gani pamoja na dili nyingine anazofanya, ukishajua hilo anza kuchunguza matumizi yake, vitu anavyonunua, mavazi anayovaa, gari analoendesha na mambo mengine kama hayo. Kama matumizi yake yako juu kuliko kipato chake, jaribu kuongea naye na kumshauri kuhusu matumizi yake.
Tunakuja kwenye swala ya kujamiiana, hili ndio jambo la pili ambalo linaongoza kwa kusababisha mahusiano kuvunjika hasa kwa kizazi kipya. Miaka kama 30 iliyopita, watu wengi walikuwa wanaoana wakiwa bado bikra. Jambo zuri la kuoana mkiwa bado bikra ni kwamba wote mnaingia mkiwa hamna ujuzi na hamna wasichana au wanaume wengine ambao umelala nao wa kulinganishe ujuzi wao na mke wako au mume wako. Tatizo lipo siku hizi ambapo watu wanaoana wakiwa na ujuzi tofauti (diffetent experience level) ndio maana michepuko imezidi.
Wanadamu tumezoea kulingalisha vitu, pale utakapoanza tu kulinganisha utaalamu wa mwenzako na wanawake au wanaume wako wa zamani ndio utakapoanza kumuona mwenzako hafai. Jitahidi kutolinganisha uhusiano wako na watu waliopita, hamna watu wawili wanafanana kila kitu humu duniani. Kabla sijamalizia, napenda kusisitizia kuhusu umuhimu wa mawasiliano, sio kupigiana simu na kuandikiana message kwenye whatsapp, kutaneni mahali, wekeni simu zenu mbali na sio unaangalia picha instagram wakati unaongea na mwenzako.
Tafuteni sehemu iliyotulia mara mbili kwa wiki mzungumze na kupanga maisha yenu, usiogope wala kuona haya kuuliza swali lolote.
Read More

February 2, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 10:07 AM | Be the first to comment!

Zijue Tabia 7 za Wanawake wanao-Cheat

Kama mke wako, demu wako au side chick wako ana tabia zifuatazo, amesha-cheat kwako au ipo siku ataku-cheat.



1) Ana boreka haraka – Wanawake wanaoboreka haraka nirahisi kutafuta mwanaume mwingine wa kum-entertain, muda sio mrefu huyo mwanaume atachoka kum-entatain rafiki asiye na faida na ndio hapo atakapo anza kudai faida zake na wanaishia kuwa friends with benefits.
2) Marafiki wengi wa kiume – Mwanamke mwenye marafiki wengi wa kiume ni rahisi ku-cheat kwasababu anapata muda mwingi wa kuongea na wanaume wengine, watamsifia anavyopendeza, kama wewe unamwambia amependeza mara moja kwa wiki basi wenzako watamwambia anapendeza kila wanapoonana. Wataabza kumtoa out na mwisho wake ataona hao wanaume wamanjali kuliko wewe na kulala nao.
3) Anapenda attention – Wanawake wanaopenda attention ni rahisi kudanganyika. Wanaume wengi hasa ambao hawataki kuwa committed kwenye mahusiano yoyote wanatoa sana attention kwa wanawake. Mwanamke anayependa sana attention hawezi ridhishwa na attention ya mwanaume mmoja.
4) Anapenda vitu “material things” Wanawake wengi wanaopenda material things wanashindwa kupata kila kitu kutoka kwa waume zao au maboyfriend zao na kuishia kutafuta mwanaume mwingine ambaye ana uwezo wa kumnunulia vitu anavyotaka ili awatese wenzake kwenye instagram
5) Ana marafiki ambao ni michepuko – Umeshasikia usemi kuwa ndege wanaofanana huruka pamoja, hata kama demu wako hana tabia ya ku-cheat, akiwa anakaa sana na marafiki ambao wana-cheat na yeye atashawishika kujaribu. Kama mke wako au demu wako ana kupigia story za marafiki zake wanao-cheat mwambie aachane nao haraka sana.
6) Anapenda kufanya ngono kuliko wewe – kila mkimaliza kufanya tendo la ndoa mwenzako anakwambia anataka tena, na wewe humtimizii basi lazima tatafuta serengeti boy ambaye anamsikiliza na kumpa anachotaka.
7) Anaujuzi kitandani kuliko wewe – Wewe kama umeshawahi kuingia kwenye dancing floor na kucheza na mtu ambaye anajua kucheza kuliko wewe, unasubiria tu wimbo ukiisha ukakae chini kabla hujaaibishwa, au kama wewe ndio unayejua kucheza vizuri utatafuta mtu mwingine anayejua kucheza kama wewe. Kwenye tendo la ndoa ni hivyo hivyo kama mwenzako ana ujuzi kuliko wewe, inabidi ufanye mazoezi ufikie kwenye ujuzi wake la sivo muda sio mrefu atasubiri wimbo ukiisha akakae chini au atafute mtu mwingine anayejua kucheza kama yeye.
Demu wako au mchepuko wako una tabia moja wapo kati ya nilizozitaja hapo juu? Usisite kuacha comments hapo chini.

Read More

January 29, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 1:10 AM | Be the first to comment!

Shitka!!Tabia Kuu Tano Za Watu Waliofanikiwa Kimaisha!

Kwanza, kabla sijaendelea embu tuwekane sawa kuhus hii falsafa ya “kufanikiwa kimaisha”, ina maana gani haswa? Ukweli ni kwamba watu wengi wakisikia fulani amefanikiwa kimaisha, basi moja kwa moja wanafikiri au wanaamini mtu huyo atakuwa na pesa nyingiiii au kwa maneno mengine, mtu huyo ni tajiri fulani hivi. Pamoja na kwamba pesa ndio mtatuzi wa mahitaji mengi hapa duniani, lazima tukumbuke kwamba pesa ina uwezo wa kununulia kitanda cha gharama kubwa sana, lakini ukashindwa kulala katika kitanda hicho kwa msongo wa mawazo. Pia pesa inaweza ikakufanya uopoe mwenza mzuri kuliko wote duniani, lakini mwenza huyo asiwe na mapenzi ya dhati kwako.
Hapa tunajifunza kwamba ingawa pesa ni muhimu sana maishani, kufanikiwa au kutofanikiwa kwa mtu kimaisha hakuwezi kupimwa kwa kiasi tu cha pesa alichonacho. Mtu anaweza akawa na pesa, lakini akakosa raha kutokana na ukosefu wa amani ya ndani na nje ya mwili. Hivyo basi, Kufanikiwa au kutofanikiwa maishani kwa mtu, ni lazima pia kupimwe kwa mambo mengine muhimu kama uchamungu, ukarimu, maadili, busara, uvumilivu, na ujasiri (wa kufanya na kuishi na maamuzi magumu). Hivi “viambatanisho” 6 vya pesa ndio vinarutubisha na kudumisha pesa, na zaidi humfanya mtu afurahie (enjoy) pesa hizo. Kwa uzoefu wangu, mchanganyiko wa mambo haya yote muhimu, ndio humfanya mtu “afanikiwe kimaisha” kwa maana pana ya falsafa hiyo. Baada ya muhtahsari huu, tuendelee sasa na mada yetu, ambayo leo inagusia mambo makuu matano ya watu waliofanikiwa kama ifutavyo:
#1: Huishi Kwa Siku Za Baadae (Future), Na Sio Siku Zilizopita (Past). Bila shaka umeshasikia ule usemi wa siku nyingi kwamba “yaliyopita si ndwele, tugange yajayo”. Watu waliofanikiwa kimaisha huwa na tabia ya kutokatishwa tamaa na mambo ambayo yameshapita, na hayakwenda kama walivyotarajia, kwani siku zote huwa wanakubali matokeo ya kutofanikiwa kwao katika suala fulani na kujipanga upya kulikabili suala hilo. Siku zote hujizuia kuruhusu matukio ya kushindwa kwao kufanikiwa katika masuala fulani maishani, kushusha imani yao yakufanikiwa katika masuala ya baadae (future)

#2: Hawalii Shida Na Wala Hawana Kinyongo Hisia zako za siku kwa kiasi kikubwa zinategemea na wapi ulipoelekeza mawazo yako. Kwa mujibu wa mtaalam wa Saikolojia, Travis Bradberry, anaweka wazi kwamba “kama umeelekeza mawazo yako kwenye shida ambazo zinakukabili, basi unajijengea hisia hasi mwilini na kujiongezea mastresi kibao, ambayo yana athiri na kuzuia uwezo wako wa kufanya mambo ya kimaendeleo”. Hivyo basi, watu waliofanikiwa maishani huwa wanaelekeza mawazo yao kwenye masuala chanya, ili kupiga vita mastresi na kujiongezea uwezo wa kukomaa na mambo ya maendeleo. Pia, watu waliofanikiwa maishani huwa hawaendekezi kinyongo, kwani wanaelewa kuwa kuweka kinyongo katika masuala yaliyopita ni hatari sana kwa maendeleo. Vinyongo kama ilivyo kubebea shida mbeleko, ni vitu ambavyo huzalisha hisia hasi mwilini na kumfanya mtu kuwa na mastresi (au msongo wa mawazo), ambayo yana mzuia kufanya mambo ya maendeleo
#3: Hawatoi Kipaumbele Katika Ukamilifu. Hapa ina maanisha kwamba, watu waliofanikiwa maishani huwa hawapotezi muda katika kutafuta ukamilifu (perfection) katika mambo yao. Ni watu, ambao wanafaham kwamba binaadam ni viumbe dhaifu na ukamilifu ni wa Mungu peke yake. Hivyo basi, hii sifa inawasaidia sana linapokuja suala la kuridhika na kile walichoweza kufanya baada ya kujitahidi kwa uwezo wao. Hii inawafanya waendelee kujiamini, badala ya kujilaumu na kujihisi wamefeli kama wale watu wanaolenga ukamilifu katika ufanyaji wa mambo yao.


#4: Hawapotezi Muda Wao Na Watu Wenye Mawazo Hasi. Hii sifa ni muhimu sana na kwa ufupi ni muendelezo wa sifa #2, kwani ili mtu aendelee kubaki na mawazo chanya kwa mustakbali mzima wa maendeleo yake, ni lazima apinge kukaa na watu wenye mawazo hasi au walalamikaji. Kwa ung’eng’e wanasema “ don’t hangout with negative people!” Hapa wanazungumziwa marafiki, ndugu, na jamaa, yaani kuwa makini sana kuhusu watu unaokaa na kuzungumza nao kwa siku. Kama watu hawa wamejaa malalamiko tu kuhusu maisha yao siku nzima, basi jua wanagonjwa hatari sana na ni watu wa kukaa nao mbali, ili wasikuambukize gonjwa hilo hatari kwa maendeleo yako. Siku zote watu waliofanikiwa maishani (au wale walio mbioni kufanikiwa) huwa wanajihusisha na watu wenye mawazo chanya na matumaini tele kuhusu mustakbali wa maisha yao.
#5: Hawaoni Hatari Kusema “Hapana!” Hii pia ni sifa muhimu sana, kwani watu wengi wanaostrago maishani, ni watu ambao wanataka kumridhisha kila mtu, kitu ambacho ni kigumu sana. Mbali na kwamba sifa moja wapo ya mtu aliyefanikiwa maishani ni ukarimu, watu hawa pia wana ujasiri wa kusema hapana katika mambo ambayo hawataki au hawana muda wa kufanya. Ni watu ambao hawazunguki mbuyu linapokuja suala la kumwambia mtu kwamba ombi lao kwao limekataliwa. Hapa sio tu kwa wale watu wanaopenda kupiga mizinga ya pesa (ambayo mengine haina msingi wowote), bali pia kusema hapana linapokuja suala la kuombwa msaada wa kikazi na washirika wa biashara au ajira. Watu waliofanikiwa maishani hawaoni hatari kukataa kutoa msaada wa kikazi kwa watu wengine, ili kujipa muda zaidi na uwezo wa kufanya kazi zao.
Anza kufanya uchunguzi wako leo kwa watu unaowafaham, ambao “wamefanikiwa maishani” na utaona mifano hai ya sifa hizi au kama tayari unawafaham watu hao, basi tupe maoni yako kwa faida ya wasomaji wote!


Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 1:01 AM | Be the first to comment!

Karibu na Zijue Faida Tatu za Tendo la Ndoa!


                                            

Watu wanaoshiriki tendo la ndoa mara kwa mara, huwa hawa umwi umwi hovyo”, anasema Dkt.Yvonne K. Fullbright, mtaalam wa afya ya tendo la kujamiina. Baada ya nukuu hii kutoka kwa mtaalam, sio ajabu basi tukisikia kwamba faida kuu ya kwanza ni kuimarisha uwezo wa mwili wako kupambana na maradhi (strengthen your immune system). Uchunguzi uliofanyika Chuo Cha Wilkes huko jimbo la Pennsylvania, ulibaini kwamba kati ya wanafunzi waliojihusisha na vitendo vya kujamiiana mara moja au mbili kwa wiki, walikuwa na virutubisho zaidi vya kupambana na maradhi mwilini ukilinganisha na wale ambao walishiriki tendo hilo chini ya hapo. Pamoja na faida hiyo ya tendo la kujamiiana, wataalam walisisitiza kwamba ni muhimu kwa watu kuendelea kufanya vitu ambavyo pia ni muhimu kwa uimarishaji wa virutubisho vya kupambana na maradhi mwilini. Vitu hivyo ni kama ifuatavyo:
  • Kula vizuri
  • Kufanya mazoezi
  • Kupata usingizi wa kutosha
  • Kuhakikisha umepata chanjo zote muhimu kwa ajili ya maradhi ambukizi
  • Tumia kinga (condom) kama hamfahamu hali zenu (Katika hili, thehabari tunashauri kama wewe ni mume, basi tafuta mke wa kuoa, na kama wewe ni mke, basi tafuta mume. Baada ya hapo, tulia katika ndoa yako, michepuko sio dili!!!)
Pamoja na kwamba kufanya mazoezi imetajwa kama nyongeza ya tendo la kujamiina kama vitu ambavyo vinaongeza vurutubisho vya kupambana na maradhi mwilini, tendo la kujamiina peke yake linahesabika kama mazoezi. Ndio maana, faida kuu ya pili ni kukufanya ufungue gym kitandani. Kwa maneno mengine, kujamiiana ni njia moja wapo ya mazoezi. Hapa ni muhimu kukumbuka kwamba hata mazoezi yanahitaji mapumziko, kwahiyo usije ukafanya tendo hilo kutwa nzima (kama unao ubavu) na kutegemea faida, badala yake utachuma hasara, ambazo sio mjadala wetu leo. Kama tendo hili litafanyika kwa umakini na utaratibu maalum, basi wataalam wanasema tendo hilo linachoma kalori (calories) tano kwa dakika, kalori nne zaidi zinachomwa ukilinganisha na mtu anayeangalia TV!

Sababu kuu ya tatu, tendo la kujamiiana linapunguza uwezekano wa kuvamiwa na mshtuko wa moyo (heart attack!). Ukiachilia mbali kwamba tendo hili ni njia nzuri ya kuongeza mapigo yako ya moyo, pia ni njia nzuri ya kuhakikisha viwango vyako vya estrogen na testosterone vipo katika mizani sahihi kitu ambacho ni muhimu linapokuja suala la kuzuia uwezako wa kupatwa na mshtuko wa moyo, wataalam wanamalizia.
Hizi ni baadhi tu ya faida, bila shaka unazifaham faida nyingine lukuki, ambazo hazikutajwa hapa. Kama tulivyoonya hapo juu, kujamiiana ni tendo la kiungwana na lina faida nyingi kwa afya yako, hivyo basi, tafuta mke au mume, halafu dili nae! Michepuko sio diliii!

Read More

January 28, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 11:55 PM | Be the first to comment!

Mambo Nane Yatakayokuongezea Furaha

Fanya kawaida yako Kila siku ukiamka asubuhi Mshukuru Mungu kwa kukuwezesha kuamka salama na mwenye afya. Kitendo cha kushukuru kitakufanya ujione una jambo la kushukuru na kuwa wewe ni mwenye bahati. Kuna mambo mengi sana ya kushukuru, kama vile afya yako, nyumba unayolala, gari unaloendesha, chakula unachokula, mpenzi uliyenaye n.k. Fikiria mambo matano ya kushukuru kila siku asubuhi na utajiongezea furaha maishani mwako.

2) Amka mapema

Uchunguzi uliofanywa na chuo kikuu cha boston huko Marekani kinaonyesha kuwa watu wanaoamka mapema wanakuwa na furaha zaidi kuliko watu wanaochelewa sana kuamka. Kama unaweza ni vyema kuamka saa 11 au 12 asubuhi.



3) Panga ratiba ya siku nzima
Umeshawahi kurudi nyumbani jioni na kujiona kama siku yako imepotea bure na hamna cha maana ulichokifanya? wakati mwingine inawezekana kabisa kuwa umefanya kazi nyingi lakini kwasababu hukupanga ni nini utafanya siku hiyo unajiona kuwa hujafanya chochote. Ni vyema kuandika list ya vitu unavyopanga siku nzima, mwisho wa siku ukifika unaangalia list ya vitu ulivyovifanya na kuvimaliza, utajipongeza na kulala vizuri ukijua siku yako imekuwa ya mafanikio.
4)Fanya mazoezi
Kufanya mazoezi kunasaidia kujisikia vizuri, kuwa na afya njema, kulala vizuri, kupendezesha ngozi na kujiepusha na magonjwa mbali mbali hasa yale yanayosababishwa na unene.


5) Kula Breakfast
Kwa wale waliozoea kupiga desh asubuhi huu ndio muda muafaka kuacha hiyo tabia. Umeshasikia kuwa “breafast is the most important meal of the day”. Ukiacha tumbo bila chakula muda mrefu unajiweka kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Kumbuka wengi wetu huwa tunakula chakula cha jioni saa mbili usiku, ikifika saa mbili asubuhi tayari ni masaa 12 hujaweka kitu tumboni, ukipiga desh breakfast mpaka saa saba mchana hayo ni masaa 17 umekaa bila kuweka kitu tumboni. Faida nyingine ya kula breakfast ni kukupa nguvu na hujisikii umechoka choka ukifika kazini. Ukiona mtu ameingia kazini amenuna, muulize kama amekunywa chai na jibu lake litakuwa ni hapana.


6) Mfanyie mtu yeyote jambo jema
kumfanyia mtu jambo jema inakufurahisha wewe na pia inamfurahisha mtu ambaye umemfanyia jambo jema, Na sio lazima huyo mtu awe ni ndugu yako au mtu aunayemjua. Mambo ya kufanya kumfurahisha mtu ni mengi sana, nitakupa mfano wa mambo machache ambayo mimi mwenyewe huwa nafanya. Mambo hayo ni kama kumfungulia mtu mlango, Kumsaidia omba omba barabarani, kumnunulia rafiki yako lunch, kumrushia bibi yako hela ya sukari, kumpa mtu lift ya gari n.k Hakikisha kila siku unamfanyia mtu jambo jema na itakuongezea wewe furaha.
7) Sikiliza muziki wenye furaha (up beat music)

Utakuta mtu anaingia kwenye gari asubuhi anaweka wimbo wa majonzi jinsi anavyo-m-miss bebi wake au nyimbo nyingine tu za huzuri, mwisho wake utaishia kujisikia mwenye huzuni. Sikiliza nyimbo zilizo changamka na utajisikia umechangamka na mwenye furaha.

8) Mpigia simu mtu na umwambie unampenda

Kusema neno nakupenda ni ngumu kidogo kwenye jamii yetu. Lakini jitahidi kusema nakupenda mara kwa mara, ukiongea na mke wako , mtoto wako, bibi yako waambie unawapenda. Kuna miujiza katika neno nakupenda na ukilitumia vizuri utaiona hiyo miujiza.
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 11:15 PM | Be the first to comment!

Jifunze Njia sahihi ya kubajeti Mshahara wako

Elimu ya hela na matumizi yake ni muhimu kuliko elimu nyingine yoyote kwa watu wanaofanya kazi za kuajiriwa na hata kujiajiri, jambo la kusikitisha ni kwamba haifundishwi mashuleni na ni pasenti ndogo ya wazazi wanaofundisha watoto wao namna ya kutumia hela. Watu wanamaliza chuo kikuu, wanaanza kazi na bado wanaishia kukopa kwasababu ya kutokujua namna ya kubajeti matumizi.
 

Katika hii blog posti, utajifunza namna ya kupanga bajeti yako, namna ya kusavu hela na kusaidia ndugu zako. Watu wengi wanaishi maisha yasiyo na furaha kutokana na matumizi mabaya ya hela. Unakuta mtu anafanya kazi lakini anaishi mshahara kwa mshahara, huo ni utumwa.
Ukiangalia instagram utakuta watu wanafurahia mwisho wa mwezi ukifika, kisa? paycheck imeingia… Watu matajiri na waliofanikiwa kifedha,wanabajeti hela zao namna hii.
Asilimia 30% – inaenda kwenye kulipia kodi ya nyumba kwa walo wanaopangisha, au wanaojenga. Kama wewe tayari una nyumba, unaweza ukaweka asilimia 30 kwenye “investment” nyingine.
Asilimia 10 – inaenda kusaidia ngudu na wasiojiweza. Jinsi unavyotoa hela ndio jinsi zinavyoingia, hivi ndivyo dunia ilivyo.
Asimilia 10 inaenda kwenye savings account.
Asilimia 40 ndio ya matumizi yako ikiwemo chakula, usafiri, mavazi n.k.
Asilimia 10 inayobaki inaenda kwenye starehe “intertainment”.
Ukifuata hii formula, utajikuta muda wote una hela kwenye savings account kwa ajili ya emergency. Hamna haja ya kwenda kukopa, au kusubiri mwisho wa mwezi ili uende kutembea bagamoyo. Bagamoyo unaenda muda wowote kwani tayari umeshaweka fungu lake pembeni. Ukiishi kwa namna hii utakuwa na control na maisha yako na hutakuwa na matumizi makubwa kuliko kipato chako. Na kwasababu unaweka asilimia 10 kusaidia watu, utajikuta hela zinakurudia kwa namna ambavyo huwezi kuelezea.
Je wewe una unapangaje matumizi yako, acha komenti hapo chini.
Read More