Advertising

  • Matunda

    faida ya tunda la KITZ
  • Matunda

    kula matunda kwa wingi
  • GYm

    Mazoezi muhimu kwa afya
  • Mazoezi

    dada anaimarisha misuli
  • Jovago

    Promoo siku ya watendao

February 4, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 1:24 AM | Be the first to comment!

Mambo ya Kuzingatia Wakati Mnaanza Kuchumbiana

HAMNA raha ya pekee kama kuwa kwenye mahusiano ambayo mume na mke au ‘boyfriend’ na ‘girlfriend’ wanaelewana vizuri. Ni vigumu kupata mtu ambaye mnaelewana kila jambo.
Sio lazima kama mwenzako anasapoti Arsenal na wewe usapoti Arsenal. Wataalamu wa masuala ya mahusiano wanashauri kuwa, ili uweze kuishi vizuri na mtu kama mume na mke ni vizuri kuwa mnaelewana kwenye masuala ya msingi na mnashea visheni moja ya maisha. Kati ya masuala ya msingi ambayo ni muhimu kuwa kwenye ukurasa mmoja ni Matumizi ya fedha na kujamiiana. Haya ndio mambo makuu mawili ambayo yanasababisha ndoa nyingi sana kuvunjika. Utajuaje matumizi ya mtu ya fedha kama ndio wachumba na bado hamjaanza kuishi pamoja? Ni rahisi, utakuwa unajua mwenzako anafanya kazi wapi, dadisi kwa watu kuwa kazi kama anayofanya mwenzako ina mshahara kiasi gani pamoja na dili nyingine anazofanya, ukishajua hilo anza kuchunguza matumizi yake, vitu anavyonunua, mavazi anayovaa, gari analoendesha na mambo mengine kama hayo. Kama matumizi yake yako juu kuliko kipato chake, jaribu kuongea naye na kumshauri kuhusu matumizi yake.
Tunakuja kwenye swala ya kujamiiana, hili ndio jambo la pili ambalo linaongoza kwa kusababisha mahusiano kuvunjika hasa kwa kizazi kipya. Miaka kama 30 iliyopita, watu wengi walikuwa wanaoana wakiwa bado bikra. Jambo zuri la kuoana mkiwa bado bikra ni kwamba wote mnaingia mkiwa hamna ujuzi na hamna wasichana au wanaume wengine ambao umelala nao wa kulinganishe ujuzi wao na mke wako au mume wako. Tatizo lipo siku hizi ambapo watu wanaoana wakiwa na ujuzi tofauti (diffetent experience level) ndio maana michepuko imezidi.
Wanadamu tumezoea kulingalisha vitu, pale utakapoanza tu kulinganisha utaalamu wa mwenzako na wanawake au wanaume wako wa zamani ndio utakapoanza kumuona mwenzako hafai. Jitahidi kutolinganisha uhusiano wako na watu waliopita, hamna watu wawili wanafanana kila kitu humu duniani. Kabla sijamalizia, napenda kusisitizia kuhusu umuhimu wa mawasiliano, sio kupigiana simu na kuandikiana message kwenye whatsapp, kutaneni mahali, wekeni simu zenu mbali na sio unaangalia picha instagram wakati unaongea na mwenzako.
Tafuteni sehemu iliyotulia mara mbili kwa wiki mzungumze na kupanga maisha yenu, usiogope wala kuona haya kuuliza swali lolote.
Read More

February 2, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 10:07 AM | Be the first to comment!

Zijue Tabia 7 za Wanawake wanao-Cheat

Kama mke wako, demu wako au side chick wako ana tabia zifuatazo, amesha-cheat kwako au ipo siku ataku-cheat.



1) Ana boreka haraka – Wanawake wanaoboreka haraka nirahisi kutafuta mwanaume mwingine wa kum-entertain, muda sio mrefu huyo mwanaume atachoka kum-entatain rafiki asiye na faida na ndio hapo atakapo anza kudai faida zake na wanaishia kuwa friends with benefits.
2) Marafiki wengi wa kiume – Mwanamke mwenye marafiki wengi wa kiume ni rahisi ku-cheat kwasababu anapata muda mwingi wa kuongea na wanaume wengine, watamsifia anavyopendeza, kama wewe unamwambia amependeza mara moja kwa wiki basi wenzako watamwambia anapendeza kila wanapoonana. Wataabza kumtoa out na mwisho wake ataona hao wanaume wamanjali kuliko wewe na kulala nao.
3) Anapenda attention – Wanawake wanaopenda attention ni rahisi kudanganyika. Wanaume wengi hasa ambao hawataki kuwa committed kwenye mahusiano yoyote wanatoa sana attention kwa wanawake. Mwanamke anayependa sana attention hawezi ridhishwa na attention ya mwanaume mmoja.
4) Anapenda vitu “material things” Wanawake wengi wanaopenda material things wanashindwa kupata kila kitu kutoka kwa waume zao au maboyfriend zao na kuishia kutafuta mwanaume mwingine ambaye ana uwezo wa kumnunulia vitu anavyotaka ili awatese wenzake kwenye instagram
5) Ana marafiki ambao ni michepuko – Umeshasikia usemi kuwa ndege wanaofanana huruka pamoja, hata kama demu wako hana tabia ya ku-cheat, akiwa anakaa sana na marafiki ambao wana-cheat na yeye atashawishika kujaribu. Kama mke wako au demu wako ana kupigia story za marafiki zake wanao-cheat mwambie aachane nao haraka sana.
6) Anapenda kufanya ngono kuliko wewe – kila mkimaliza kufanya tendo la ndoa mwenzako anakwambia anataka tena, na wewe humtimizii basi lazima tatafuta serengeti boy ambaye anamsikiliza na kumpa anachotaka.
7) Anaujuzi kitandani kuliko wewe – Wewe kama umeshawahi kuingia kwenye dancing floor na kucheza na mtu ambaye anajua kucheza kuliko wewe, unasubiria tu wimbo ukiisha ukakae chini kabla hujaaibishwa, au kama wewe ndio unayejua kucheza vizuri utatafuta mtu mwingine anayejua kucheza kama wewe. Kwenye tendo la ndoa ni hivyo hivyo kama mwenzako ana ujuzi kuliko wewe, inabidi ufanye mazoezi ufikie kwenye ujuzi wake la sivo muda sio mrefu atasubiri wimbo ukiisha akakae chini au atafute mtu mwingine anayejua kucheza kama yeye.
Demu wako au mchepuko wako una tabia moja wapo kati ya nilizozitaja hapo juu? Usisite kuacha comments hapo chini.

Read More

January 29, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 1:10 AM | Be the first to comment!

Shitka!!Tabia Kuu Tano Za Watu Waliofanikiwa Kimaisha!

Kwanza, kabla sijaendelea embu tuwekane sawa kuhus hii falsafa ya “kufanikiwa kimaisha”, ina maana gani haswa? Ukweli ni kwamba watu wengi wakisikia fulani amefanikiwa kimaisha, basi moja kwa moja wanafikiri au wanaamini mtu huyo atakuwa na pesa nyingiiii au kwa maneno mengine, mtu huyo ni tajiri fulani hivi. Pamoja na kwamba pesa ndio mtatuzi wa mahitaji mengi hapa duniani, lazima tukumbuke kwamba pesa ina uwezo wa kununulia kitanda cha gharama kubwa sana, lakini ukashindwa kulala katika kitanda hicho kwa msongo wa mawazo. Pia pesa inaweza ikakufanya uopoe mwenza mzuri kuliko wote duniani, lakini mwenza huyo asiwe na mapenzi ya dhati kwako.
Hapa tunajifunza kwamba ingawa pesa ni muhimu sana maishani, kufanikiwa au kutofanikiwa kwa mtu kimaisha hakuwezi kupimwa kwa kiasi tu cha pesa alichonacho. Mtu anaweza akawa na pesa, lakini akakosa raha kutokana na ukosefu wa amani ya ndani na nje ya mwili. Hivyo basi, Kufanikiwa au kutofanikiwa maishani kwa mtu, ni lazima pia kupimwe kwa mambo mengine muhimu kama uchamungu, ukarimu, maadili, busara, uvumilivu, na ujasiri (wa kufanya na kuishi na maamuzi magumu). Hivi “viambatanisho” 6 vya pesa ndio vinarutubisha na kudumisha pesa, na zaidi humfanya mtu afurahie (enjoy) pesa hizo. Kwa uzoefu wangu, mchanganyiko wa mambo haya yote muhimu, ndio humfanya mtu “afanikiwe kimaisha” kwa maana pana ya falsafa hiyo. Baada ya muhtahsari huu, tuendelee sasa na mada yetu, ambayo leo inagusia mambo makuu matano ya watu waliofanikiwa kama ifutavyo:
#1: Huishi Kwa Siku Za Baadae (Future), Na Sio Siku Zilizopita (Past). Bila shaka umeshasikia ule usemi wa siku nyingi kwamba “yaliyopita si ndwele, tugange yajayo”. Watu waliofanikiwa kimaisha huwa na tabia ya kutokatishwa tamaa na mambo ambayo yameshapita, na hayakwenda kama walivyotarajia, kwani siku zote huwa wanakubali matokeo ya kutofanikiwa kwao katika suala fulani na kujipanga upya kulikabili suala hilo. Siku zote hujizuia kuruhusu matukio ya kushindwa kwao kufanikiwa katika masuala fulani maishani, kushusha imani yao yakufanikiwa katika masuala ya baadae (future)

#2: Hawalii Shida Na Wala Hawana Kinyongo Hisia zako za siku kwa kiasi kikubwa zinategemea na wapi ulipoelekeza mawazo yako. Kwa mujibu wa mtaalam wa Saikolojia, Travis Bradberry, anaweka wazi kwamba “kama umeelekeza mawazo yako kwenye shida ambazo zinakukabili, basi unajijengea hisia hasi mwilini na kujiongezea mastresi kibao, ambayo yana athiri na kuzuia uwezo wako wa kufanya mambo ya kimaendeleo”. Hivyo basi, watu waliofanikiwa maishani huwa wanaelekeza mawazo yao kwenye masuala chanya, ili kupiga vita mastresi na kujiongezea uwezo wa kukomaa na mambo ya maendeleo. Pia, watu waliofanikiwa maishani huwa hawaendekezi kinyongo, kwani wanaelewa kuwa kuweka kinyongo katika masuala yaliyopita ni hatari sana kwa maendeleo. Vinyongo kama ilivyo kubebea shida mbeleko, ni vitu ambavyo huzalisha hisia hasi mwilini na kumfanya mtu kuwa na mastresi (au msongo wa mawazo), ambayo yana mzuia kufanya mambo ya maendeleo
#3: Hawatoi Kipaumbele Katika Ukamilifu. Hapa ina maanisha kwamba, watu waliofanikiwa maishani huwa hawapotezi muda katika kutafuta ukamilifu (perfection) katika mambo yao. Ni watu, ambao wanafaham kwamba binaadam ni viumbe dhaifu na ukamilifu ni wa Mungu peke yake. Hivyo basi, hii sifa inawasaidia sana linapokuja suala la kuridhika na kile walichoweza kufanya baada ya kujitahidi kwa uwezo wao. Hii inawafanya waendelee kujiamini, badala ya kujilaumu na kujihisi wamefeli kama wale watu wanaolenga ukamilifu katika ufanyaji wa mambo yao.


#4: Hawapotezi Muda Wao Na Watu Wenye Mawazo Hasi. Hii sifa ni muhimu sana na kwa ufupi ni muendelezo wa sifa #2, kwani ili mtu aendelee kubaki na mawazo chanya kwa mustakbali mzima wa maendeleo yake, ni lazima apinge kukaa na watu wenye mawazo hasi au walalamikaji. Kwa ung’eng’e wanasema “ don’t hangout with negative people!” Hapa wanazungumziwa marafiki, ndugu, na jamaa, yaani kuwa makini sana kuhusu watu unaokaa na kuzungumza nao kwa siku. Kama watu hawa wamejaa malalamiko tu kuhusu maisha yao siku nzima, basi jua wanagonjwa hatari sana na ni watu wa kukaa nao mbali, ili wasikuambukize gonjwa hilo hatari kwa maendeleo yako. Siku zote watu waliofanikiwa maishani (au wale walio mbioni kufanikiwa) huwa wanajihusisha na watu wenye mawazo chanya na matumaini tele kuhusu mustakbali wa maisha yao.
#5: Hawaoni Hatari Kusema “Hapana!” Hii pia ni sifa muhimu sana, kwani watu wengi wanaostrago maishani, ni watu ambao wanataka kumridhisha kila mtu, kitu ambacho ni kigumu sana. Mbali na kwamba sifa moja wapo ya mtu aliyefanikiwa maishani ni ukarimu, watu hawa pia wana ujasiri wa kusema hapana katika mambo ambayo hawataki au hawana muda wa kufanya. Ni watu ambao hawazunguki mbuyu linapokuja suala la kumwambia mtu kwamba ombi lao kwao limekataliwa. Hapa sio tu kwa wale watu wanaopenda kupiga mizinga ya pesa (ambayo mengine haina msingi wowote), bali pia kusema hapana linapokuja suala la kuombwa msaada wa kikazi na washirika wa biashara au ajira. Watu waliofanikiwa maishani hawaoni hatari kukataa kutoa msaada wa kikazi kwa watu wengine, ili kujipa muda zaidi na uwezo wa kufanya kazi zao.
Anza kufanya uchunguzi wako leo kwa watu unaowafaham, ambao “wamefanikiwa maishani” na utaona mifano hai ya sifa hizi au kama tayari unawafaham watu hao, basi tupe maoni yako kwa faida ya wasomaji wote!


Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 1:01 AM | Be the first to comment!

Karibu na Zijue Faida Tatu za Tendo la Ndoa!


                                            

Watu wanaoshiriki tendo la ndoa mara kwa mara, huwa hawa umwi umwi hovyo”, anasema Dkt.Yvonne K. Fullbright, mtaalam wa afya ya tendo la kujamiina. Baada ya nukuu hii kutoka kwa mtaalam, sio ajabu basi tukisikia kwamba faida kuu ya kwanza ni kuimarisha uwezo wa mwili wako kupambana na maradhi (strengthen your immune system). Uchunguzi uliofanyika Chuo Cha Wilkes huko jimbo la Pennsylvania, ulibaini kwamba kati ya wanafunzi waliojihusisha na vitendo vya kujamiiana mara moja au mbili kwa wiki, walikuwa na virutubisho zaidi vya kupambana na maradhi mwilini ukilinganisha na wale ambao walishiriki tendo hilo chini ya hapo. Pamoja na faida hiyo ya tendo la kujamiiana, wataalam walisisitiza kwamba ni muhimu kwa watu kuendelea kufanya vitu ambavyo pia ni muhimu kwa uimarishaji wa virutubisho vya kupambana na maradhi mwilini. Vitu hivyo ni kama ifuatavyo:
  • Kula vizuri
  • Kufanya mazoezi
  • Kupata usingizi wa kutosha
  • Kuhakikisha umepata chanjo zote muhimu kwa ajili ya maradhi ambukizi
  • Tumia kinga (condom) kama hamfahamu hali zenu (Katika hili, thehabari tunashauri kama wewe ni mume, basi tafuta mke wa kuoa, na kama wewe ni mke, basi tafuta mume. Baada ya hapo, tulia katika ndoa yako, michepuko sio dili!!!)
Pamoja na kwamba kufanya mazoezi imetajwa kama nyongeza ya tendo la kujamiina kama vitu ambavyo vinaongeza vurutubisho vya kupambana na maradhi mwilini, tendo la kujamiina peke yake linahesabika kama mazoezi. Ndio maana, faida kuu ya pili ni kukufanya ufungue gym kitandani. Kwa maneno mengine, kujamiiana ni njia moja wapo ya mazoezi. Hapa ni muhimu kukumbuka kwamba hata mazoezi yanahitaji mapumziko, kwahiyo usije ukafanya tendo hilo kutwa nzima (kama unao ubavu) na kutegemea faida, badala yake utachuma hasara, ambazo sio mjadala wetu leo. Kama tendo hili litafanyika kwa umakini na utaratibu maalum, basi wataalam wanasema tendo hilo linachoma kalori (calories) tano kwa dakika, kalori nne zaidi zinachomwa ukilinganisha na mtu anayeangalia TV!

Sababu kuu ya tatu, tendo la kujamiiana linapunguza uwezekano wa kuvamiwa na mshtuko wa moyo (heart attack!). Ukiachilia mbali kwamba tendo hili ni njia nzuri ya kuongeza mapigo yako ya moyo, pia ni njia nzuri ya kuhakikisha viwango vyako vya estrogen na testosterone vipo katika mizani sahihi kitu ambacho ni muhimu linapokuja suala la kuzuia uwezako wa kupatwa na mshtuko wa moyo, wataalam wanamalizia.
Hizi ni baadhi tu ya faida, bila shaka unazifaham faida nyingine lukuki, ambazo hazikutajwa hapa. Kama tulivyoonya hapo juu, kujamiiana ni tendo la kiungwana na lina faida nyingi kwa afya yako, hivyo basi, tafuta mke au mume, halafu dili nae! Michepuko sio diliii!

Read More

January 28, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 11:55 PM | Be the first to comment!

Mambo Nane Yatakayokuongezea Furaha

Fanya kawaida yako Kila siku ukiamka asubuhi Mshukuru Mungu kwa kukuwezesha kuamka salama na mwenye afya. Kitendo cha kushukuru kitakufanya ujione una jambo la kushukuru na kuwa wewe ni mwenye bahati. Kuna mambo mengi sana ya kushukuru, kama vile afya yako, nyumba unayolala, gari unaloendesha, chakula unachokula, mpenzi uliyenaye n.k. Fikiria mambo matano ya kushukuru kila siku asubuhi na utajiongezea furaha maishani mwako.

2) Amka mapema

Uchunguzi uliofanywa na chuo kikuu cha boston huko Marekani kinaonyesha kuwa watu wanaoamka mapema wanakuwa na furaha zaidi kuliko watu wanaochelewa sana kuamka. Kama unaweza ni vyema kuamka saa 11 au 12 asubuhi.



3) Panga ratiba ya siku nzima
Umeshawahi kurudi nyumbani jioni na kujiona kama siku yako imepotea bure na hamna cha maana ulichokifanya? wakati mwingine inawezekana kabisa kuwa umefanya kazi nyingi lakini kwasababu hukupanga ni nini utafanya siku hiyo unajiona kuwa hujafanya chochote. Ni vyema kuandika list ya vitu unavyopanga siku nzima, mwisho wa siku ukifika unaangalia list ya vitu ulivyovifanya na kuvimaliza, utajipongeza na kulala vizuri ukijua siku yako imekuwa ya mafanikio.
4)Fanya mazoezi
Kufanya mazoezi kunasaidia kujisikia vizuri, kuwa na afya njema, kulala vizuri, kupendezesha ngozi na kujiepusha na magonjwa mbali mbali hasa yale yanayosababishwa na unene.


5) Kula Breakfast
Kwa wale waliozoea kupiga desh asubuhi huu ndio muda muafaka kuacha hiyo tabia. Umeshasikia kuwa “breafast is the most important meal of the day”. Ukiacha tumbo bila chakula muda mrefu unajiweka kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Kumbuka wengi wetu huwa tunakula chakula cha jioni saa mbili usiku, ikifika saa mbili asubuhi tayari ni masaa 12 hujaweka kitu tumboni, ukipiga desh breakfast mpaka saa saba mchana hayo ni masaa 17 umekaa bila kuweka kitu tumboni. Faida nyingine ya kula breakfast ni kukupa nguvu na hujisikii umechoka choka ukifika kazini. Ukiona mtu ameingia kazini amenuna, muulize kama amekunywa chai na jibu lake litakuwa ni hapana.


6) Mfanyie mtu yeyote jambo jema
kumfanyia mtu jambo jema inakufurahisha wewe na pia inamfurahisha mtu ambaye umemfanyia jambo jema, Na sio lazima huyo mtu awe ni ndugu yako au mtu aunayemjua. Mambo ya kufanya kumfurahisha mtu ni mengi sana, nitakupa mfano wa mambo machache ambayo mimi mwenyewe huwa nafanya. Mambo hayo ni kama kumfungulia mtu mlango, Kumsaidia omba omba barabarani, kumnunulia rafiki yako lunch, kumrushia bibi yako hela ya sukari, kumpa mtu lift ya gari n.k Hakikisha kila siku unamfanyia mtu jambo jema na itakuongezea wewe furaha.
7) Sikiliza muziki wenye furaha (up beat music)

Utakuta mtu anaingia kwenye gari asubuhi anaweka wimbo wa majonzi jinsi anavyo-m-miss bebi wake au nyimbo nyingine tu za huzuri, mwisho wake utaishia kujisikia mwenye huzuni. Sikiliza nyimbo zilizo changamka na utajisikia umechangamka na mwenye furaha.

8) Mpigia simu mtu na umwambie unampenda

Kusema neno nakupenda ni ngumu kidogo kwenye jamii yetu. Lakini jitahidi kusema nakupenda mara kwa mara, ukiongea na mke wako , mtoto wako, bibi yako waambie unawapenda. Kuna miujiza katika neno nakupenda na ukilitumia vizuri utaiona hiyo miujiza.
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 11:15 PM | Be the first to comment!

Jifunze Njia sahihi ya kubajeti Mshahara wako

Elimu ya hela na matumizi yake ni muhimu kuliko elimu nyingine yoyote kwa watu wanaofanya kazi za kuajiriwa na hata kujiajiri, jambo la kusikitisha ni kwamba haifundishwi mashuleni na ni pasenti ndogo ya wazazi wanaofundisha watoto wao namna ya kutumia hela. Watu wanamaliza chuo kikuu, wanaanza kazi na bado wanaishia kukopa kwasababu ya kutokujua namna ya kubajeti matumizi.
 

Katika hii blog posti, utajifunza namna ya kupanga bajeti yako, namna ya kusavu hela na kusaidia ndugu zako. Watu wengi wanaishi maisha yasiyo na furaha kutokana na matumizi mabaya ya hela. Unakuta mtu anafanya kazi lakini anaishi mshahara kwa mshahara, huo ni utumwa.
Ukiangalia instagram utakuta watu wanafurahia mwisho wa mwezi ukifika, kisa? paycheck imeingia… Watu matajiri na waliofanikiwa kifedha,wanabajeti hela zao namna hii.
Asilimia 30% – inaenda kwenye kulipia kodi ya nyumba kwa walo wanaopangisha, au wanaojenga. Kama wewe tayari una nyumba, unaweza ukaweka asilimia 30 kwenye “investment” nyingine.
Asilimia 10 – inaenda kusaidia ngudu na wasiojiweza. Jinsi unavyotoa hela ndio jinsi zinavyoingia, hivi ndivyo dunia ilivyo.
Asimilia 10 inaenda kwenye savings account.
Asilimia 40 ndio ya matumizi yako ikiwemo chakula, usafiri, mavazi n.k.
Asilimia 10 inayobaki inaenda kwenye starehe “intertainment”.
Ukifuata hii formula, utajikuta muda wote una hela kwenye savings account kwa ajili ya emergency. Hamna haja ya kwenda kukopa, au kusubiri mwisho wa mwezi ili uende kutembea bagamoyo. Bagamoyo unaenda muda wowote kwani tayari umeshaweka fungu lake pembeni. Ukiishi kwa namna hii utakuwa na control na maisha yako na hutakuwa na matumizi makubwa kuliko kipato chako. Na kwasababu unaweka asilimia 10 kusaidia watu, utajikuta hela zinakurudia kwa namna ambavyo huwezi kuelezea.
Je wewe una unapangaje matumizi yako, acha komenti hapo chini.
Read More

January 26, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 11:48 PM | Be the first to comment!

Hii ni historia au uhalisia Jaman Ebu na wewe Usome kwani dini zote zinamlengo wa kumnyenyekea mwomba wetu

Japo Uislamu pia umegawanyika katika makundi mawili ya Sunni na Shia, lakini mgawanyiko huu ni wa kisiasa, sio wa kidini. Katika Ukristo mgawanyiko ni wa kidini. Japo wote wanamuamini Mungu, lakini tusimsahau Yesu - - - mambo yanakhitilafiana kuanzia hapa.
Ingawa idadi kamili haieleweki, ninafahamu takribani madhehebu hamsini ndani ya Ukristo, tukianzia na wa - Amish, ambao wameamua kujitenga na ulimwengu na mambo yote yanayorahisisha maisha (ya kisasa) kama vile umeme na magari, na kumalizia na Unitarians ambao wanaonekana mbele ya wakristo walio wengi kuwa sio wakristo kwa sababu hawaamini kuwa Yesu ni mwana wa Mungu wala hawaamini utatu Mtakatifu.
Waromani Katoliki, ambao ni dhehebu la kikristo kubwa kuliko yote ulimwenguni leo, wanawatukuza watakatifu (saints) na mama wa Yesu. Mliwaji (yaani mkate) wakati wa kumunio inasemekana kwamba huwa ni mwili halisi wa Yesu, divai huwa ni damu halisi inapobarikiwa na padri.
Kwa sababu ya kutoridhishwa kwao na imani ya kutooa au kutoolewa (celibacy), kanisa la Orthodox lilijitenga kutoka Roma katika zama za kati (middle ages) na sasa hivi kanisa hili lina wafuasi wengi katika Ulaya ya Mashariki. Wanaendelea na mapambo katika makanisa yao kama yale ya kanisa katoliki lakini wana sikukuu tofauti na wanaapa kiapo cha utii kwa "Baba Mtakatifu" mwingine asiye kuwa Yule wa Roman Katoliki.
Mnamo mwaka 1517, kanisa la kiprotestanti lilianzishwa, kwa sababu ya kutokubaliana na baadhi ya mambo (vitendo) ndani ya kanisa katoliki. Baadhi ya mambo hayo ni:
1) Wakatoliki wanapamba na kuyanakshi makanisa yao. Waprotestanti wanayafanya kuwa rahisi.
2) Maandiko Matakatifu ya Wakatoliki yanajumuisha vitabu vya "Apocrypha" (vitabu vilivyofichikana ). Waprotestanti hawakubali kitabu chochote katika vitabu hivi.
3) Wakatoliki wana vinyago katika makanisa yao, majumba yao, katika magari yao. Pia wanavichimbia vinyago hivi mbele ya bustani za nyumba wanazotaka kuziuza, na wa misalaba iliyopambwa kwa umbo la Yesu akiwa amesulubiwa. Waprotestanti wanashutumu jambo hili kuwa ni "ibada ya masanamu" kwa hiyo wengi hawana hata msalaba mtupu (usiokuwa na sanamu ya Yesu) ndani ya makanisa yao.
Ndani ya tawi hili la Ukristo la Kiprotestanti kuna madhehebu mengine lukuki (mengi sana).
Walutherani wanafuata mafundisho ya Martin Luther. Baadhi ya Wakristo kutoka katika makanisa yaliyofanya Mageuzi (Reformed Churches). Hata hivyo waliona kuwa Martin Luther hakuwa mwangalifu na makini vya kutosha, hivyo waliamua kufuata mafundisho ya John Calvin.
Wa-Baptisti, ambao wanaamini kuwa watu wazima - - sio watoto - - ndio wanaotakiwa kubatizwa, waliuawa kikatili na wakatoliki na Waprotestanti katika Zama za Kati (Middle Ages) lakini sasa hivi wamekuwa miongoni mwa madhehebu makubwa ya Ukristo.
Kamwe Wakatoliki hawakuwa wa pole kuhusiana na harakati za Waprotestanti, na lilikuwa ni hitajio la uhuru wa kidini lililowahamisha Wazungu kutoka miji yao na kwenda katika nchi za ugenini. Wa-puritan walipohamia Amerika, katika karne ya kumi na saba, kundi la zima la madhehebu ya kikristo lilianza kuwepo katika miaka michache iliyofuatia.
Wa-shaker walikuwa na imani kali juu ya imani ya kutokuoa (ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu). Dhehebu hili leo limeshakufa (kutokana na ubovu wa imani na misingi yake).
Wapentekoste wanadai "kuzungumza kwa ndimi" (kuzungumza kwa Roho mtakatifu). Huduma zao za kanisa inasemekana zinafurahisha sana. Pia wanaamini kuwa Biblia ndani yake haina makosa hata kidogo - - - yaani haina kasoro au dosari japo ile ndogo kabisa. Kutokana na nyadhifa zao tumekuja kuwajua watu "maarufu" kama akina Jimmy Swaggert, Jim na Tammy Fay Bakker.
Mashahidi wa Yehova wanatumia muda wao mwingi kutafakari kitabu cha Ufunuo, wakiiota siku ambayo kila na mtu na kila kitu kitakhiliki (kitaangamia) isipokuwa wao.
Wa-Mormon walikuwa na mtume wao, Joseph Smith, ambaye aliwaletea kitabu cha maandiko ambacho wanaamini kuwa ni kitakatifu kama Biblia. Sera yao ya "ndoa za mbinguni" (yaani wake wengi bila mpaka) ilipelekea mwisho wa kuendelea kufanywa kuwa taifa (state) katika nchi hii.
Wanasayansi wa kikristo pia wana kitabu chao cha Maandiko mbali na Biblia; Mary Baker Eddy, mtume wao (wa kike) aliwaambia wafuasi wake kuwa imani na sayansi hushinda vyote - - - hata matamanio ya ngono (sexual desires).
Madhehebu mengi tofauti tofauti yakiwa na vitendo vingi tofauti tofauti, yote yameungana na kukubaliana kwamba imani yao ya Ukristo ndiyo "imani pekee ya kweli". Kiapo hiki cha kishahidi kwenye dini imekuwa ndio sababu ya matukio mengi ya ukatili na utumiaji wa nguvu usioelezeka dhidi ya wale wenye imani tofauti na hii. Matukio haya ni kama vile vita vitakatifu dhidi ya Uislamu (crusades). Upelelezi na hata Maangamizi ya moto ya Nazi (Nazi Holocaust). Kutovumiliana ni kitu chenye kutisha sana na hasa kunapotokana na ushabiki.
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 11:42 PM | Be the first to comment!

Fahamu Masuala Kumi huenda Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislam

  •  mwanaume anaweza kuoa hadi wake wanne, mwanamke anaweza kuolewa na        mwanaume mmoja tu.
  •  sehemu ya urithi wa mwanamme ni kubwa kuliko ya mwanamke.
  •  mwanamme anaweza kuoa mwanamke asiye Muislamu, mwanamke hawezi
  • mwanamke ni lazima avae hijaab.

 JIBU
Suala hili pana halielekei kufuatana kwa mnasaba wa hoja zinazotolewa. Tathmini ya mwanzo na muhimu zaidi ya kuifanya ni kuhusu suala maarufu “Je wanaume ni sawa na wanawake?” Ni suala ambalo limetengenezwa vibaya, lisiloweza kujibika. Tatizo ambalo watu wengi wanatumia kuliepuka ni kutolitafsiri neno “usawa”. Hii ni nukta inayohitaji kuupambanua usawa ambao ni lazima uelezwe kwa hali inayopimika. Kwa mfano, wanawake kwa kiwango fulani wapo juu kuliko wanaume kama tutauliza nani ni mfupi kwa (kupambanisha na) urefu kuliko mwengine (“Ukuaji na Maendeleo” Encyclopaedia Britannica, 1992). Wanawake pia wapo juu kwa kiwango fulanikama tutauliza watoto wana mapenzi zaidi na nani, mama au baba? Wanawake pia wapo juu kwa kiwango fulanikama tutauliza nani ana tabia ya kujiweka kwenye jamii zaidi. Kwa upande mwengine, wanaume wapo juu kwa kiwango fulani kama tutauliza nani ni mrefu kwa (kupambanisha na) ufupi kuliko mwengine. Na mambo mengineyo: kila suala linaweza kugeuzwa upande mwengine, na muhimu zaidi ni kuwa hali hizi hazina mnasaba.
Je, kinachofuata, ni hali gani muhimu ambayo tuna wasiwasi nayo kuhusiana na usawa wa jinsia? Kiasili, kutokana na uoni wa Qur-aan na Sunnah, hali iliyokuwa muhimu zaidi ni nani aliyekuwa mtiifu kwa Allaah, wanaume au wanawake? Suala hili bila ya shaka linajibiwa ndani ya Qur-aan (iliyotafsiriwa):
{{Na watakaofanya vitendo vizuri, wakiwa wanaume au wanawake, hali wao ni wenye kuamini, basi hao wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa hata tundu ya kokwa ya tende.}} [4:124]
{{Bila shaka wanaume wenye kufuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanawake wenye kufuata vizuri nguzo za Uislamu; na wanaume wanaoamini vizuri nguzo za Imani, na wanawake wanaoamini vizuri nguzo za Imani; na wanaume wasemao kweli, na wanawake wasemao kweli; na wanaume wanaosubiri, na wanawake wanaosubiri; na wanaume wanaonyenyekea na wanawake wanaonyenyekea; na wanaume wanaotoa (Zakaat na) sadaka, na wanawake wanaotoa (Zakaat na) sadaka, na wanaume wanaofunga, na wanawake wanaofunga; na wanaume wanaojihifadhi tupu zao, na wanawake wanaojihifadhi; na wanaume wanaomtaja Mwenyezi Mungu (kwa wingi), na wanawake wanaomtaja Mwenyezi Mungu (kwa wingi) Mwenyezi Mungu Amewaandalia msamaha na ujira mkubwa.}} [33:35]
Qur-aan na Sunnah zinarudia tena na tena kwamba Allaah Anampendelea mtu mmoja dhidi ya mtu mwengine kwa kigezo chake cha hamasa, unyenyekevu, khofu, mapenzi, na matarajio ya Allaah (neno la kiarabu la ‘Taqwa’ ‘ucha Mungu’ ni gumu kulipatia tafsiri yake halisi). Sifa nyengine zote zimetenguliwa: jinsia, kabila, taifa, asili, n.k.
Kwa vile Allaah Hapendelei jinsia moja dhidi ya nyengine ndani ya matakwa Yake kwetu sisi (na inasaidia kukumbuka kwamba Allaah sio mwanamume wala mwanamke), na sasa tunaweza kuelezea tofauti baina ya jinsia ndani ya Uislamu.
Kwanza, wanaume na wanawake hawapo sawa kama tunavyoelewa. Muumba Anaelezea ndani ya Qur-aan (iliyotafsiriwa):
{{…na mwanamume si sawa na mwanamke…}} [3:36]
Wanaume na wanawake ni tofauti kwenye tabia, na kwenye majukumu yao ndani ya Uislamu. Hata hivyo, wote wana ulazima wa uwajibikaji kwa mwenziwe, hususan nukta hii muhimu inayofuata ambayo ni lazima ieleweke ndani ya mjadala wowote kuhusu wanaume na wanawake.
{{Na waozeni wajane miongoni mwenu (waungwana), na walio wema katika watumwa wenu (wanaume) na wajakazi wenu, kama watakuwa mafakiri Mwenyezi Mungu Atawatajirisha katika fadhila Zake; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua}} [24:32]
Ndani ya Aayah hii, Muumba Anatilia mkazo kwamba ndoa ni lazima ifungwe mapema na Waislamu: tabia ya kuwa pweke isikuwepo. Kwa kuwepo hili akilini, tunaweza kuanza kuelewa hoja nne zilizotajwa hapo juu kwa hitimisho lisilo na kosa lolote.
Wanaume na wanawake ni tofauti kwenye kuwajibika kwao kwa familia ambazo wanahimizwa sanakuzisimamisha. Wanawake hawawajibiki kufanya kazi, wakati wanaume wanalazimika. Mwanamume ni lazima atoe mahitaji kwa familia, lakini mwanamke hana haja ya kutumia pesa yake kwa ajili hiyo, ingawa anapata malipo kwa kufanya hivyo. Allaah Anasema ndani ya Qur-aan (iliyotafsiriwa):
{{Wanaume (wawe) ni walinzi wa wanawake; kwa sababu Mwenyezi Mungu Amewafadhilisha baadhi yao kuliko wengine, na kwa sababu ya mali zao wanazozitoa. Basi wanawake wema ni wale wenye kutii, wanaojihifadhi (hata) wasipokuwapo (waume zao); kwa kuwa Mwenyezi Mungu Amewaamrisha wajihifadhi. Na wanawake ambao mnaona uasi wao kwenu waonyeni na waacheni peke yao katika vitanda na wapigeni. Na kama wanakutiini msiwatafutie njia (ya kuwaudhi bure). Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Aliye juu (na) Mkuu.}} [4:34]

Kutokana na Sunnah, hususan ndani ya somo la Sunnah linaloitwa Swahiyh al-Bukhaariy, tunaona:
Amesimulia ‘Amr bin Al-Haarih: Zaynab, mke wa ‘Abdullaah alisema: “Nilikuwa Msikitini nikamuona Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ‘Enyi wanawake! Toeni sadaka hata kama kutoka kwenye mapambo yenu’ Zaynab alikuwa akimpatia ‘Abdullaah na mayatima walio chini ya hifadhi yake. Hivyo alimwambia ‘Abdullaah, “Je unaweza kumuuliza Mtume wa Allaah iwapo naweza kutumia sehemu ya Zakaat kwako na mayatima walio chini ya hifadhi yangu?” Alijibu “Je, utamuuliza mwenyewe Mtume wa Allaah?” (Zaynab akaongeza): Hivyo nilienda kwa Mtume na hapo nikamuona mwanamke wa ki-Aanswari aliyekuwa amesimama mlangoni (kwa Mtume) aliyekuwa na tatizo lililo sawa na langu. Bilaal alipita mbele yetu na tukamuomba, “Muulize Mtume wa Allaah iwapo naweza kutumia sehemu ya Zakaat kwa mume wangu na mayatima walio chini ya hifadhi yangu” Na tukamuomba Bilaal kutomtaarifu Mtume kuhusu sisi. Hivyo Bilaal aliingia ndani na kumuuliza Mtume kuhusiana na tatizo letu. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliuliza, “Hao wawili ni kina nani?”Bilaal alijibu kwamba alikuwa ni Zaynab. Mtume alisema, “Zaynab gani?” Bilaal alisema, “Mke wa ‘Abdullaah (bin Mas’uud)”. Mtume akasema, “Ndio, (inawezekana kwake), na atapata malipo mara mbili yake (kwa tendo hilo): Kwanza kwa kusaidia jamaa zake, na pili kwa kutoa Zakaat.”
Kutokana na waume kulazimishwa kuwahudumia wake, na kwamba ndoa ni pendekezo lililotiliwa mkazo (sana) la Uislamu, ni rahisi kuona kwanini urithi wa wanawake ni nusu ya wanaume. Pia tunatambua kwamba, katika ndoa ni wanaume wanaolazimishwa kuwapatia wanawake mahari yaliyo muafaka. Ni kweli, na inafaa kwa sasa kuzungumza misamiati ya waume na wake kuliko wanaume na wanawake. Allaah Anasema ndani ya Qur-aan (iliyotafsiriwa):
{{Na wapeni wanawake mahari yao, hali ya kuwa ni hadiya (aliyowapa Mungu). (Lakini hao wake zenu) wakikupeni kwa radhi ya nafsi zao kitu katika hayo (mahari) basi kuleni kwa furaha na kunufaika.}} [4:4]
Allaah Anasema ndani ya Qur-aan (iliyotafsiriwa):
{{… Nao (wanawake) wanayo haki kwa Sharia (kufanyiwa na waume zao) kama ile haki iliyo juu yao kuwafanyia waume zao. Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao.}} [2:228]
Hali hii haimuathiri (hata chembe) wadhifa wa Muumba ambaye Ameeleza kwamba Hawaangalii wanawake kuwa ni bora Kwake kuliko wanaume, au kinyume chake. Isipokuwa kwa njia nyepesi ya kugawa majukumu ndani ya nyumba yenye watu wazima wawili: mtu mmoja ni lazima awe na kauli ya mwisho katika masuala ya kila siku.Kama itakavyooneshwa hapa chini ndani ya sehemu kwenye masuala tofauti yanayoeleweka vibaya, ingawa kauli ya mwisho inaangukia kwa mume, ni kwa kupitia njia ya mashauriano kwamba amri zilizo nzuri zinafikiwa.
Wakati wanaume wanaruhusiwa kuoa hadi wake wanne, pia wanalazimika kabla yake kutimiza masharti ya kuweza kuwahudumia kifedha. Pia wamtumikie kila mke kwa haki na usawa pamoja na majukumu ya ndoa na uchumi. Allaah Anasema ndani ya Qur-aan (iliyotafsiriwa):
{{Na kama mkiogopa kutowafanyia uadilifu mayatima (basi ogopeni vile vile kutowafanyia uadilifu wanawake). Basi oeni mnaowapenda katika wanawake, (maadamu mtawafanyia insafu) wawili au watatu au wanne (tu). Na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi (oeni) mmoja tu, au (wawekeni masuria) wale ambao mikono yenu ya kiume imewamiliki. Kufanya hivi ndiko kutapelekea kutofanya jeuri.}} [4:3]
Juu ya hivyo, wanawake wanaruhusiwa kukataa posa yoyote iliyofanywa kwake na mposaji aliye tayari (kuoa), hivyo kama atahisi kwamba hawezi kutimiza kanuni za Qur-aan na Sunnah ikiwa ataolewa na mtu fulani, anaweza kukataa posa yake (mposaji). Ingawa (tuhuma hizi) si sahihi kwa Uislamu, ni vyema ikabainishwa kwamba dini zote mbili; Uyahudi na Ukristo unakubali ndoa ya mke zaidi ya mmoja. Fikra hii sio kwamba ni ngeni kwa wasiokuwa Waislamu kama inavyodaiwa.
Mwisho, uvaaji wa hijabu kwa wanawake ni jambo lisilo na mantiki kudai kwamba wanawake wapo chini kuliko wanaume. Ni bora kuikemea jamii inayokubali picha za uchi pornography kuliko kuikemea jamii inayokubali hijabu. Ikiangaliwa kwamba Allaah sio mwanamume wala mwanamke, na ikiangaliwa kwamba Hawatukuzi watu Kwake kwa kigezo cha jinsia zao, ikiangaliwa kwamba Muumba Anatujali sote wanaume kwa wanawake, ikiangaliwa kwamba shahawa za kimwili na shinikizo la mahitaji ya wanaume yapo juu kuliko yale ya wanawake….yakiangaliwa yote haya, basi hakuna maana yoyote kuvurumisha maelezo mabaya kwenye kanuni inayofuata iliyomo ndani ya Qur-aan (iliyotafsiriwa):
{{Waambie Waislamu wanaume wainamishe macho yao (wasitazame yaliyokatazwa), na wazilinde tupu zao, hili ni takaso kwao; bila shaka Mwenyezi Mungu Anazo habari za (yote) wanayoyafanya. Na waambie Waislamu wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasidhihirishe viungo vyao isipokuwa vinavyodhihirika (nao ni uso na vitanga vya mikono). Na waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao, na wasionyeshe mapambo yao ila kwa waume zao….}} [24:30-31]
{{Ewe Mtume! Waambie wake zako, na binti zako, na wanawake wa Kiislamu (wengine – waambie) wajiteremshie uzuri nguo zao. Kufanya hivyo kutapelekea upesi wajulikane (kuwa ni watu wa hishima ili) wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu.}} [33:59]
Kwenye suala hili linaloeleweka vibaya, kuna maelezo marefu ya kuendelea kuandika, mengi yao yakuonesha namna matendo ya sasa ya ardhi zilizo nyingi za Waislamu yanavyokwenda kinyume na amri za Qur-aan na Sunnah, ardhi ambazo wanawake wanafanywa kama vile ni bidhaa (huu sio Uislamu), hawana elimu (huu sio Uislamu), wanazuiwa haki zao za uchumi (huu sio Uislamu), na mengineyo. Hakika katika nukta hii, tunamuhimiza kila mmoja kushauriana na Qur-aan na Sunnah kabla ya kuukosoa Uislamu. Daima kumbuka kwamba Uislamu ni njia kamili ya maisha inayotoka kwa Muumba, na kwamba Waislamu ni watu wanaodai kuifuata njia hiyo ya maisha. Muislamu anaweza kudai kufuata Uislamu, lakini akawa ana makosa.


Read More