Advertising

  • Matunda

    faida ya tunda la KITZ
  • Matunda

    kula matunda kwa wingi
  • GYm

    Mazoezi muhimu kwa afya
  • Mazoezi

    dada anaimarisha misuli
  • Jovago

    Promoo siku ya watendao

February 3, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:53 PM | Be the first to comment!

HIVI NI VYAKULA VIKUU VYA KULA KWA MTU MWENYE VIDONDA VYA TUMBO MATOKEO NI NDANI YA MUDA MFUPI TU.




Imekuwa ni changamoto sana kwa watu wanaosumbuliwa na vidonda vya tumbo hii ni kwa sabubu zifuatazo
1.       Jamii haijatambua kuwa vidonda vya tumbo husababishwa na mienendo ya maisha yetu. Hivyo tiba yake kuu ni kubadili maisha tunayoishi nayo,kuanza lishe tunayopata,jamii tunayo ishi nayo, na kuepuka vinywaji vinavyo hatarisha afya ya ukuta wa mfuko wa chakula.
2.       Dawa kama omeprazole na zingine nyingi ambazo kwa pamoja tunaziita PROTON PUMP INHIBITORS zinapunguza utoaji wa asiodi ambayo ikitolewa kwa wingi inaenda kuharibu kuta za mfuko wa chakula. Hivyo zinazuia tu tindikali bila kushugulika na chanzo cha kuongezeka kwa hiyo tindikali. Hivyo bila kuondoa chanzo kinachosababisha kuongezeka kwa tindikali hiyo ya HCL hata siku moja huwezi kupona ndio mana siku hizi kuna dawa za kutuliza kama mmoja wapo wa wagonjwa nilikutana nae anasema hivyo. Inaweza kuwa leo hii na wewe umebahatika kusoma makala hii hivyo napenda nikuambie kuwa tiba ya vidonda vya tumbo ni wewe mwenyewe na tiba yake unayo hapo nyumbani tatizo ni kwamba tumeshaga kalili tu kwamba tiba lazima uikute madukani inauzwa.. vidonda vya tumbo vinatibika pata elimu ya lishe na badili tabia yako hakika utapona.

3.       Hizi dwa za vidonda vya tumbo zinatakiwa zitumike pale panapohitajika siyo maisha yako yote. Kwani hizi dawa mara nyingi huja na maudhi mbalimbali kwani ni dawa ambazo zimetengenezwa kwa chemikali. Dawa pekee ambazo ni sahihi kwa matumizi na zina madhara kidogo ni zile ambazo ni asili. Changamoto kubwa kwa hapa Tanzania ni kuwa huduma hii bado haijapata wataaalamu waliobobea wakaanza kutoa bidhaa bora na zenye kufanyiwa utafiti wa kutosha na zenye kiwango cha kimataifa.
4.       Tunapenda kula vyakula vyenye sukari nyingi,vyakusindika,viwandani na vyenye viungo vingi hivi vyote ndio visababishi vyakutolewa kwa tindikali ya HCL mwilini ambayo ikizidi inaharibu kuta za tumbo. Hivyo ni wakati sasa wa kurudi katika vyakula ambavyo bibi na babu zetu walivyo kula. Ni ukweli usiopingika kuwa vyakula vya super markert ni vya bei ya chini kuliko vyakula vya matunda, na mboga mboga. Je umeshaga jiuliza kwa nini hivyo vyakula vinauzwa kwa bei ndongo!!!  Fanya uchunguzi huu juice ya zabibu lita moja ukiitengeneza wewe ya asili itagharimu shilingi ngapi!! Na je lita moja ya zabibu juisi kiwandani ni shilingi ngapi!! Ifike sehemu tubadirike kwani tiba ipo nyumbani na vyakula tunavyokula ndivyo vinaangamiza jamii. Nalijua hilo mtanzania anapokuwa ana afya njema ni mjuaji sana kuhusu afaya yake laikini waswahili walisema mganmga hajigangi.

VIDONDA VYA TUMBO NINI??
>Ni kuharibika kwa ukuta wa tumbo la chakula na sehemu ya mwanzo ya utumbo mwembamba
Kuna aina kuu mbili za vidonda vya tumbo
1.       Gastric ulcers-hivi hutokea kwenye mfuko wa tumbo la chakula
2.       Duodenal ulcers-hivi hutokea sehemu ya mwanzo ya utumbo mwembamba



VISABABISHI VIKUU VYA VIDONDA VYA TUMBO
1.       KUONGEZEKA KWA TINDIKALI YA HCL KWENYE TUMBO LA CHAKULA
>imekuwa ni changamoto kubwa sana kwani moja ya visababishi hivi kila siku tunakumbana navyo ndiyo maana kwa nchi kama Tanzania kutibu vidonda vya tumbo ni changamoto kubwa.
VIFUATAVYO HUONGEZA TINDIKALI YA HCL
A.      MAWAZO
Watu wengi tunasumbuliwa na changamoto hii ya kushambuliwa na msongo wa mawazo kila siku hii inatokana na kutojua namna ya kushughulika na msongo wa mawazo. Jifunze namna ya kuepuka msongo wa mawazo utaona mabadiliko yakitokea .
B.      Madawa mbalimbali
Ø  Imekuwa ni desturi sisi kutumia dawa kama diclofenac,aspirin na zingine nyingi kama makande. Dawa hizi huzuia utengenezaji wa uteute unaolinda ukuta wa tumbo na hivyo kushambulia kwa kasi kwa ukuta wa tumbo. Pia dawa hizi huzia utengenezwaji wa ukuta wa tumbo na hatimaye ukuta kudhoofika na kuanza kushambuliwa na tindikali. Pia dawa hizi zinaua bacteria wanao stahili kukaa tumboni yani normal flora na kufanya wadudu nyemelezi kama helicobacter pylori kushambulia ukuta wa tumbo. Kuwepo kwa walinzi hawa huyo mdudu anaye sababisha vidonda vya tumbo hata siku moja hawezi kushambuliwa. Hivyo kuwalinda bakiteria hawa ni kuhakikisha tunawalisha chakula kinachowafanya waendelee kustawi na kukulinda. Jiulize ni chakula gani kinafaa?? Jibu ni vyakula vitokanavyo na mimea na matunda hufanya bactria walinzi wetu watulindi kwa umahili mkubwa.
C.      Uvutaji wa sikara na kunywa pome sana
D.      Vyakula vibaya tunavyokuwa kila siku
DALILI ZA VIDONDA VAYA TUMBO
1.       Tumbo kuwaka moto sehemu ya juu kulia na endapo maumivu yakizidi husambaa hadi mgongoni.
2.       Njaa hasa wakati wa usiku saa kumi na moja asubuhi utasikia tumbo linawaka moto
3.       Tumbo kujaa gesi sana
4.       Kichefu chefu na kuharisha kutokana na kubagua vyakula
5.       Inaweza kupelekea kutapika damu,kuishiwa damu na hatimaye kifo kama mgonjwa asipo wahishwa hospitali
6.       Kutoa choocheusi ni kiashiria damu inavia sehemu ya juu ya tumbo.
UKIONA DALILI KAMA HIZI TAFADHARI MUONE DAKTARI





VYAKULA VYA KUEPUKA KABISA
1.       Vyakula vyenye viungo vingi.
2.       Vyakula au kinywaji chenye caffeine hivyo angalia label kama wewe ni muhanga wa vyakula vya viwandani na hutaki kuacha.
3.       Pombe ya aina yoyote
4.       Vyakula vyote vya ngano nyeupe kama mikate nk kwani zina glutten
5.       Vyakula vya sukari nyinngi pia vinywaji vya sukari nyingi. Hii ni kwa sababu ulapo au unywapo sukari nyingi inalisha bakiteria wabaya na hatimaye hao bacteria wazuri kufa na hawa wabaya kuanza kushambulia kuta za tumbo la chakula. Hivyo sukari huenda kulisha bacteria wabaya.




HIVI NI VYAKULA VIKUU VYA KULA KWA MTU MWENYE VIDONDA VYA TUMBO
MATOKEO NI NDANI YA MUDA MFUPI TU.

1.       KULA CHAKULA KIDOGO KIDOGO
Ø  Hii ina maaana unatakiwa kuepuka kitendo cha kula chakula kingi kwa mara moja. Tenga chakula chako na kigawanye ule mara nyingi hii ni kwa sababu unapokula chakula kingi kwa wakati mmoja kunasababisha mmengenyo wa chakula utaenda polepole na hivyo kuzidi kuathiri zaidi ukuta wa tumbo. Pia tunashauri ule mara kwa mara ili kufanaya chakula cahako kifanyiwe kazi ipasavyo bila mrundikano na pia kupunguza maumivu ya tumbo.

2.       KULA VYAKULA VYA NYUZINYUZI AU FIBER
Ninapo ongelea fiber nina maaanisha kutoka kwenye mboga mboga na matunda pia nafaka kidogo. Hakikisha kila siku unatapata angalau 30gm za fiber itakusaidia na kukubadilisha maisha kabisa. Kwani utafiti unaonesha kuwa fiber inaongeza wingi wa kichocheo cha LEPTIN ambacho hukusaidia wewe ule kwa kiasi pia zinakata ulaji mwingi wa sukari pia inakufanya ukae muda mrefu tumbo likiwa limeshiba. Hivyo hapo utakuwa umeua ndege wawili kwa jiwe moja kwani umezuia aside,umeakata ulaji wa sukari na hakuna maumivu tena ya njaa. Swali la kujiuliza ni vyakula gani vina fiber nyingi?? Vyakula vipo vingi lakini jitahidi sana kutumia juice na mboga za majani ulizo zipika kwa mvuke pekee kwani zina fiber nyingi sana ppia kuna matunda yani wengi mkubwa wa fiber karibuni tujifunze mengi.
3.       JUICE YA KABEJI
Imekuwa ni furaha iliyoje nataja mboga ambayo kila siku tunaona ni mboga ambayo haina manufaa kwetu. Kwani utafiti unaonesha kuwa kabeji ina alkali ambayo hupunguza makali ya tindikali pia ina wingi wa vitamin C na viambata vingine mahususi ambavyo hufanya wale bacteria wazuri wale vizuri na watulinde na magonjwa nyemelezi kama huyo h. pylori. Pia ina VITAMINI K AMBAYO INA KAZI KUBWA SANA YA KUPONYESHA KABISA KUTA ZA MFUKO WA CHAKULA.
MATUMIZI
Andaa kabeji yako na uoshe vizuri hakikisha una APPLE MBILI NA CARROTI HATA MBILI katakata weka kwenye Brenda kasha saga kwa muda wa dakika 5-8 tumia juice hii mara tatu kwa siku asubuhi mchana na jioni kabla ya kula chochote kaa nusu saa kula chakula.

4.       MAJANI YA ALOE VERA
Utafiti unaonesha kwamba utumiapo kinywaji hiki kwa muda mrefu kinaponyesha vidonda vya tumbo. Wengi kinyaji hiki wanakiogopa ni kwa sababu ya uchungu wake. KAMA UTAHITAJI VIDONGE VILIVYOTENGENEZWA KITAALAMU BILA KUWEKEWA KEMICALI YOYOTE NIPIGIE 0767074124 KUMBUKA HIVI NI VIZURI HIVYO INAFAA KWA YULE AMBAYE ANASUMBUKA KUNYWA JUICE KWA SABABU YA UCHUNGU WAKE. HIVI NI VIDOBNGE VIKO KAMA PIPI VINAITWA ALOESOFT GEL CAPSULES
Unashauriwa utumie juice ya aloe vera  ROBO KIKOMBE MARA TATU KWA SIKU NUSU SAA BAADA YA KULA. Kwa wale watakao hitaji vidonge ni ALOE SOFT GEL CAPSULES 500mg mara mbili kwa siku nusu saa kila baada ya kula. Unashauriwa utumie dozi hii kwa muda wa miezi mitatu mpaka mine. ALOE CAPSULES ZINATIBU KABISA UKUTA WAKO ULIO ATHIRIWA NA ASIDI TUMBONI.
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:41 PM | Be the first to comment!

VIDONDA VYA TUMBO



                                       

Ugonjwa wa vidonda vya tumbo hutokea iwapo kidonda cha ukubwa wa angalau wa nusu sentimita kitatokea kwenye sehemu yeyote ya ukuta wa tumbo au utumbo wa binadamu. Kwa kawaida tatizo hili huleta maumivu makali sana ya tumbo ingawa si lazima kila maumivu ayapatayo mgonjwa husababishwa na vidonda vya tumbo.

Tafiti zimeonesha kwamba karibu asilimia 70 mpaka 90 ya vidonda vya tumbo husababishwa na aina ya vimelea vya bakteria wajulikanao kama Helicobacter pylori. Aidha matumizi ya baadhi ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya Non Steroid Anti-inflamatory Drugs kama Aspirin au Diclofenac huweza kusababisha au kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa huu.

Kuna dhana iliyozoeleka kuwa vidonda vya tumbo huathiri zaidi mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo (stomach). Dhana hii si kweli kwani sehemu inayoadhiriwa zaidi na tatizo hili ni sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo ijulikanayo kama duodenum.

Makundi ya PUD

Kuna makundi makuu yafuatayo ya ugonjwa huu

1. Vidonda vinavyotokea kwenye mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo (Gastric ulcers)
2. Vidonda vinavyotokea kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (Duodenal Ulcers)
3. Vidonda vinavyotokea kwenye koo (Oesophageal ulcers)
4. Vidonda vijulikanavyo kama Merckel’s Diverticulum ulcers.


Visababishi vya PUD

Vidonda vya tumbo husababishwa na

Maambukizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylori: Imeonekana kuwa zaidi ya asilimia 50 ya watu duniani wana vimelea hivi katika utumbo. Aidha, miongoni mwao, karibu asilimia 80 huwa hawaoneshi dalili yeyote ya kuugua ugonjwa wa vidonda vya tumbo.

Aina hii ya vimelea vya bacteria husababisha karibu asilimia 60 ya vidonda vinavyotokea kwenye tumbo (gastric ulcers) na zaidi ya asilimia 90 ya duodenal ulcers.

Hali hii husababishwa zaidi na kushindwa kwa mfumo wa kinga mwilini kuwaua na kuwaondoa kabisa vimelea hawa ndani ya mwili. Matokeo ya kushindwa huku husababisha kuwepo kwa uambukizi wa kudumu katika kuta za tumbo (chronic active gastritis), uambukizi ambao huharibu mfumo na uwezo wa kuta za tumbo kutunza homoni ya Gastrin, ambayo ni muhimu katika kuhakikisha mazingira ya tumbo yanakuwa na kiwango salama cha tindikali.

Kwa kawaida, kazi ya gastrin ni kuchochea utolewaji wa tindikali (gastric acid) kutoka kwenye seli za ukuta wa tumbo zijulikanazo kama Parietal cells. Iwapo bacteria hawa watashambulia na kuharibu ukuta wa tumbo, mfumo wa gastrin pia uharibika, na hivyo kusababisha gastrin kuzalishwa kwa wingi hali ambayo pia huchochea uzalishaji wa gastric acid kwa wingi. Matokeo ya kuzalishwa kwa wingi kwa tindikali hii hupelekea kuchubuka kwa ukuta wa tumbo na hivyo kusababisha vidonda vya tumbo.

Matumizi ya muda mrefu ya dawa za kuondoa maumivu za kundi la NSAIDs: Ukuta wa utumbo hujilinda na madhara yatokanayo na tindikali ya utumbo (gastric acid) kwa kuwa na utando laini (mucus) ambao hutolewa na vichocheo vijulikavyo kama Prostaglandins. Dawa hizi za kundi la NSAIDs huharibu mfumo wa kutengeza vichocheo hivi yaani prostaglandins na hivyo kufanya kuta za tumbo kukosa utando wa kuzilinda na mashambulizi ya tindikali hali ambayo hupelekea kutokea kwa vidonda vya tumbo.

Uvutaji wa sigara: Uvutaji sigara sambamba na maambukizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylorihuongeza madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Ifahamike tu kuwa uvutaji sigara pekee hausababishi vidonda vya tumbo.

Vyakula au viungo vya chakula vyenye uchachu: Kinyume na dhana iliyozoeleka miongoni mwa watu wengi, baadhi ya vyakula vyenye uchachu na upilipili kama vile pilipili, ndimu, limao na masala havina uhusiano na uwezekano wa kupata vidonda vya tumbo.

Watu walio katika kundi la damu la O: Imeonekana pia kwamba kundi la damu lijulikanalo kama blood group O, halina uhusiano wa kusababisha vidonda vya tumbo.

Unywaji wa pombe: Unywaji wa pombe pekee hausababishi vidonda vya tumbo. Hata hivyo, unywaji wa pombe sambamba na maambukizi ya vimelea vya Helicobacter pylori huongeza madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo.

Vitu vingine: Vitu vinavyohusishwa na uongezaji wa madhara ya vidonda vya tumbo ni pamoja na upasuaji wa tumbo (major abdominal surgeries), kuungua kwa moto (burns), ugonjwa wa figo; na kubadilishwa kwa viungo vya mwili kama figo au ini.

Dalili au viashiria vya PUD

Maumivu makali au kiungulia maeneo ya chembe moyo (epigastic pains): Maumivu juu kidogo ya tumbo mara nyingi huendana na muda wa kula chakula. Mtu mwenye vidonda kwenye tumbo (gastric ulcers) hupata maumivu makali sana kipindi anapokula au mara tu baada ya kumaliza kula wakati aliye na vidonda kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (duodenal ulcers) hupata maumivu makali anapokuwa na njaa na hupata nafuu pindi anapokula.

  • Kuvimbiwa au tumbo kujaa gesi. Hali hii pia yaweza kuendana na kubeua au kujamba mara kwa mara.
  • Kucheua na kuongezeka kwa mate yanayoshuka tumboni baada ya kucheua.
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito
  • Kutapika damu
  • Kupata haja kubwa cha rangi nyeusi au kahawia chenye harufu mbaya sana. Hii humaanisha mgonjwa anapata haja kubwa au choo kilichochanganyika na damu kwa mbali
Uwepo wa dalili kama kiungulia cha muda mrefu, kucheua na kutapika baada ya kula na historia ya kutumia dawa za kupunguza maumivu (NSAIDs) kwa muda muda mrefu bila kufuata ushauri wa daktari ni ishara tosha ya kumfanya mgonjwa kumuona daktari kumpima na kumfanyia uchunguzi ili kujiridhisha kuwa hana tatizo la vidonda vya tumbo.

Vipimo vya kutambua Ugonjwa wa vidonda vya tumbo

Vipimo vinavyotumika katika kutambua tatizo la vidonda vya tumbo ni pamoja na

1. Vipimo vya kuangalia ndani ya utumbo ambavyo ni pamoja na

  • Kipimo cha oesophagogastroduodenoscopy (EGD) au Upper GI endoscopy au gastroscopy. Kwa kutumia kipimo hiki, daktari huangalia moja kwa moja ndani ya utumbo wa mgonjwa kuona sehemu iliyo na vidonda pamoja na ukubwa wa tatizo lake. Aidha vipimo hivi humuwezesha daktari kuchukua sehemu ya utumbo iliyoathiriwa kwa ajili ya kuchunguza zaidi maabara ili kutambua uwepo wa vidonda au tatizo jingine linalomsumbua mgonjwa tofauti na vidonda vya tumbo.
  • Kipimo kingine kijulikanacho kama Barium meal kina uwezo pia wa kuthibitisha uwepo wa ugonjwa wa vidonda vya tumbo.
2. Vipimo vya kutambua uwepo wa uambukizi wa bakteria aina ya Helicobacter pylori kama

  • Kipimo kiitwacho Urea breath test
  • Kipimo cha kuotesha kinyama kilichochukuliwa kutoka katika kipimo cha OGD (culture from an OGD biopsy specimen).
  • Kipimo kinachoitwa Rapid Urease Test ambacho hufanywa kwa kutumia kinyama kilichochukuliwa kutoka kwenye utumbo wakati wa kufanya OGD. Kipimo hiki huangalia tabia ya vimelea hawa wa H. pylori.
  • Kipimo cha damu kwa ajili ya kutambua kiwango cha maambukizi ya vimelea wa H. pylori (antibody levels).
  • Kipimo cha haja kubwa kwa ajili ya kutambua kama bacteria wapo hai au wamekufa (stool antigen test). Kipimo hiki ni cha uhakika zaidi na nafuu kuliko kipimo cha Urea Breath Test.
  • Kipimo cha kimaabara cha kuchunguza kinyama kilichochukuliwa wakati wa kipimo cha OGD.
3. Vipimo vingine maalum vya kitaalamu zaidi kama

  • Kiwango cha homoni ya gastrin katika damu
  • Kipimo cha kuangalia uzalishaji wa homoni ya secretin ambayo uhusika katika uchocheaji wa homoni ya gastrin
  • Kupima kiwango cha tindikali inayozalishwa katika tumbo.
Hata hivyo vipimo hivi ni vya gharama zaidi na ni aghalabu hutumika mara kwa mara.

Matibabu ya Ugonjwa wa vidonda vya tumbo

Habari nzuri ni kuwa ugonjwa huu wa vidonda vya tumbo unatibika. Hata hivyo tabia ya baadhi ya wagonjwa wengi kuacha kumalizia dawa au kutumia dawa chini ya kiwango tofauti na walivyoshauriwa na madaktari husababisha kujirudia kwa tatizo au kufanya tatizo kuwa sugu zaidi.

Iwapo itagundulika uwepo wa H. pylori tiba inayotumika ni kuchanganya dawa za antibayotic (antibiotic) za aina tofauti kama Amoxicillin, Tetracycline, Clarithromycin au Metronidazole na dawa zenye uwezo wa kupunguza uzalishaji wa tindikali kwa wingi au kwa kitaalamu Proton Pump Inhibitors (PPI). Wakati mwingine daktari anaweza pia kuongeza dawa ya Bismuth Compound.

1. Kwa wagonjwa sugu, dawa za antibioc za aina tatu tofauti zinaweza kutumika. Dawa hizi ni pamoja na Amoxicillin + Clarithromycin + Metronidazole ambazo hutumika sambamba na dawa yeyote moja kutoka kundi la PPI kama vile Omeprazole au Pantoprazole pamoja na Bismuth Compound.

2. Kwa mgonjwa wa kawaida ambaye si sugu tiba bora inayoshauriwa ni kuchanganya dawa za antibiotic za aina mbili kama Amoxycillin + Metronidazole sambamba na dawa yeyote moja ya jamii yaPPI kama Pantoprazole.

3. Iwapo hakuna ushahidi wa kuwepo kwa uambukizi wa bacteria, dawa yeyote moja ya jamii ya PPIyaweza kutumika kwa muda mrefu zaidi bila kuchanganya na antibiotic yeyote.

Kwa kawaida kitendo cha kutibu na kuwaondoa Helicobacter Pylori humaliza na kuponyesha kabisa vidonda vya tumbo.

Hata hivyo, inawezekana kabisa ugonjwa huu kujirudia tena, hali ambayo hulazimisha kurudiwa tena kwa matibabu kwa kutumia aina nyingine ya antibiotics.

Aidha msomaji, inashauriwa si vyema kwa mgonjwa kujitibu mwenyewe bila kufuata ushauri wa daktari ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea iwapo dawa hazitatumiwa inavyopaswa.

Ni kweli Maziwa ya ng’ombe yanaponyesha vidonda vya tumbo?

Kinyume na dhana iliyozoeleka ndani ya jamii, maziwa ya ng'ombe hayaponyeshi vidonda vya tumbo, bali huongeza madhara yatokanayo na ugonjwa huu. Hii ni kwa sababu, maziwa huwa na tabia ya kutengeneza aina fulani ya kinga au ukuta (protective coat) kwa vimelea vya Helicobacter Pyloriambayo huvikinga vimelea hivi dhidi ya mashambulizi ya dawa na hivyo kufanya dawa kushindwa kuwaua na kuwaondoa kabisa vimelea hivi.

Kinachotokea ni kuwa, maziwa huondoa tu kwa muda maumivu ya tumbo kwa kupunguza makali ya tindikali iliyopo tumboni. Pindi maziwa haya yanapoisha, maumivu hurejea tena na kuwa makali kama hapo awali.

Matibabu ya vidonda vya tumbo kwa njia ya upasuaji

Zipo aina nyingi ya upasuaji unaofanywa ili kutibu ugonjwa huu. Kuvuja damu ndani ya mwili kupitia vidonda vya tumbo ni sababu mojawapo ya kufanyiwa upasuaji kwa vile ni hatari sana hata kupelekea kifo iwapo mgonjwa hatapata tiba haraka.

  1. Endoscopy: ni njia inayotumika kutibu uvujaji wa damu unaotokana na vidonda vya tumbo. Aina hii ya tiba hutegemea sana aina na sehemu vilipo vidonda vya tumbo. Tiba hii yaweza kufanyika kwa kuchoma sehemu inayovuja damu ndani ya tumbo au utumbo kwa lengo la kusitisha uvujaji wa damu (cautery) au kwa kuvifunga vidonda kwa kutumia vifaa maalum (clippings). Aidha tiba hii ni nzuri na haina madhara yeyote yale.
  2. Madaktari wengi hupendelea upasuaji ujulikanao kitaalamu kama simple oversewing sambamba na tiba ya kuondoa bakteria. Aidha, mgonjwa pia hushauriwa kuacha matumizi ya dawa zaNSAIDs kwa ajili ya kuondoa uwezekano wa damu kuendelea kutoka kwa vile kama ilivyoonekana hapo awali, matumizi ya dawa hizi huweza kusababisha uvujaji wa ndani kwa ndani ya mwili.
  3. Wagonjwa sugu, hufanyiwa baadhi ya upasuaji ambao huitaji utaalamu wa hali ya juu katika kuondoa neva na mishipa ya fahamu yenye kuhusika na uzalishaji wa tindikali katika tumbo.
Madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo

  1. Uvujaji wa damu ndani ya utumbo: Hali hii yaweza kusababishwa na vidonda kuenea hadi kwenye mishipa ya damu na hivyo kufanya damu kuanza kuvuja. Hali hii ni hatari sana na inahitaji tiba ya dharura.
  2. Vidonda vya tumbo huweza kusababisha tundu (kutoboka kwa ukuta wa tumbo) na kufanya vitu vilivyo ndani ya utumbo kutapakaa katika tumbo (abdomen) Hali hii huitwa peritonitis na ni hatari sana na inahitaji matibabu ya dharura. Aidha, kuenea huko kunaweza pia kuathiri tezi kongosho na kusababisha madhara katika tezi hiyo, ugonjwa unaojulikana kama pancreatitis.
  3. Vidonda vya tumbo vinaweza pia kuenea na kuathiri pia viungo vya jirani kama vile ini au kongosho (pancrease)
  4. Kuvimba kwa kuta za tumbo pamoja na makovu yasababishwayo na vidonda hivi huweza kusababisha kuziba kwa njia ya kupitishia chakula kutoka kwenye tumbo (stomach) kwenda sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (duodenum) hali ambayo kitaalamu huitwa gastric outlet obstruction.
  5. Iwapo vidonda vya tumbo vimesababishwa na H. pylori, kuna uwezekano wa kati ya mara tatu hadi ya sita ya mgonjwa kupata kansa ya tumbo (stomach cancer).
Read More