Advertising

  • Matunda

    faida ya tunda la KITZ
  • Matunda

    kula matunda kwa wingi
  • GYm

    Mazoezi muhimu kwa afya
  • Mazoezi

    dada anaimarisha misuli
  • Jovago

    Promoo siku ya watendao

February 3, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 8:56 PM | Be the first to comment!

CHAKULA KIFAACHO KAMA UNA UKIMWI






Kama unamaambukizo ya ukimwi unatakiwa ujue umuhimu wa kula chakula kitakachokuwezesha kuendelea kuishi maisha bora na yenye afya ili kupunguza magonjwa. kwa vile chembechembe za kulind mwili zimepunguzwa na ukimwi, mdudu yeyote wa magonjwa anaweza sababisha matatizo
Hizi ni muhimu kwani  ndio hujenga cells, muscles, organ na immune system. Kama mwili unakosa protein basi huanza tumia zile zilizobaki mwilini na ndipo mwili wako utaanza kuwa mnyong'ofu. Kiasi cha protein kinachohitajika kwa mtu mwenye ukimwi kisipungue gram 100 kwa mwanaume, na grams 80 kwa mwanamke kwa siku. 
Vyakula vya protein na kiasi chake ni kama ifuatavyo:
  • ziwa la kuku                                                   30gm
  • mguu wa kuku                                                11gm
  • bawa la kuku                                                  6gm
  • samaki   mmoja                                               22 gm
  • kipande kidogo cha nguruwe                            22 gm
  • mayai                                                                6gm
  • maziwa                                                              8gm
  • maharage        nusu kikombe                                kama 14 gm
  • karanga         vijiko 5                                           8gm
  • korosho robo kikombe                                       9gm
 Carbohydrate:
Hichi ni chakula  kinachotoa nguvu mwilili. Hakikisha unakula chakula cha nafaka na cha aina ya kunde. Vyakula kama ugali, ngano na viazi vina nutrients nyingi, pia vinachukua mda kuisha mwilini. Vyakula vya carbohydrate na kiasi chake angalia link hii: http://web.mit.edu/athletics/sportsmedicine/wcrhighcarbs.html

  
Fat
Kwa mgonjwa wa ukimwi kiasi cha fat  kisizidi 30gm. Kuna wakati kiasi cha cholesterol huwa kinaongezeka kukosababishwa na dawa anazokunywa mgonjwa. Hivyo ni muhimu sana kuangalia kiasi cha fat unachokula. Vyakula vya fat na kiasi chake fungua
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 8:54 PM | Be the first to comment!

Dawa za Kinga ya Ukimwi Zatumiwa Vibaya na Machangudoa




WANAWAKE wanaofanya biashara ya kuuza miili na wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja sasa wanatumia dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi aina ya Truvada kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo badala ya kutumia mipira ya kondomu.
Mwananchi lilizungumza na baadhi ya wafanyabiashara ya ngono jijini katika maeneo ya Mwananyamala Hospitali, Komakoma na Vingunguti ambao walisema kuwa wanatumia dawa hizo kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya VVU ili kuwaridhisha wateja wasiopendelea mipira hiyo. Baadhi ya wafanyabiashara hao walidai kuwa wanatumia Truvada kuzuia maambukizi pindi wanapokutana na wanaume wakware ambao huwabaka au kuwalazimisha kufanya mapenzi bila kinga.
“Hizi dawa tunazipata katika hospitali na wakati mwingine katika maduka makubwa ya dawa. Kwa sababu zinazuia maambukizi ya Ukimwi na sisi ni watu ambao tunafanya kazi katika mazingira hatarishi,” anasema Leyla Musa, mmoja wa wanawake hao.
Si hivyo tu, kwa kuwa hii ni biashara baadhi yao hukubali kufanya mapenzi bila mipira ili kupata fedha nyingi kutoka kwa wanaume.
Wengine hukimbilia huduma ya PEP
Baadhi ya wanawake hao wanasema kuwa baada ya kufanya mapenzi na wanaume kadhaa asubuhi huenda katika kliniki zinazotoa huduma za ARV na kudanganya kuwa wamebakwa na kisha hupewa huduma za dharura za ARV zinazoitwa kwa kitaalamu Post-exposure prophylaxis. Kwa kawaida mtu aliyebakwa au kujikata hupewa dawa aina ya Lamivudine, Zerophidine au Truvada kulingana na uzito wa tatizo.
“Tunatumia hizi dawa mara kwa mara lakini tunafanya hivyo katika kliniki tofauti ili tusigundulike,” alisema mmoja wao, mkazi wa Mwananyamala, Mariam Leshaniki.
Kwa maelezo ya Dk Rachel Baggaley, mtaalamu wa masuala ya Ukimwi wa Shirika la Afya Duniani anasema dawa za PEP zipo maeneo mengi duniani kwa sasa na zinafanya kazi kwa ufanisi pia hazina madhara kwa mwanamke.
“Dawa hizi siyo sumu mwilini, zinaingia kwenye mfumo wako wa damu kabla virusi havijajizatiti na inavizuia ili mradi uzitumie ndani ya saa 72,” anasema Dk Baggaley.
Dawa ya Truvada, ambayo ina mchanganyiko wa dawa aina ya Tenovofir na Emtricitabine, imethibitishwa kuwa salama kwa kupunguza makali ya VVU pia kuzuia maambukizi mapya. Dawa hizi zinazotengenezwa nchini India, zimekuwa msaada mkubwa wa tiba kwenye nchi zinazoendelea.
Mkurugenzi wa Sera, Mpango na Utafiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) Dk Raphael Kalinga alisema Tume hiyo inakemea kwa nguvu zote tabia inayofanywa na watu hao, kwani hakuna tofauti na kuvaa chuma kisha kujitumbukiza kwenye moto uwakao.
“Wanachofanya siyo sahihi. Ina maana kama una kinga ya malaria basi unatakiwa ukae karibu na mbu wakuume. Si unawakimbia… huo siyo uamuzi sahihi kabisa na ninawataka waondokane na tabia hiyo,” alisema.
Hata hivyo, Dk Kalinga alikiri kuwa ni kweli dawa hizo zinazuia maambukizi, lakini bado inategemea wingi wa virusi alivyonavyo mgonjwa pia mtu anaweza kuambukizwa magonjwa mengine ya zinaa kama kisonono, kaswende na pangusa.
“Kwa kweli tunakemea kwa nguvu zote na tunawashauri kwa usalama wao waondokane na mawazo hayo na wala wasijaribu hata mara moja kuacha kutumia kondom kuzuia maambukizi,” alisema.
Kama njia hii ya kuzuia maambukizi ya VVU itaendelea kufuatwa basi itabadilisha mfumo mzima wa kupambana na virusi hivyo ambao unahimiza matumizi ya kondomu kama kinga. Tangu mwaka 2010, tafiti tatu tofauti kuhusu dawa ya Truvada zimefanyika na kuonyesha uwezo mkubwa wa kuzuia maambukizi ya VVU iwapo zitanywewa kila siku. Wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsi moja waliotumia dawa hizo kila siku, walipopimwa damu walionekana kuwa salama kwa asilimia 99.
Wakati Dk Kalinga akipinga matumizi ya Truvada kama kinga ya VVU, Daktari wa magonjwa ya kuambukiza wa New York, Anthony Fauci, alisema ni vyema dunia nzima ikakubaliana na mpango wa kuanza kutumia dawa hizo ili kuokoa mamia ya watu walio katika hatari ya maambukizi.
“Kaswende, kisonono kinaweza kutibiwa na dawa za viua sumu (antibiotics), lakini Ukimwi ukiupata ni wa maisha yote hauwezi kutibiwa,” alisema Dk Fauci.
Kituo cha Kuzuia Magonjwa cha Marekani, kinaeleza kuwa hata kama itakubaliwa Truvada zitumike kama kinga, basi zitatolewa kwa wale ambao bado hawajaambukizwa. Pia, watatakiwa kupimwa kila baada ya miezi mitatu kuhakikisha kuwa hawajapata maambukizo na kupimwa ili kujua kama hawapati madhara yoyote yanayosababishwa na dawa hizo pia kama hawana magonjwa ya zinaa.
Watafiti waliogundua Truvada wanaeleza kuwa dawa hiyo kwa sehemu kubwa inakinga VVU na upande mwingine inasaidia kuua virusi vya Ukimwi kwa mtu ambaye tayari ameshaathirika. Hata hivyo, FDA na watafiti hao hawajaeleza kama Truvada inatibu moja kwa moja, isipokuwa wanasisitiza: “Inamkinga mtu kupata maambukizi mapya, inamsaidia mwathirika kwa kuua VVU pamoja na kumkinga dhidi ya magonjwa nyemelezi.”
Mtafiti wa Masuala ya Ukimwi, Dk Edward Maswanya anakana kuwa Truvada inazuia maambukizi na kusema siyo sahihi kutumia dawa hizo kama kinga.
“Kinga inayoaminika na kukubalika kuzuia maambukizi ni kondomu pekee hiyo Truvada haizuii kabisa,” alisema.
Alisema wanaofanya biashara ya ukahaba wanajiweka hatarini kupata maambukizi ya VVU pia wapo hatarini kuambukiza wengine. Baadhi ya wanawake wanaofanya biashara ya ngono wa eneo la Temeke, Tandika na Mbagala Zakhem walipohojiwa walidai kuwa mipira ya kiume imekuwa siyo salama kwao tena, kwani kuna wakati wanaume huitoboa kwenye chuchu na mara nyingine huzama ukeni kiasi cha kusababisha wafanyiwe upasuaji.
“Kondomu zinasaidia, lakini kwa wanaume wastaarabu, lakini ninapomeza hizi dawa hata nikibakwa zinazuia maambukizi na zinasaidia kama ninao nisiwaambukize,” alisema mmoja wa wanawake hao.
Mashoga nao
Mwanamume anayeshiriki mapenzi ya jinsi moja, Aly maarufu kama Aunt Aly, mkazi wa Kinondoni anasema ingawa anaishi na VVU, lakini yeye huzitumia dawa hizo kuepuka kupata maambukizi mapya na kuzuia asiwaambukize wengine, kwani hubakwa mara kwa mara na vibaka.
“Mara kwa mara sisi tunaingiliwa kwa nguvu na wakati mwingine wabakaji hawavai mipira sasa, tunakunywa hizi kama sehemu ya kinga, ingawa mimi nazinywa kama ARV za kawaida,” alisema.
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 8:51 PM | Be the first to comment!

SERIKALI KUDHIBITI UGONJWA WA UKIMWI KUFIKIA MAAMBUKIZI SIFURI




Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka akifungua Mkutano wa Serikali na wadau wa Ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi jana jijini Dar es 

Serikali imepanga mikakati na kusimamia juhudi zinazofanywa na kuendelezwa na wadau wa ukimwi kuhakikisha kuwa maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi yanapungua hadi kufikia sifuri ifikapo mwaka 2025.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti mtendaji kutoka Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt. Fatma H. Mrisho wakati wa mkutano wa serikali na wadau wa ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi jana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa mkutano huo Dkt. Mrisho amesema kuwa maambukizi ya ukimwi yamepungua ukilinganisha na miaka 10 iliyopita kwani idadi imepungua kutoka waathirika laki moja na elfu themanini hadi kufikia waathirika elfu sabini na mbili kwa sasa.
Akitoa mfano Dkt. Mrisho amesema kuwa Mkoa wa Njombe, Shinyanga, Dar es Salaam, Mbeya na Rukwa ni mikoa ambayo inaonyesha kuwa na idadi kubwa ya waathirika wa ukimwi hivyo kuwataka wadau wa ukimwi kutoka mikoa hiyo kutoa elimu ya kutosha kwa jamii ili kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi pamoja na magojwa ya zinaa.
Akifungua mkutano huo, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka amesema kuwa serikali imedhamiria kuanzisha mfuko utakaokua unashughulikia masuala ya ukimwi wakati wa bajeti ya mwaka 2015/2016 wenye lengo la kuondoa maambukizi mapya ya ukimwi nchini.
Aidha Dkt. Turuka ameitaka jamii kutowanyanyapaa waathirika wa ukimwi bali wawapende na kuwapa moyo ili waendelee kuwa na afya bora kwani serikali inawapigania na kuhakikisha kuwa wanatumia dawa za kuongeza maisha ili kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo.
Mkutano wa serikali na wadau wa ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi ulianzishwa mwaka 2003 ukifuatiwa na ule wa mwaka 2006 na kuendelezwa kila baada ya miaka miwili ambapo mkutano wa mwaka huu ni wa sita na umebeba kauli mbiu inayosema “Kwa yale mafanikio ambayo tumeyapata mpaka sasa tunayaendeleza”
Read More