Advertising

  • Matunda

    faida ya tunda la KITZ
  • Matunda

    kula matunda kwa wingi
  • GYm

    Mazoezi muhimu kwa afya
  • Mazoezi

    dada anaimarisha misuli
  • Jovago

    Promoo siku ya watendao

February 2, 2016

Mr Mtinangi

ADC kushiriki uchaguzi ZANZIBAR

Mr Mtinangi | 9:51 AM |

Makamu Mwenyekiti wa Kamati teule ya bodi ya wadhamini ya Chama cha Alliance Democratic Change - ADC, KHAMIS MOHAMMED amethibitisha ushiriki wa chama hicho
Makamu  Mwenyekiti wa  Kamati teule ya bodi ya wadhamini ya Chama  cha Alliance  Democratic Change  - ADC, KHAMIS  MOHAMMED  amethibitisha ushiriki wa chama hicho katika uchaguzi wa marejeo  unaotaraji kufanyika  tarehe 20 MACHI mwaka huu wa 2016.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari mjini UNGUJA, KHAMIS  amesema kutokana na vikao vya Chama vilivyofanyika , Chama hicho cha ADC kimeamua kutoa msimamo wake ambao ni kushiriki uchaguzi huo  wa marudio katika ngazi za uwakilishi na udiwani.

Khamis amesema kutokana na maamuzi hayo waliyoyafikia kama Chama , wametoa ombi maalum kwa wananchi wa Zanzibar kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi huo ili waweze kutimiza  haki yao ya kikatiba inayomtaka mwananchi achague ama kuchaguliwa  kwa mujibu wa sheria za nchi.

Akizungumzia kuhusu ushiriki wa nafasi ya urais wa Zanzibar  Kamishna wa mkoa wa MJINI MAGHARIBI UNGUJA kutoka ADC, JUMA ALI KHAMIS chama bado kimo katika mchakato wa majadiliano ya pamoja.

Mpaka  sasa vyama ambavyo vimethibitisha kushiriki marudio ya uchaguzi ni pamoja na  Chama cha Mapinduzi, Alliance Democratic Change ADC na Chama  cha Wakulima  -AFP.

Mr Mtinangi

About Mr Mtinangi -

Hajasomea uandishi wa habari yeye anapenda kuisaidia jamii kufahamu yale yanayotokea duniani japo kwa kiasi kidogo na nifuraha kwako hata kama mtu mmoja akipata taarifa mpya kupitia moojuhudi,namini katika haba ile na ile hujaza kibaba

Subscribe to this Blog via Email :