Advertising

  • Matunda

    faida ya tunda la KITZ
  • Matunda

    kula matunda kwa wingi
  • GYm

    Mazoezi muhimu kwa afya
  • Mazoezi

    dada anaimarisha misuli
  • Jovago

    Promoo siku ya watendao

MPYA

FAHAMU

February 7, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 4:06 AM | Be the first to comment!

Leicester City Baada ya Kuilaza City Yatuma Salamu Kwa Arsenal



Leicester City wanazidi kujikita kileleni mwa ligi kuu England baada ya leo kuwatungua vigogo wa EPL Man City kwa mabao 3-1.
Licha ya kuwa hawapewi nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa, vijana hao wa Ranieri wanaonekana kuwa na ari ya hali ya juu na kuwapa fursa kubwa ya kuendelea kuongoza ligi na hatimaye kutwaa ubingwa
Ifuatayo ni michezo ambayo endapo watashinda, basi watakuwa wamejipalilia njia ya kutwaa ndoo ya EPL msimu huu.

Robert Huth amepiga bao mbili kwenye game hiyo huku Riyad Mahrez akipiga bao moja wakati huo akiwa amepika moja ya bao ambalo lilifungwa na Huth na kumfanya kuingia top Five of master assist
Sergio Aguero aliifungia Manchester City bao pekee la kufutia machozi dakika za lala salama na kumfanya ashike nafasi ya nne baada ya kufikisha magoli 14.
Leicester tayari imeshatoa kichapo kwa Tottenham ambayo ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kwenye uwanja wa Spurs White Hart Lane mwezi January lakini matokeo ya leo dhidi ya City yalikuwa muhimu sana kwenye msimu huu wa kihistoria kwao.
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 3:47 AM | Be the first to comment!

Samatta Aanza Kwa Kishindo, Timu yake Yashinda 1 – 0



Baada ya nyota wa Tanzania Mbwana Samatta kufanikiwa kukipiga kwa mara ya kwanza kwenye klabu yake ya KCR Genk, mkali huyo ameandika ujumbe kwenye account yake ya instagram kuwashukuru wale wote wanaom-support na kumtakia mema.
Samatta ameandika ujumbe unaosomeka kama ifuatavyo: “Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru watanzania pamoja na mashabiki wangu wote wa @krc_genk_ kwa maombi na support yenu, Leo nimefanikiwa kucheza mchezo wa kwanza rasmi nikiwa na klabu yangu mpya @krc_genk_na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0”.
Kwenye mchezo huo ambao Genk ilikuwa ugenini ikicheza dhidi ya Muscron, Popa aliingia dakika ya 73 kuchukua nafasi ya Nikos Kareli na kumaliza dakika zote zilizo salia.
Mtanzania Mbwana Samatta ameishaanza kuichezea KRC Genk ya Ubelgiji baada ya jana kuingia katika mechi ya ligi na kucheza kwa dakika 17 wakati timu hiyo ilipoivaa Mouscron na kushinda kwa bao 1-0.
Samatta anaonyesha ni mtu wa malengo kweli baada ya kuacha magari yake zaidi ya matatu, na kwenda kuanza kutafuta maisha upya Genk.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa TP Mazembe, ameamua kuachana na kila kitu ukiwemo umaarufu wake mkubwa nchini DR Congo na kwenda kuanza upya nchini Ubelgiji kwa kuwa anataka kutimiza ndoto yake


Read More

February 6, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:59 AM | Be the first to comment!

Serikali yatoa tamko kuhusu udhalilishwaji aliyofanyiwa Mtanzania, India

Serikali imetoa tamko la kulaani kitendo kilichotokea nchini India kwa mwanafunzi wa kike wa kitanzania kuvuliwa nguo na kutembezwa barabarani ambapo Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje,Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na kimataifa imetoa tamko la kulaani suala hilo kwa kuitaka Serikali ya india kuchukua hatua.
Akitoa tamko hilo Bungeni Mjini Dodoma Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Dkt. Augustine Mahiga amesema ni kweli kwamba kuna mwanafunzi wa kike wa kitanzania alifanyiwa kitendo cha udhalilishaji nchini India kwa kuvuliwa nguo na kutembezwa 


barabarani suala ambalo lilizua mijadala mikubwa nchini kuhusu udhalilishaji huo.
“Wizara yetu imezungumza na Balozi wa India nchini na kumweleza ni kwa jinsi gani watanzania wamefadhaika na kusononeshwa na kitendo alichofanyiwa mtanzania mwenzao huko India na Balozi alituhakikishia kwamba amewasiliana na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi yake na kusema Serikali ya India kwa kushirikiana na Jeshi la polisi nchini humo wamefanikisha kuwakamata wote waliohusika na kitendo hicho na kuwafikisha mahakamani kujibu mashataka hayo”
“Pia Serikali ya India imeahidi kutoa ulinzi kwa wanafunzi wa kitanzania na wenye asilia ya Afrika  wanaosoma huko ili kuwalinda na kuwaepusha na vitendo hivyo vinavyofanya na raia ambao hawana nia njema kwa mahusiano mazuri ya kimataifa yaliyopo kati ya India na Tanzania”Alisema Mhe. Mahiga.
Serikali ya Tanzania imekuwa na mahusiano mazuri na Serikali ya India kwa miaka mingi sasa na kutokana na kitendo hiki kilichotokea nchini India,Waziri wa Mambo ya Nje ya India amefatana na Balozi wa Tanzania nchini humo kwenda Mji wa Bangalo ili kuongea na wanafunzi wakitanzania na wale wenye asili ya Afrika wanaosoma huko ili kujenga mahusiano mazuri na wazawa ikiwa ni jitihada za kupunguza vitendo hivyo kutokea mara kwa mara.
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:57 AM | Be the first to comment!

Twitter yazifunga akaunti za IS


Mtandao wa kijamii wa Twitter, umesema kuwa umesimamisha akaunti zaidi ya 120,000 kwa uchochezi tangu katikati mwa mwaka uliopita.
Kampuni hiyo inasema akaunti nyingi zilikuwa na uhusiano mkubwa ma kundi la kigaidi la Islamic State.
Twitter walisema kuwa kutokana na hatua hiyo mawasiliano ya kigaidi imeanza kutoweka kwenye mtandao wao.
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:55 AM | Be the first to comment!

AU yaitaka Burundi kukubali wanajeshi wake

                                                 Rais wa Chad Idris Deby ndio mwenyekiti wa AU
Muungano wa Afrika, AU, umetoa wito kwa viongozi wa mataifa matano kuishawishi Burundi kukubali kikosi maalum cha kudumisha amani kufuatia miezi kadhaa ya ghasia za kisiasa nchini humo.


Kamati hiyo maalumu ya AU, inamshirikisha Waziri Mkuu wa Ethiopia, pamoja na Marais wa Afrika Kusini, Mauritania, Gabon na Senegal.
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza amepinga mpango huo, akisema huo ni uvamizi.
Uamuzi wake wa mwaka uliopita kutaka kugombea awamu ya tatu ulianzisha mapigano hayo ambapo kufikia sasa mamia ya watu wameuawa.
iongozi wa Afrika waliokuwa wakikutana juma lililopita walighairi juu ya swala la kuwatuma wanajeshi 5,000 wa kudumisha amani, na badala yake wakaamua kutumia njia za kidiplomasia.

Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:49 AM | Be the first to comment!

Wengine waliomvua nguo Mtanzania mbaroni

                                            Gari la wanafunzi hao liliteketezwa
Washukiwa zaidi wamekamatwa na maafisa wa polisi nchini India kuhusiana na kisa ambapo mwanafunzi Mtanzania alipigwa na kuvuliwa nguo mjini Bangalore.
Washukiwa wengine wanne wamekamatwa na kufikisha tisa, jumla ya washukiwa wanaozuiliwa na polisi.
Maafisa watatu wa polisi pia wamesimamishwa kazi, wakisubiri kufanyiwa uchunguzi.
Watatu hao wanatuhumiwa kukataa kupokea malalamiko kuhusu kushambuliwa kwa mwanafunzi huyo wa kike wa umri wa miaka 21 pamoja na wenzake wa tatu.
Balozi wa Tanzania nchini India John WH Kijazi anatarajiwa kukutana na waziri wa mambo ya ndani ya jimbo la Karnataka.
Baadaye, atakutana na wanafunzi waliodhalilishwa karibu na chuo chao.
Maafisa wawili kutoka afisi ya wizara ya mambo ya nje ya India wataandamana na balozi huyo.
Kisa cha kushambuliwa kwa wanafunzi hao kimeshutumiwa vikali na serikali ya Tanzania ambayo imeitaka India kuhakikisha usalama wa wanafunzi wanaoishi na kusomea humo.
Watanzania mtandaoni pia wamekuwa wakishutumu kisa hicho na kuitaka serikali kuchukua hatua.
Tangu kutokea kwa kisa hicho, wanafunzi wengi kutoka Tanzania wamekuwa wakihofia usalama wao
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:44 AM | 1 Comment so far

Balozi wa Tanzania aridhishwa na hali Bangalore


Balozi Kijazi amesema wenyeji na Waafrika wanafaa kuwa wakikutana na kujadiliana
Balozi wa Tanzania nchini India John Kijazi amesema ameridhika kwamba serikali ya nchi hiyo imeweka mikakati ya kutosha kuwalinda wanafunzi, kufuatia kisa ambapo wanafunzi wanne walishambuliwa mjini Bangalore Jumapili.
Akizungumza baada ya kutembelea pahala ambapo wanafunzi hao walishambuliwa, na mmoja wao kuvuliwa nguo, Bw Kijazi amesema huenda kisa hicho kilitokana na suitafahamu.
“Kilicho muhimu ni tuangalie siku za usoni kwa sababu tusipofanya hivyo tutapotea. Tunahitaji kutatua tatizo la sasa lakini pia tuangalie mikakati ya muda mrefu,” ameambia wanahabari.
“Nimeridhishwa na hatua za kiusalama ambazo zimechukuliwa na serikali hapa. Kuna maafisa ambao wamesimamishwa kazi.”
Balozi huyo alikata kutaja kisa hicho kama cha ubaguzi wa rangi.
“Hatukutaka kuangazia masuala ya ubaguzi wa rangi na mambo mengine kwa sababu nadhani vyombo vya habari vinapendezwa sana na hilo. Tumejadiliana kuhusu masuala halisi na hatua madhubuti ambazo tayari zimechukuliwa na serikali ya hapa,” amesema.
Bw Kijazi alisafiri hadi Bangalore akiandamana na maafisa wawili wa wizara ya mambo ya nje ya India ambapo walikutana na waziri wa mambo ya ndani wa jimbo la Karnataka Dkt G Parameshwara na wakuu wa polisi wa jimbo hilo.
Polisi mjini Bangalore wamewakamata watu tisa kuhusiana na kisa hicho.
Mkuu wa kituo cha polisi cha Soldevenahalli pia amesimamishwa kazi kwa tuhuma kwamba hakuchunguza kwa undani kisa hicho baada ya mmoja wa wanafunzi hao kupiga ripoti.
Konstebo wa polisi pia amesimamishwa kazi kwa kutochukua hatua kuzuia wanafunzi hao wasishambuliwe na umati
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:40 AM | Be the first to comment!

Tetemeko baya lakumba Taiwan



Tetemeko kubwa la ardhi limekumba Taiwan Kusini, na kuangusha jengo moja la ghorofa 17 ambapo hadi kufikia sasa watu watatu wamethibitishwa kufariki.
Tetemeko hilo la kipimo cha Ritcher 6.4 lilitokea karibu na mji wa Tainan.
Zaidi ya watu 200 wameokolewa kutoka kwa jengo hilo, ingawa waokoaji wangali wanajaribu kuwafikia watu wengine ambao inadhaniwa wangali wamekwama katika mabaki ya jengo hilo.
Tetemeko hilo liligonga usiku wa manane wakati watu wengi walikuwa wamelala.
Kumetokea matetemeko mengine madogo matano mda mfupi baada ya tetemeko hilo kuu.
Idara ya kusimamia maswala ya chini ya radhi inasema kuwa tetemeko hilo lilitokea sehemu ya juu pekee, hali ambayo husababisha madhara makubwa zaidi
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:36 AM | Be the first to comment!

Washauriwa kubeba Kondomu siku ya Valentine

Thailand imezindua kampeni kabla ya siku ya wapendanao ya Valentine ikiwataka vijana kutosikia aibu wanapobeba mipira ya kondumu.


Mpango huo unaonekana kubadilika ikilinganishwa na kampeni zilizokuwa zikifanywa hapo awali,ambapo vijana walihamasishwa kuzuru maeneo ya kidini na baadaye kwenda nyumbani baada ya mikutano na wapenzi wao badala ya kushiriki katika ngono.
Thailand ina idadi kubwa ya wasichana waliotungwa mimba duniani pamoja na na viwango vya juu vya magonjwa yanayoambukizwa kupitia ngono
Kampeni hiyo inayotarajiwa kuendelea hadi mwaka 2019,inaambatana na mipiango ya hivi karibuni inayolenga kuangazia mimba za vijana.
Mamlaka zimehamasisha umuhimu wa kutumia mipiria ya kondomu katika miaka ya nyuma pamoja na kuwashuri vijana kutoshiriki ngono.
Lakini mwaka huu wamesema watalenga kupunguza unyanyapaa kuhusu utumizi wa kondomu pamoja na kurahisisha upatikanaji wake mbali na kuimarisha mipira hiyo.
Msemaji wa Wizara ya afya nchini Thailand Lertwilairrattanapong amesema kwamba vijana hawafai kuaibishwa kuhusu ununuzi wa mipira ya kondomu.
''Jamii pia inafaa kukubali kwamba vijana wasichana wanafaa kununua kondomu,ambazo ni bora badala ya wasichana hao kupata mimba'',akisema.
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:25 AM | Be the first to comment!

Alikiba azindua video ya Lupela, mastaa wenzie wampa kampani






Alikiba amezindua video ya wimbo wake Lupela Alhamis hii kwenye hoteli ya Slipway jijini Dar es Salaam.

Alikiba akiongea mbele ya wageni waalikwa
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na mastaa kibao walioenda kumpa kampani. Video hiyo iliyofanyika nchini Marekani na sehemu ya mradi wa Wild Aid 
Inamuonesha Kiba akicheza dance ya kukata na shoka na msichana mrembo wa Kimarekani aliyechukua uhusika wa Lupela.
Mastaa waliouhudhuria uzinduzi huo ni pamoja na Weusi, Wema Sepetu, Jokate, Vanessa Mdee, Lady Jaydee, Navy Kenzo, Ommy Dimpoz, Mr Blue, Mwana FA, Barakah Da Prince na wengine.
Pia walikuwepo watangazaji mbalimbali kama B12 na Perfect Crispin wa Clouds FM, Dulla wa EA Radio na wengine. Mama yake Alikiba pamoja na dada yake nao walikuwepo
                                                

Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 12:17 AM | Be the first to comment!

Kun Sergio Aguero Kutoa tuzo ya mchezaji bora January 2016





Mkali wa kucheka na nyavu wa the blues wa jijini Manchester ameisaidia timu yake kubeba point 8 katika mechi nne na kuifanya manchester city unbeaten.
 Katika mechi hizo nne Sergio Aguero amefunga magoli matano na kutoa asist moja,December tuzo hiyo ilichukuliwa na mkali wa Nigeria na club ya watford Odion Ighalo ambaye pia alifunga magoli 5 december
               
Read More

February 5, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 11:59 PM | Be the first to comment!

Kwanini kocha Mayanja wa Simba hampi nafasi kikosini Said Ndemla?


February 3 kocha wa Simba Jackson Mayanja amekutana na swali la waaandishi wa habari juu ya kiungo wa Simba anayeichezea timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Said Hamisi Ndemla kutopewa nafasi kwenye kikosi cha Simba toka kocha Masanja aanze kazi.
Kama ulikua hujui, Wataalamu wa mambo wanasema Ndemla ameichezea Simba sio zaidi ya dakika 50 hadi sasa
Read More

February 4, 2016

Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 7:52 AM | Be the first to comment!

Kinana aanza shughuli mbalimbali za maendeleo kuelekea siku ya maadhimisho ya miaka 39 ya Kuzaliwa kwa CCM




Wajumbe wa Kamati ya Siasa CCM mkoa wakisikiliza wakati Kaimu Katibu wa Mkoa Ndugu Mary Maziku akiwakilisha taarifa za maandalizi ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye ofisi za CCM mkoa wa Singida
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 7:49 AM | Be the first to comment!

Habari njema “Lady In Red” kufanyika nchini Uingereza 13 Februari



Lady In Red ni onesho la mitindo ambalo limekuwa likifanyika kwa muda mrefu hapa nchini Tanzania, Onesho hilo lilianzishwa na Mama mitindo maarufu nchini kama Asya Idarous, kwa lengo la kuendeleza na kuibua vipaji vipya ndani ya Tasnia hiyo ya Mitindo. Kadri siku zinavyo zidi kusonga Onesho hilo limeendelea kuwa na ufanisi mzuri ukilinganisha na awali, ikiwa ni pamoja na ongezeko la hamasa kwa wanamitindo na kuwapa muamko wa kimaendeleo zaidi kupitia Onesho hilo, hasa kwa kuwapa kipaumbele upcoming Designers.
Lady In Red 2016  kwa sasa inaelekea kuwa ya kimataifa kufuatia hamasa kubwa ya Onesho hilo kwenda kufanyika nchini Uingereza. Hii ni habari njema kwa wote wapenzi wa mitindo yaani designers, models na wadau wengine.
Lady In Red 2016 Tanzania  imefanyika  31/1/2016 katika ukumbi wa Danken House Jijini Dar, ambapo ilifanikiwa kung’ara kwa style yake, chini ya usimamizi mzuri kabisa wa Asya Idarous, siku hiyo ndipo ilitangazwa Rasmi kuwa Lady In Red 2016 kwa mara nyingine itafanyika nchini Uingereza usiku wa kuamkia valentine day tarehe 13,/2/2016. Siku hiyo nyota wa wimbo wa “Pacha wangu” maarufu kama Rich Mavoko, akitokea hapa Tanzania atatumbiza kwenye onesho hilo.  Support yako inaweza ikapelekea Lady In Red iwe yakimataifa zaidi.

Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 7:46 AM | Be the first to comment!

Mama Janeth Magufuli atembelea kambi ya wazee wasiojiweza na walemavu ya Nunge

Mke wa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli, mama Janeth Magufuli ametembelea katika kituo cha Nunge kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam ambacho kinatumika kuhifadhi wazee wasiojiweza na walemavu.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi mchele, unga na maharage Mzee Anthony Kingongoti Mwenyekiti wa wakaazi wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao



Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na wagonjwa waliofika kupata huduma katika zahanati ya  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao

Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 7:40 AM | Be the first to comment!

Kasi ya Rais Dkt. Magufuli yagonga mwamba kwa polisi Mlandizi




Askari wa Kikosi cha Polisi cha Usalama barabarani, Kituo cha Polisi Mlandizi wamewasotesha kwa takribani masaa mawili  na nusu wanahabari kupata risiti ya malipo ya faini aliyotozwa dereva wao baada ya kudaiwa kufanya kosa la kutaka kulipita gari lingine sehemu isiyoruhusiwa.
Sakata hilo lilianza wakati polisi alipolisimamisha gari hilo katika Kituo cha Visiga, Mlandizi, wilayani Kibaha, Pwani ambapo alimuomba dereva leseni yake na kumuamuru ateremke ili ajieleze akiwa nje ya gari na hatimaye kumlipisha faini ya sh. 30,000 kwa kosa hilo.
Baada ya wanahabari waliokuwa kwenye gari hilo kumsubiri dereva kwa takribani nusu saa, waliamua kuteremka kumfuata kujua kinachoendelea, kwani walikuwa wana haraka ya kufika Dodoma muda waliopangiwa  ili waungane na msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenda Singida kwenye maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM.
Lakini baada ya mmoja wao kuwauliza trafiki sababu zinazosababisha kutomwachia dereva, walijibu kwa kashfa na kejeli, wakihoji kwani nyie ni akina nani? na dereva wenu asipolipa faini basi watakaa hapo kituoni hadi jioni.
Mmoja wa wanahabari hao alilipa faini ya sh. 30,000 na kuomba risiti, hapo ndo songombingo ilianza ambapo Trafiki wa kike alijibu kuwa hawana risti bali kinachofanyika pale ni kuandikiwa tu taarifa ya kosa lao na kwenda Kituo cha Polisi cha Mlandizi kilichopo takribani umbali wa Km 5, na wengine waliokamatwa kwa makosa mbalimbali ya usalama barabarani waliamuliwa kwenda kupata risiti katika kituo hicho.
Mabishano makubwa yalitokea hapo baina ya Trafiki na wanahabari waliokuwa wanahoji ni kwa nini kitabu cha risiti wala mashine za kielekroniki havipo hapo ili kurahisisha kazi. Askari wa kike na mmoja wa kiume walijibu kuwa wasifundishwe kazi.
“Msitupotezee muda hapa, nendeni Mlandizi, mkapate hiyo risiti,”alisema trafiki wa kike. Wakati anasema hivyo kumbe mhasibu wao alikuwepo palepale Visiga, lakini bila kuwaambia ondokeni naye ili akawahudumie.”
Pia, mmoja wa Trafiki aliuponda sana utaratibu wa wakosaji kulipia faini kwa kutumia mashine za elekroniki akidai kwamba ni hasara kwa trafiki na madereva ni bora mashine hizo ziishie Dar es Salaam zisipelekwe Mkoa wa Pwani.
Trafiki wengine walisikika wakisema kuwa hivi hawa jamaa wanaolazimisha kupewa risiti ni akina nani, waache waende zao, wakafie mbali.
Maneno hayo yalionekana kuwaudhi wanahabari na kuamua kuondoka kwenda Kituo cha Polisi Mlandizi, kufuatilia risiti, lakini walichokikuta huko ni maajabu, hasa ya kuambiwa kuwa Mhasibu hayupo ofisini kwake amekwenda kununua peni.
Baada ya wanahabari hao kusubiri kwa takribani saa moja, waliamua kwenda kaunta kuulizia na kuomba kuzungumza na Mkuu wa Kituo ili awasaidie kupata risiti wawahi kwenda Dodoma, lakini mmoja wa askari aliyekuwa zamu aliwajibu kuwa Mkuu wa Kituo hajafika ofisini amepitia Kibaha Mjini kwenye mkutano.
Alipoombwa awasaidie kumpata mhasibu, askari huyo alitoka nje hadi ofisi ya Mhasibu alipomkosa akaamua kumpigia simu na kuwajibu kuwa ametoka mara moja kwenda kununua peni. Jambo hilo liliwashangaza sana wanahabari na kuanza kuhoji kwamba iweje kitendo cha kununua peni  kitumie muda wote huo na kusababisha watu wakiwemo wao kukosa huduma tena asubuhi majira ya saa 3.
Mmoja wa wananchi aliyekwenda kituoni kupata huduma ya risiti, alisikika akilalamika kuwa tabia hiyo ya kuchelewesha kutoa huduma ipo sana kituoni hapo na kwamba wanaoonekana kabisa hawaendani na kasi ya kufanya kazi anayoitaka Rais Dk  John Magufuli ya ‘Hapa Kazi Tu’.
Mle ndani ya Kituo cha Polisi walisikika wakiulizana kwamba hivi hawa watu wanaowasumbua na kutaka kuzungumza na mkuu wa kituo ni akina nani hawa, eti wanataka risiti, ebu tumpigie simu mhasibu aje atuondolee balaa hapa.
Baada ya muda askari mwenye E 3275 alitoka nje na kuwaambia wanahabari kuwa mhasibu amepigiwa simu atakuja muda si mrefu mhudumiwe muondoke, lakini mmoja wa wanahabari hao anayemiliki blogu ya Full Shangwe, John Bukuku,  alihoji kuwa hivi ni kwanini polisi wa kituo hicho hawaendani na kasi ya Rais Dk. Magufuli? alijibu kuwa kwani kuna nini?
Baada ya muda Mhasibu aliwasili kwa Bodaboda, na alipofika aliwakebehi wanahabari kwamba anawashangaa kwa yeye kumuacha kule Visiga alikokuwa nao na kuwahi kituoni, ndipo wanahabari nao wakashangaa kumuona tena kituoni hapo wakati wlipofika kituoni waliambiwa ameenda kununua peni.
Dereva alimwambia haya twende ukachukue risiti yako muondoke na watu wako. Dereva aliingia na kupatiwa risiti kutoka kwenye kitabu kipya ambacho kwa mujibu wa dereva kilionekana dhahiri kuwa ni kipya.
Lakini kwa masaa yote waliyokaa wanahabari kituoni hapo (takribani masaa mawili), hawakuwaona madereva wa magari waliokamatwa pamoja na gari lao na kuandikiwa makosa na faini pale Visiga, hawakufika Kituo cha Polisi kupatiwa risiti, kitendo ambacho kinaashiria fedha wanazolipishwa madereva kwa kutenda makosa hazitolewi risiti, hivyo mapato ya serikali kupotelea mifukoni mwa baadhi ya askari wa kikosi cha usalama barabarani.
Baada ya wanahabari hao kupata risiti majira ya saa 4:15 waliamua kuondoka kituoni hapo kuanza safari ya kwenda Dodoma kuwahi msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Abdulrahman Kinana uliokuwa unawasubiri kwenda Singida.
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 7:37 AM | Be the first to comment!

ATE yalia na kukithiri kwa vitendo vya rushwa nchini




chama cha Waajiri nchini (ATE) kimelalamikia vitendo vya rushwa kuwa vikwazo katika biashara hivyo wameiomba serikali kukemea vitendo vya rushwa pamoja na urasimu ili kuboresha mazingira mazuri ya biashara za kitaifa na kimataifa.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa  Chama cha Waajiri (ATE),Aggrey Mlimuka  akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Waajiri amesema kuwa serikali inapaswa kujenga mazingira bora kwa waajiri wanaotoa nafasi za  ajira ili kujenga uchumi endelevu wa nchi.
Mkurugenzi huyo ameiomba serikali iondoe vikwazo kwa waajiri wanaoajiri wataalamu kutoka nje kutokana na kukosekana kwa wataalamu hao nchini pamoja na kupunguza tozo kubwa za mafunzo ya wafanyakazi ambayo ni asilimia 5%.
Kwa upande wake Afisa Mwajiri wa Kampuni ya Utalii amesema kuwa kwa muda mrefu wamekua wakipata adha kubwa wakati wa kuajiri watu kutoka nje ya nchi suala ambalo serikali inatambua kuwa baadhi ya taaluma hazipatikani nchini hivyo kulazimika kuchukua wataalamu kutoka nje
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 4:44 AM | Be the first to comment!

Wabunifu chipukizi walivyolipamba jukwaa la Lady In Red Fashion show 2016




Wabunifu zaidi ya thelasini (30) wameweza kulipamba vilivyo jukwaa la mitindo hapa nchini la Lady In Red fashion show 2016 lililofanyika jijini Dar es Salaam huku likishuhudiwa na wadau mbalimbali wa mitindo hapa nchini.Jukwaa hilo linaloandaliwa kila mwaka na Mama wa Mitindo nchini,  Asya Idarous Khamsini  ameelezea kuwa lengo la jukwaa hilo ni kuwa kimbilio la wabunifu chipukizi na kama darasa la tasnia hiyo.Onesho hilo kwa mwaka huu ni la 12 tokea kuanzishwa kwake huku likia limewatoa wabunifu chipukizi mbalimbali hapa nchini ambao wanamajina makubwa kwa sasa

Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 4:36 AM | Be the first to comment!

Dayna Nyange anatukaribisha kuitazama hii video yake mpya ‘angejua’

Dayna Nyange ni kipaji kingine tulichonacho kwenye muziki wa bongofleva Tanzania, 2016 ameianzisha kwa kutusogezea hii single yake ya kwanza kwa mwaka huu inaitwa ‘angejua‘ na video yake mpya ndio hii                angejua





                           
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 3:45 AM | Be the first to comment!

Waajiriwa Waomba Serikali Kudhibiti Rushwa Maofisini



Chama cha Waajiri nchini kimelalamikia vitendo vya rushwa kuwa vikwazo katika biashara hivyo wameiomba serikali kukemea vitendo vya rushwa pamoja na urasimu ili kuboresha mazingira mazuri ya biashara za kitaifa na kimataifa
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Waajiri (ATE), Aggrey Mlimuka akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Waajiri amesema kuwa serikali inapaswa kujenga mazingira bora kwa waajiri wanaotoa nafasi za ajira ili kujenga uchumi endelevu wa nchi
Mkurugenzi huyo ameiomba serikali iondoe vikwazo kwa waajiri wanaoajiri wataalamu kutoka nje kutokana na kukosekana kwa wataalamu hao nchini pamoja na kupunguza tozo kubwa za mafunzo ya wafanyakazi ambayo ni asilimia 5%.
Kwa upande wake Afisa Mwajiri wa Kampuni ya Utalii amesema kuwa kwa muda mrefu wamekua wakipata adha kubwa wakati wa kuajiri watu kutoka nje ya nchi suala ambalo serikali inatambua kuwa baadhi ya taaluma hazipatikani nchini hivyo kulazimika kuchukua wataalamu kutoka nje.
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 3:41 AM | Be the first to comment!

Kwa Mwendo Huu wa Barcelona Wengi Watalia Mwaka Huu!na kwa moto huu Arsenal wataweza kuwazuia?

Klabu ya Valencia chini ya nyota wa zamani wa Manchester United Gary Neville ilipokezwa kichapo cha mwaka na klabu ya Barcelona katika nusufainali ya michuano ya Copa del Rey baada ya kubebeshwa magoli saba.
Mechi hiyo ya mkondo wa kwanza ilichezewa uwanjani Nou Camp.Luis Suarez alifunga mabao manne, huku nyota wa Argentina Lionel Messi naye akijizolea magoli matatu.

Neymar alishindwa kufunga penalti. Valencia walidhofishwa zaidi na hatua ya beki Shkodran Mustafi kumchezea visivyo Messi kipindi cha kwanza, kosa lililomfanya kufukuzwa uwanjani
Neville hajashinda mechi hata moja ligini kati ya nane alizosimamia tangu kuchukua usukani Desemba.
Neville alikuwa amerejea uwanja ambao enzi yake ya uchezaji alipanda ushindi mkubwa na muhimu sana.
Akiwa na umri wa miaka 24, alikuwa kwenye timu ya United iliyoshinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kujikwamua dhidi ya Bayern Munich fainali ya 1999 uwanjani Nou Camp.
Akizungumza baada ya mechi hiyo dhidi ya Barca, Neville alisema siku hiyo ni moja ya siku zenye machungu zaidi katika maisha yake katika ulimwengu wa soka

Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 1:47 AM | Be the first to comment!

Rais Magufuli Aanzisha Mkoa Mpya wa Songwe…!



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Joseph Magufuli ameidhinisha kuanzishwa kwa Mkoa mpya wa Songwe na wilaya nyingine mpya nchini.
Akitoa tamko hilo kwa niaba ya Rais Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amesema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imempa Mamlaka Rais ya kugawa Nchi kwa kadri ambavyo atakapoona inafaa.
George Simbachawene alisema kutokana na mamlaka hayo aliyopewa Rais jumla ya Wilaya sita na Mkoa mmoja wa Songwe umeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Mkoa mpya wa Songwe umeanzishwa kutoka Mkoa wa Mbeya.
Amezitaja Wilaya mpya zilizoanzishwa kuwa ni Wilaya ya Songwe Mkoa wa Songwe,Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es salaam, Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam, Wilaya ya Mlanyi Mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi.
“Nichukue fursa hii kuwaagiza Wakuu wa Mikoa wote ambao Wilaya mpya zimeanzishwa kufanya maandalizi rasmi ili Mkoa na Wilaya hizo ziweze kuanza kufanya kazi,aidha mkazo uwekwe kwenye upatikanaji wa Ofisi na huduma zote muhimu kupatikana kwa urahisi katika Mkoa naWilaya hizo mpya” Alisema Mhe Simbachawene.
Read More
Mr Mtinangi
Mr Mtinangi | 1:42 AM | Be the first to comment!

Guinea Yatupwa Nje CHAN,DR Congo Yatinga Fainali

Jamhuri ya Demokrasia ya Congo imefuzu kwa fainali ya mchuano wa CHAN. Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ilijikatia tikiti ya fainali baada ya kuilaza Guinea mabao 5-4 kwa mikwaju ya penalti.
Mechi hiyo ilikuwa imeishia sare ya moja kwa moja katika muda waziada baada ya Ibrahim Sankhon kuisawazishia Guinea kunako dakika ya mwisho ya kipindi cha pili cha muda wa ziada.

Lakini dalili za kufuzu zilionekana mapema,Ibrahim Bangoura alipokosa penalti ya kwanza ya Guinea. Kimwaki,Mika,Jonathan Bolingi,Gikanji,Mechak Elia walifungia Leopards ya DRC huku
Ibrahim Sankhon,Leo Camara,Kile Bangoura,Daouda Camara wakiifungia Guinea. Hata hivyo Kipa nambari moja wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo Vumi Ley Matampi aliokoa mkwaju wa penalti uliopigwa na Youla na kuipa DRC ushindi wa mabao 5-4 Guinea
Timu hizo zilitoshana nguvu muda wa kawaida na mechi ikaingia muda wa ziada uwanjani Amahoro, Rwanda. Ni katika muda wa ziada ambapo Jonathan Bolingi Mpangi kunako dakika ya 101 alifanikiwa kutikisa wavu wa Guinea.
Mapema kwenye mechi, mchezaji wa DR Congo Padou Bompunga alipewa kadi ya njano dakika ya 38. Hili lina maana kwamba hataweza kucheza fainali iwapo timu yake itafuzu.
Kipa wa DR Congo Ley Matampi pia alipewa kadi ya njano, kosa lake likiwa kunawa mpira nje ya eneo lake.
Rais wa Rwanda Paul Kagame ni miongoni mwa wageni mashuhuri waliohudhuria mechi hiyo. DRC sasa watasubiri hadi kesho kujua mpinzani wao kati ya Mali na Cote de Voire.
Mechi hiyo ya nusu fainali ya pili imeratibiwa kusakatwa katika uwanja wa taifa wa Kigali kuanzia saa kumi jioni saa za Afrika ya kati.



Read More